Tafadhali hizi Kanzu Nyeupe nyingi Mitaani leo zifanye hata Roho zetu ziwe Nyeupe kwa Mungu hadi Funga ijayo 2022

Krav Maga

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
4,626
2,000
Ni matumaini yangu makubwa Krav Maga hivi ninavyopishana na Kanzu nyingi nyeupe Mitaani leo basi hata Wahusika nae kwa Miezi 11 ijayo nao Roho zao zitakuwa Nyeupe hivyo hivyo.

Ushauri wa bure wengine ambao huwa hampendi Kuvaa Kanzu au hamjazoea Kuzivaa basi muanze Kuchukua Mazoezi taratibu ya Kuzivaa kwani kuna baadhi nawaona Kanzu zimewavaa Wao hadi Kuwatambua imekuwa ni shida.

Nitoe Pongezi zangu kwa wale waliofunga Kweli, Wamesamehe yote, wamenialika Krav Maga kwenda kula Pilau na wamedhamiria kuacha Kutenda tena Dhambi zao ili wasimkere zaidi Mtume Mohammed ( SAW ) na Allah Mwenyewe.

Namalizia pia kwa Kuwaomba Wahusika ( hasa Vijana ) kuwa kule Kujazana Kwenu sana Ibadani Misikitini Kusihitimishwe rasmi leo bali baada ya Kula Pilau leo, kesho na kulimalizia Jumapili kuanzia Jumatatu tuendelee Kufurika Misikitini.

Krav Maga nawatakia wote Eid Njema.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom