Tafadhali kwa watanzania wanaoishi Marekani pita hapa

Status
Not open for further replies.

cadey

JF-Expert Member
Oct 14, 2014
1,455
4,412
Naomba Msaada kwa wenu kwa wale wenye uzoefu na hili jambo,
Nimeshinda iyo dv lottery 2016/2017 nilichaguliwa kwenye second selection September,
Sasa Nipo njia panda niendelee na process au nipotezee,nasikia maisha ya marekani magumu sio kama zamani na Kazi pia hazipatikani kirahisi, naogopa nisije kujuta .. Nina miaka 32 ,nimeoa na Nina mtoto mmoja 3yrs old,Nina biashara na nimefanikiwa kujenga nyumba.
Na sasa maisha bongo ndo yanazidi kuwa magumu na biashara pia ngumu,naombeni ufafanuzi kuhusu maisha ya marekani,.
Nahitaji kufanya maamuzi yaliyo sahihi..
NATANGULIZA SHUKRANI ZANGU .
 
Kupanga ni kuchagua... Hizo mikitu labda kama hutoi pesa... na wewe hiyo ushaambiwa ati second na bado hujachaguliwa unajiona Tayari kabisa kha!

Usije Mkuu Trump hataki wazembe
 
Natamani lakini naogopa nisije jutia baadae,naona nifanye research kabla sijaamua, watu wanasema maneno mengi kuhusu Maisha ya marekani
Wewe unaonekana ni mtoto wa mama, yaani kula kulala.
.
Hata Kama Marekani kuna maisha magumu, je? Utafananisha na maisha ya Tanzania Chini ya ccm?
Ugumu wa maisha wa marekani una afadhali mara 100,000 kuliko bongo.
wala hukupaswa kuhoji, Marekani ktk majimbo yote 51 hakuna mfanyabiashara aliyefunga biashara eti Kwa Sababu ya kubambikiwa kodi au mzunguko mbovu wa pesa.
Marekani hakuna mwanaharakati aliyepotea Kwa Sababu ya kumkosoa Rais.
Bongo ni Jehanamu bana asikuambie mtu, kwanza hukupaswa kuhoji humu ungejiondokea zako kimya kimya tu, humu kuna mi ccm ina laana itakukatisha tamaa.
Yaani kwenda USA baby hadi unataka ushauri?
Aisee hiyo bahati na ije kwangu jamani,siye tunaishia vinchi vya Africa tu, halafu wewe unaleta mapozi...
 
Ungekuwa peke yako mkuu ningekushauri uende, Bahati mbaya Una familia mmnh kama Una uhakika wa kula hapo ulipo, mie nakushauri utulie, naskia trump hataki mchezo na wageni lol,sina sababu ila sikushauri uache familia uende lol labda umesoma na Una uhakika wa kupata kazi nzuri huko lol, kwa uhakika zaidi muone lemutuz
 
Naomba Msaada kwa wenu kwa wale wenye uzoefu na hili jambo,
Nimeshinda iyo dv lottery 2016/2017 nilichaguliwa kwenye second selection September,
Sasa Nipo njia panda niendelee na process au nipotezee,nasikia maisha ya marekani magumu sio kama zamani na Kazi pia hazipatikani kirahisi, naogopa nisije kujuta .. Nina miaka 32 ,nimeoa na Nina mtoto mmoja 3yrs old,Nina biashara na nimefanikiwa kujenga nyumba.
Na sasa maisha bongo ndo yanazidi kuwa magumu na biashara pia ngumu,naombeni ufafanuzi kuhusu maisha ya marekani,.
Nahitaji kufanya maamuzi yaliyo sahihi..
NATANGULIZA SHUKRANI ZANGU .
Kama wewe ni mpiganaji, basi tambua umelamba bingo.
 
Kama una uwezo na una mtu wa kukupokea tangulia ww kwanza ukaangalie mambo yakoje then baadae ndio family ikufuate. Inachukua miezi kadhaa kabla hujasettle hivyo jiandae kwa hilo, lakini pia angalia kama biashara unayofanya inalipa(mfano faida ya kama million 2 kwa mwezi) then baki au mwachie wife kwa sasa
 
Hongera sana mkuu hiyo ni bahati iliyoje. Usiache ipite as you will always wonder what-if. That said, please note maisha ugenini si mchezo, especially kama huna box la maana. My advice to you is go by yourself and taste the waters first, ndio ujipange kuhusu familia (approx. year or so). However, do so if and only if;

  • Una mwenyeji realible and/or savings ya kueleweka to help support you (for at least 6-8 months) ukifika huko
  • You are not afraid of work (mambo ya sijui mimi nilikuwa nafanya ofisini, ni branch manager and blah blah forget it)
  • Your wife is able to financially support the family in your abscence. This way if things don't work out you can come back to a somewhat comfortable life.
 
USA baby....

20161231_150734.jpg
 
Kupanga ni kuchagua... Hizo mikitu labda kama hutoi pesa... na wewe hiyo ushaambiwa ati second na bado hujachaguliwa unajiona Tayari kabisa kha!

Usije Mkuu Trump hataki wazembe

Nimechaguliwa tayari ,natakiwa niendelee na Hatua zinazofuata ili kupata visa
 
Wewe unaonekana ni mtoto wa mama, yaani kula kulala.
.
Hata Kama Marekani kuna maisha magumu, je? Utafananisha na maisha ya Tanzania Chini ya ccm?
Ugumu wa maisha wa marekani una afadhali mara 100,000 kuliko bongo.
wala hukupaswa kuhoji, Marekani ktk majimbo yote 51 hakuna mfanyabiashara aliyefunga biashara eti Kwa Sababu ya kubambikiwa kodi au mzunguko mbovu wa pesa.
Marekani hakuna mwanaharakati aliyepotea Kwa Sababu ya kumkosoa Rais.
Bongo ni Jehanamu bana asikuambie mtu, kwanza hukupaswa kuhoji humu ungejiondokea zako kimya kimya tu, humu kuna mi ccm ina laana itakukatisha tamaa.
Yaani kwenda USA baby hadi unataka ushauri?
Aisee hiyo bahati na ije kwangu jamani,siye tunaishia vinchi vya Africa tu, halafu wewe unaleta mapozi...
Mwanaharakati gani kapotea.??
 
Mi niko marekani mume wangu alipata hiyo green card inategemea na mji gan unaenda. Si tuko Massachusetts kazi zipo nyingi lakin ungekuja mwenyewe kwanza ujiandae vizur ndo uchukue familia baadae

Shukrani mkuu.. tutapata visa mimi na familia yangu itakuwa valid miezi 6,
Mji niliopanga kufikia ni Michigan ndo yupo mtu ambaye atanidhamini,sasa sijajua maisha ya jimbo hilo yapoje,
Kuhusu pesa ya kulipia visa na process zingine ipo na pesa ya kujikimu si haba nitakuwa nayo,naogopa nisije tumia pesa nyingi nikajutia ,
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom