Ndugu zangu nahisi naibiwa sio kwa miamala hii. Wenye ujuzi mnisaidie

Smart Contract

JF-Expert Member
Sep 24, 2014
1,016
2,406
Wasaalam!
Poleni kwa majukumu, moja kwa moja kwenye mada naomba mnisaidie kwa mnaojua hizi aina za miamala (kwenye picha)
Kuna huu muamala CRDB wanaita
TMS Cash Withdrawal
Desc. Persanal Cash withdrawal
Naomba kujua ni muamala wa aina gani maana kuna kiasi cha pesa 300k nilipokea, nasikutoa hata mia kwa sababu kwanza hata text haikuja kwamba nimepokea hela na hii si kawaida.
Lakini nilipokuja kuangalia bank statement niliona kuwa hiyo 300k iliingia lakini, 200k ilitokewa kwa aina ya muamala niliouorodhesha hapo juu.
Naomba wenye uelewa huu ni muamala wa aina gani wanijuze nahisi kuibiwa kama sio na watu niliowaamini basi ni benki.
Natanguliza shukrani
 
Attachments

  • _20230722_125844.JPG
    _20230722_125844.JPG
    78.1 KB · Views: 9
Nenda branch watakupatia majibu.
Ila uwe na uhakika hakuna mtu mwenye password yako ambae anaweza kua alitumia card yako.

Ukiemda branch watakwambia hiyo hela ilitolewa wapi na ilitolewa kwa njia gani, wakala, mobile money ama atm na nani alitoa.
Ndio maaana nikataka nijue huu muaala sijui TMS ni wa aina gani .? Yaani ni withdrawal kwa wakala, atm au benki
Maana nilitingwa na ulcers hata kutembea siwezi, kuna mtu wangu wa karibu nilimpatia password na kadi akanitolee akatoa na risiti akanipa lakini text haikurudi na sikawaida maana miamala mingine ilopita pia text hazikufika.
 
Ukienda lalamika watakuambia wewe ndio unataka kuiibia benki maana unaikana miamala yako mwenyewe
Duh
Siwezi kwenda kulalamika nitaenda kuomba ufafanuzi, huwezi jua nlitoa nikiwa bwiii (autopilot) nikapiga round bar
 
Ndio maaana nikataka nijue huu muaala sijui TMS ni wa aina gani .? Yaani ni withdrawal kwa wakala, atm au benki
Maana nilitingwa na ulcers hata kutembea siwezi, kuna mtu wangu wa karibu nilimpatia password na kadi akanitolee akatoa na risiti akanipa lakini text haikurudi na sikawaida maana miamala mingine ilopita pia text hazikufika.
hapo kuna walakini, lakini nenda tu watakupatia maelezo na wala hawatakufikiria lo lote.
 
Back
Top Bottom