Tafadhali akinamama msiwatamkie hili wanaume!!

Tafadhali akinamama msiwatamkie hili wanaume!!

Straight corner

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2010
Posts
385
Reaction score
132
Katika kukua kwangu nimegundua jambo baya ambalo mwanamke hatakiwi kumwambia mwanaume/mzazi mwenzie wakiwa wamekwazana ni kumtamkia kuwa "KWANZA HAO/HUYO MTOTO SI WAKO".
Kuna jamaa yangu kanisimulia kuwa mama watoto wake kamtamkia neno hili na kanieleza uamuzi anaotarajia kuuchukua, kweli ndugu zangu haijanipendeza kabisa na inasikitisha sana. Nimejaribu kumsihi na kumwambia kuwa amemtamkia sababu ya hasira tu (just to please him) lakini haonekani kuelewa somo, mkewe kakimbia nyumba hivyo jamaa kabaki na watoto tu na anasema akiwaona anawaonea huruma na anazidi kupta hasira zaidi. Ana siku tatu sasa hajaenda kazini analala na kuangalia TV tu.
Tafadhali akina dada/mama, msiwaambie neno hili wapendwa/waume wenu either ukimdanganya au ukimwambia ukweli kwani matokeo yake unaweza usiyatarajie kulingana tu na uvumilivu wa mhusika.
 
pole yake inategemea lkn kamwambia ktk mazingira yapi
 
MDADA: Unakunywa pombe?
MKAKA: Hapana
MDADA: Unavuta?
MKAKA: Hapana
MDADA: Una mademu?
MKAKA: Hapana MDADA: Sasa unajichanganyaje na washkaji?
MKAKA: Mi muongo ile mbaya
 
kwa kawaida huwa hatusemi huwa tunawakumbusha tu jinsi mlivofanana na watoto wenu!
po
 
Anasema walikuwa na ugomvi, sikumuuliza ulihusu nini! Lakini simnajua kwenye ndoa kuna milima na mabonde!
yaah najua kuna mabaya yake lkn angepaswa kua mvumilivu na kukaa chini wakaookangea ndo hatua nyingine zingechukuliwa sizani kama ingefikia hatua kama hiyo ya mwanamke kuonda bila kufikia muafaka inakuaje
 
A-Z Maumivu........ kinachouma ni kuchezewa kihisia muda wote huo + watoto umeshawaona kama wako ,ni ngumu sana kutengana nao ila ukishaprove kuwa siyo wako ni bora utengane nao kwa maana njemba hazichelewi kuja kudai damu zao.
ila inaumaaaaaaaaaa sana!
 
A-Z Maumivu........ kinachouma ni kuchezewa kihisia muda wote huo + watoto umeshawaona kama wako ,ni ngumu sana kutengana nao ila ukishaprove kuwa siyo wako ni bora utengane nao kwa maana njemba hazichelewi kuja kudai damu zao.
ila inaumaaaaaaaaaa sana!
Ni kweli inauma sababu nimejaribu kujiweka upande wake huyu jamaa nimejikuta niko katika wakati mgumu sana kimaamuzi! Usiombe yakukute!
 
Wewe si rafiki wa kweli
Yaani wewe ndo unamakosa na usirudie tena hata siku mmoja kumplease mtu kama ulivyo fanya. wewe una ushahidi gani wa mtoto, wala hujaweza kushuhudia waki do!! hata hujui mimba ilingia lini, pengine hata tarehe ya kuzaliwa mtoto hujui!!!Rafiki yako anaumia, mpe maneno ya faraja, uamuzi wake usiwe na madhara kwake binafsi. Ila usimwambie kuwa kaambiwa kwa hasira, na et haina maana!! nope. Inasemekana mtu akilewa, akifurahi, au kukasilika anaongea ya moyoni.
Mwenye kujua mtoto wa nani, ni mwanamke tu, period. kama kasema kwenye ugomvi basi ni ukweli, period. jamaa yako afanye vile itafaa.
Ushauri, Uamuzi wake usiwe na madhara ya moja kwa moja kwa mtot0 (watoto) tajwa, maana hana kosa yeye anahusishwa tu.
Wakatabahu
 
kwa kawaida huwa hatusemi huwa tunawakumbusha tu jinsi mlivofanana na watoto wenu!
po

Duh,kumbe ndo maana nikiwa namtazama dogo mamake ananiwahi ananiambia kuwa tunafanana!

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
huyo mwanamke nae kiazi, hajui maneno hayo yataathiri hata mustakabali wa watoto?
 
tumekoma hatuwaambii tena tutawaacha tu mlee watoto wa wenzenu
 
Wala asifanye chochote kile kwasababu kaambiwa ukweli,
Je angekaa miaka yote huku akihudumia viumbe ambavyo si damu yake na baadae kujua kutoka kwa watu wengine ingekuaje??
 
Labda kuna neno alimtamkia mkewe likamuma.
Ndio maana mwanamke akatamka neno kama hilo kwa mumewe, ili amumize nae pia. (Ndio wanawake walivo)
Kama wainge kua si wa mumewe hasinge waacha kwa mumewe.
 
huyo mwanamke nae kiazi, hajui maneno hayo yataathiri hata mustakabali wa watoto?

Ulichoongea BT ni kweli, wengi wa wanandoa hawapendi kujishusha, kila inapotokea mikwaruzano kila mtu huvimba kichwa na ile kauli ya "liwalo na liwe" ndio hutamalaki...
am damn sure kuwa hao watoto/mtoto si wa huyo jamaa...surely that's a naked truth!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom