Manyerere Jackton
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 2,438
- 4,454
Ndugu zangu, mke wangu anasumbuliwa na maradhi ya diabetes (kisukari). Anatumia dawa za Gema II. Zimemsaidia kiasi kwamba, pamoja na masharti ya vyakula, kiwango cha sukari sasa ni 5 hadi 7. Hiki si kiwango kibaya sana.
Tatizo moja kubwa linalompata kwa miezi zaidi ya sita sasa ni maumivu makali sana kweny miguu yote miwili. Maumivu hayo yanaanzia kwenye nusu ya unyayo kuelekea kwenye vidole vya miguu yote (yaani yako nusu unyayo tu). Anahisi moto ukiwaka sehemu hizo. Amepimwa na kuambiwa kapungukiwa calcium. Katibiwa MOI na hospitali nyingine nyingi, lakini hakuna mafanikio.
Hivi niandikapo taarifa hii, analia kwa maumivu makali. Naomba sana msaada wenu wadau. Naamini Jukwaa hili lina wataalamu wa kila aina.
Endapo yupo wa kunisaidia, naomba tuwasiliane kupitia 0759488 955.
Natanguliza shukrani za dhati.
Ndimi,