Tafadhar soma hapa, mchango wako wa mawazo wahitajika. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tafadhar soma hapa, mchango wako wa mawazo wahitajika.

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by BIF, Aug 7, 2012.

 1. BIF

  BIF Member

  #1
  Aug 7, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ebana mi naomba mnipe mawazo juu ya ili swala la interview kufanyika kwa lugha ya kigeni(English) Wote tunajua fika Watanzania walio wengi icho kizungu ni cha kubabaisha babaisha na hii ni kutokana na mfumo wetu wa Elimu ulivyo, wengi wetu tumepitia kwenye izi shule za wakina "kayumba" na Sec vilevile tulikua tunaongoza kuvaa lile bango la Swahili speaker.Uwa nalitafakali hili alafu nashindwa pata jibu ina maana kigezo hasa cha kujua kua uyu mtu yupo sawa kwenye hii fani flan ni icho kizungu?.Twende kwenye ivi vyuo vyetu vikuu, wanafunzi walio wengi iicho kimombo hawakijui ipasavyo kama wabisha nenda kafanye Analysis chuo chochote kile utakuja kubaliana na mimi, sasa kama ni ivi kuna aja gani hasa ya kuwafanyia watu interview kwa lugha ya kigeni? na kama kuna ulazima basi huu mfumo tulionao sasa ubadilishwe watu wawe wanatumia kizungu toka vidudu(chekechea) na kuendelea sio mara shule ya msingi kiswahili tupu Sec kingereza.Kwa matazamo wangu wapo watu wazuri wenye sifa na uwezo wa kufanya makubwa katika Nchi hii lakini walishindwa shule (kufaulu)huko masekondari kwasababu ya Lugha, unajua swala la kuklemu si la mchezo nakumbuka wakati nipo "O level" mambo yalikua mazito mtu unashinda ukiimba definition ya History na masomo mengine, ebana huku ni kama kutesa wanafunzi wa kitanzania na ndo matokeo yake tunapata makanjanja kwenye kila kona kwasababu wengine waliibia ibia tu kwenye mitihani.Wengi wanashindwa majalibio kwasababu ya lugha kujieleza kwa kizungu shida tupu ila mwambie kwa kiswahili atajieleza mpaka kesho.Sijui wenzangu mnalionaje ili?
   
 2. maria pia

  maria pia JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2012
  Joined: Jul 24, 2012
  Messages: 516
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  unhave a point mkuu,lkn kwa mfumo huu tulionao sio rahisi,cjui
   
 3. ummu kulthum

  ummu kulthum JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 2,791
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  1. si elewi kabisa kuna sababu gani ya kuendelea kufundisha kiswahili mashuleni wakati mahitaji ni lugha ya english
  2. kwa nini wanatutesa kupata kazi kwa kigezo cha kutojua ung'eng'e
  3. napata shida kuamini kwamba yeyote anayejua ung'eng'e ndio mchakazi na anajua kazi
  4. sie tunajifunza lugha yao kwa kukariri na kwa lazima je wao wanafanya hivyo
  5. af tunatabia ya kusifia vya wenzetu na kukashifu vya kwetu mfano mzuri ni humu humu jf kama unabisha fanya hata leo hili zoezi andika kwa kiswahili ukosee maneno karibu yote hakuna mtu yeyote atayejitokeza akwambie umekosa sasa andika kwa kizungu af ukosee utapata majibu ya ajabu ivi kwa nini hatupendi vya kwetu?
   
 4. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #4
  Aug 9, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Ki English ni tatizo kubwa itabidi tuamue moja.
   
 5. S

  Shuju Member

  #5
  Aug 9, 2012
  Joined: Jun 22, 2012
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  ndugu yang n kero ya weng bt hata 2meshaulizana sana imekuwa kzngmkuti yan nalo labda kwe kura za maon katba mpya
   
 6. kvelia

  kvelia JF-Expert Member

  #6
  Aug 10, 2012
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 247
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mkuu unachosema ni ukweli mtupu. Wenzetu wenye lugha hawashindwi usail, wanashindwa kuelewana kwenye mshahara. Huu mfumo ni mbaya sana, cha msingi mimi na wewe tujifunge ili tuwasomeshe watoto wetu ili waweze kupambana na hili soko linaloongozwa na Lugha ya Kiingereza.
   
 7. yaser

  yaser JF-Expert Member

  #7
  Aug 10, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 1,373
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  halafu kuna changamoto cku hizi wanatuweka kwenye soko la ajira la afrika mashariki wakati inajulikana fika kua nchi zote za afrika mashariki zko fiti kwenye lugha ukiondoa bongo.hawa jamaa watatuonea sana.
   
 8. BIF

  BIF Member

  #8
  Aug 11, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unajua nini, hii Nchi kuna viongozi ambao awastahili kuwa viongozi kwa kua wao watoto wao wanasoma uko maulaya hawahangaiki na wananchi maskini,yani ni wabinafsi sana hawa viongozi wetu.Nilishawahi kumsikia Prof mmoja wa chuo kikuu cha Dsm akisema kuwa walishafanya mchakato wa kubadili silabasi za masomo yote ya Sec kuwa ktk kiswahili na walishaanza kutafasili baadhi ya masomo kua kwa kiswahili lkn uabaishaji wizara ya Elimu ndo unakwamisha haya pia nilishawahi kusoma hisoria ya mwalimu mmoja raia wa uingereza alisema yeye amejifunza kiswahili toka yupo kwao na alikipenda sana alipo pata nafasi ya kuja TZ akajifunza zaidi na sasa ni mwalimu wa Kiswahili na akasema ili mwanafunzi akuelewe vzr ni lazima umfundishe kwa lugha anayoilewa.Sasa mi naishangaa hi Nchi tutaendelea kuyumbayumba mpaka lini jamani.
   
 9. Papa Mopao

  Papa Mopao JF-Expert Member

  #9
  Aug 11, 2012
  Joined: Oct 7, 2009
  Messages: 3,353
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 180
  Karibu wote mmenena sawasawa, nilishawahi kufanyiwa interview na Mkenya, uzuri alitumia lugha mbili kama nilivyoandika kwenye CV, yaani kiswahili na kiingereza. Sasa pale alipoona nashindwa kumuelewa katika kiingereza akanitelemshia kiswahili vizuri sana na nilimjibu vizuri sana kiasi kwamba tulielewana vizuri sana mpaka unafuu wa kwenye mawasiliano ulipendeza.

  Tatizo sisi wengi wetu tumefundishwa kukariri kujua kiingereza tu kuliko kujua jinsi ya kufanya kazi, na jinsi ya kuwa mfanyakazi kamili na utakavyotoa mchango wako ukiwa kama mwajiriwa wa kampuni husika, kwa njia hiyo naamini kabisa mtu atakuwa mfanyakazi bora mwenye mchango mzuri kwake yeye binafsi, kwa ofisi anayofanyia kazi, taifa lake na duniani kwa ujumla.

  Ni hayo tu!
   
 10. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #10
  Aug 11, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Wewe jipange tu ukafanye interview kwa kiingereza maana ndo lugha ya wawekezaji na kama unavojua sasa hivi mpaka ardhi yetu tumewapa wageni so hata mkulima siku za usoni itatakiwa ajue kiingereza ili aweze kupata kibarua kwa mwekezaji wa kilimo cha mahindi
   
 11. d

  dorroh New Member

  #11
  Aug 12, 2012
  Joined: May 26, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mnh kuna kazi kwa kweli..
   
Loading...