Tafadhalini wataalamu wa desktop msaada

idrisa S

Member
May 20, 2019
45
12
Mimi nina desktop yangu aina ya Dell. Ila tatizo lake silijui maana nikiwasha inawaka ila haitoi picha kwenye monitor.
 
Angalia VGA cable( Una Rangi ya Blue) km imechomekwa vizuri au pia ureciprocate huo waya yaan ulipochomeka kwenye desktop rudisha CPU and viceversa
 
Jaribu kuangalia ka Video graghics array cable kama ni nzima
Vilevile angalia ram kama zipo vizuri tatizo likiendelea jaribu kuweka graphics card
 
Anzana na VGA kuuchomoa na kuurudisha Ikishindikana niambie nikupe njia nyingine
 
Mimi nina desktop yangu aina ya Dell. Ila tatizo lake silijui maana nikiwasha inawaka ila haitoi picha kwenye monitor.
Hiyo mashine haiwaki . Inawaka nusu.

Swali. Je ikiwaka pale kwenye desktop unapowashia pana taa ya signal inatakiwa ikiwaka inaanza orange halafu inakuwa kijani. Sema kwako ikoje. Hii haijalishi monitor/screen ipo au haipo. Inatakiw iwe kijani . Leta mrejesho hapa.
 
Kujua kama ishu iko kwenye monitor au processor unit, jaribu kutumia monitor nyingine.
Ikifanya kazi basi ni ishi ya monitor au vga yako kama nayo haiwaki basi ni ishu ya kwenye processing unit..
 
taa ipo ila inawakaga ya njano2
 
Kujua kama ishu iko kwenye monitor au processor unit, jaribu kutumia monitor nyingine.
Ikifanya kazi basi ni ishi ya monitor au vga yako kama nayo haiwaki basi ni ishu ya kwenye processing unit..
yaani nilibadilisha monitor lakini bado inazingu ila nilivyo ifungua kuiangalia niliona kapasta 1imevimba je linaweza kuwa ndo tatizo?
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom