Tafadhali ndugu zangu naomba mnisaidie. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tafadhali ndugu zangu naomba mnisaidie.

Discussion in 'JF Doctor' started by kasitile, Oct 16, 2011.

 1. kasitile

  kasitile Member

  #1
  Oct 16, 2011
  Joined: Feb 22, 2011
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Poleni na majukumu ya kila siku wadau.

  Naomba mnisaide wadau.Mke wangu ana mimba ya mwezi mmoja na nusu.Lakini tatizo kubwa ni kwamba anaumwa sana kiuno na tumbo na damu kidogo kidogo hutoka.Hali hii inatuchanganya sana,na kwa kuwa niko mbali sana na sehemu za huduma,hivyo kabla sijaanza safari ya kwenda mjini,naomba kama kuna mtu anajua chochote kuhusu hilo anisaidie.Natanguliza shukrani.
   
 2. tunalazimika

  tunalazimika JF-Expert Member

  #2
  Oct 16, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,100
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  nakushaur uende hospitali ya karibu kwa uhakika zaid, mimba zina complecations nying ndugu yangu hasa kama ni ujauzito wa kwanza
   
 3. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  nakushauiri umPM dokta riwa anaweza kukupa ushauri wa kitaalam zaidi.
   
 4. kasitile

  kasitile Member

  #4
  Oct 17, 2011
  Joined: Feb 22, 2011
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakushuru kwa ushauri wako mdau.
   
 5. kasitile

  kasitile Member

  #5
  Oct 17, 2011
  Joined: Feb 22, 2011
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante mkuu kwa ushauri wako
   
 6. ram

  ram JF-Expert Member

  #6
  Oct 17, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 6,194
  Likes Received: 898
  Trophy Points: 280
  Kwa hizo dalili huna haja ya kusubiri, mpeleke hospitali, tena mpeleke kwa Dr. specialist wa magonjwa ya akinamam, mpe pole but Mungu ni mwema pia tamsaidia
   
 7. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #7
  Oct 17, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  anahitaji kupumzika zaidi,wakati huo ukifanya mpango wa kumpeleka kwa dr bingwa wa wanawake. apate total be rest,kwa maana alale flat wakati wote, akitoka kitandani ni toilet tu, akiketi kitandani ni kula tu! pole,mungu ni mkubwa, atawajaalia. ni muhimu kumuona dr kwa sababu huenda akahitaji kulala tu hadi ikifikisha miezi sita,kama ana fanya kazi ya kuajiriwa atahitaji maandishi.
   
 8. kasitile

  kasitile Member

  #8
  Oct 17, 2011
  Joined: Feb 22, 2011
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nashukuru ndugu yangu kwa ushauri wako!Asante sana
   
 9. kasitile

  kasitile Member

  #9
  Oct 17, 2011
  Joined: Feb 22, 2011
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante ndugu yangu,Mungu akubariki
   
 10. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #10
  Oct 17, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Pole ndugu,
  Bleeding kwa mimba iliyo chini ya miezi saba mara nyingi husababishwa na abortion ingawa tatizo lolote la kwenye njia ya uzazi laweza kusababisha bleeding. abotion ziko za aina nyingi kutegemeana na status ya shingo au njia ya kizazi (cervix) na kuwepo au kutokuwepo na uterine contractions (ikiambatana na maumivu ya tumbo).

  Kuna threatened abortion, hii ni ile ambayo mimba haijatoka lakini inatishia kutoka, ambapo cervix inakuwa imefunga, lakini damu zinatoka huwa si nyingi sana, tumbo linaweza likawa linauma au lisiume.

  Pia kuna incomplete abortion, hii ni kwamba abortion imetokea lakini kuna sehemu fulani ya kiumbe au kondo la nyuma imebaki ndani kwenye tumbo la kizazi. hapa bleeding huwa inakuwa nyingi, cervix huwa imefunguka na unaweza kushika sehemu ya kiumbe au kondo unapompima mama na tumbo linauma.

  Kuna complete abortion ambapo mimba imetoka yote, damu haitoki tena, njia imefunga na tumbo limeacha kuuma.

  Kuna aina nyingine kama missed abortion ambapo kiumbe kimefia tumboni lakini hakuna kitu kilichotoka, njia imefunga na damu mara nyingi huwa haitoki au ikitoka ni kidogo sana, na tumbo haliumi. Pia kuna septic abortion nk.

  Matibabu inategemea na aina ya abortion.

  Mkeo nadhani anaweza kuwa na threatened abortion (mimba inatishia kutoka), anaweza pia kuwa na aina nyingine za abortion kutegemeana na status ya cervix au tatizo lingine.

  Kitu cha Muhimu sana kwa sasa ni kufanya mpango wa haraka aende hospitali kwa njia ambayo haitamtikisa sana ili akachunguzwe ijulikane ni aina gani ya tatizo linalomsumbua ili apate matibabu sahihi, sisi hapa tunakupa ushauri kwa hisia lakini akionwa hospitali tena haraka itasaidia kusaidiwa kwa uhakika. Bleeding sio jambo dogo, tafadhali usimtibu nyumbani hizi measures tunazokushauri ni za kufanya wakati haraka una-arrange kumpeleka hospitali.

  Kitu cha kumsaidia kwa sasa kama ni threatened abortion ni kama alivyoshauri King'asti kwamba apate complete bed rest, wakati mnapanga mipango ya kumpeleka hospitali, umuangalie sana kiasi cha damu kinachotoka (uendelee kumonitor bleeding), mpatie dawa za maumivu, ningeshauri paracetamol, wengine huwa wanatoa dawa za kufanya kizazi kisi-contract kwa ajili ya kuzuia mimba isitoke, kama salbutamol ingawa kwa mimba ndogo uwezo wake wa kufanya kazi bado ni debetable. Hospitali watakupa pia dawa kama duphaston ambazo hufanya kazi ya kuzuia mimba isitoke kwa wale akina mama ambao corpus luteum yao imeshindwa kufanya kazi mapema kabla placenta haijaanza kutengeza hormone ya progesterone ambayo ndiyo hu-maintain pregnancy. Duphaston hufanya kazi ya progesterone. Na matibabu mengine utayapata kutegemeana na tatizo.

  Pole na kila la kheri.
   
 11. kasitile

  kasitile Member

  #11
  Oct 17, 2011
  Joined: Feb 22, 2011
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nashukuru sana ndg yangu kwa maelezo yako ambayo yamenipa mwanga.Nitajitahidi sana kuzingatia yote hasa kwenda Hospitali.Nashukuru sana na Mungu akubariki.
   
 12. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #12
  Oct 18, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  ww! yaan bado uko hapa??? unatafuta nn kimbia hosp haraka! kufumba na kufumbua nisikuone!!!
   
 13. S

  Shadya Member

  #13
  Oct 18, 2011
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 88
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kweli face book unafaa kuangalia familia
   
Loading...