Vyamavingi
JF-Expert Member
- Oct 3, 2014
- 6,071
- 5,983
Jana inadaiwa kuwa Maaskofu wa CCT na TEC walikwenda kujitambulisha Ikulu kwa Rais. Vyombo vya habari ikiwa TBC1 ktk taarifa ya habari ya usiku viliripoti juu ya Maaskofu kwenda Ikulu kujitambulisha!
Magazeti ya ikiwamo Mwananchi, limepambwa na picha na maelezeo kuwa Maaskofu walikwenda kujitambulisha!
Binafsi, nikiwa Mtanzania mwenye akili kamili, nimekwazwa na lugha ya kudhalilisha ya waandishi wa Ikulu wakidai kuwa Maaskofu walikwenda kwa rais kujitambulisha! Lugha iliyotumika ina walakini mkubwa. Maelezo ya waandishi wa Ikulu, yanataka kuwaaminisha Watanzania kuwa rais wetu bado mgeni na Maaskofu na kuwa hajawadahamu wakati tunajua wazi kuwa rais wetu ni muumini wa Kikristo, amebatizwa amepata ubarikio na husali katika Makanisa hayo na ni waandishi haohao ndiyo huripoti na kupiga hata picha rais akiwa anasali ktk makanisa hayo ambamo hukaribishwa na Maaskofu haohao ambao rais 'hawafahamu' bado.
Pili, waandishi wa Ikulu wanataka kuwaaminisha Watanzania kuwa Kanisa/Maaskofu ni 'kitu kidogo' tu mbele ya rais kitu ambacho sio sahihi na ni dharau kwa Kanisa maana Madhabahuni ni mahali patakatifu, ndiyo maana hata rais ambaye ni muumini wa kikristo hupiga magoti, kusimama na kuketi sawa na waumini wengine. Madhabahuni hakuna aliye mkuu, wote tuko sawa mradi tumeamua kwa hiyari kwenda Ibadani.
Niwashauri tu waandishi wa habari wa Ikulu wawe na staha na kujiepusha na spinning, maelezo waliyotupa yanamkweza sana rais wetu juu ya kanisa na kulidunisha Kanisa na Maaskofu wetu mbele ya umma. Taarifa waliyoitoa kwenye ziara ya Maaskofu Ikulu wameipotosha, ingetosha kusema Rais aliwaalika Maaskofu au Maaskofu wamtembelea Rais na sio kupotosha kuwa walikwenda kujitambulisha.
Yesu alisema, "chachu kidogo tu huchuchisha donge zima". Muwe makini, uhusiano kati ya Serikali na Madhehebu ya dini umejengwa katika misingi ya kuheshimiana.
Vv