Tache maneno: DED wa Itigi ni msomi

Tache maneno: DED wa Itigi ni msomi

Ukiwa nje ya taasisi ya halmashauri unaweza kuona kama ni kataasisi kadogo, lakini ukweli inahitaji mtu makini na mwenye uzoefu katika utawala wa umma kuna wakuu wa idara wenye uzoefu mkubwa, na ndio maana waliotangulia waliweka vigezo vya ukurugenzi ktk wizara na halmashauri, lakini kwa kuwa mfalme ameamua kuja na utaratibu wake sisi yetu ni macho, ila kwa maoni yangu na ninavyozifaham kazi za ukurugenzi ktk halmashauri kwa wengi wa wateule naona giza nene mbele, tusubiri panga pangua nyingine
 
Hii ya mwisho 2015 kugombea ubunge na kushindwa kura za maoni ndio bora kuliko zote hapo juu kwa awamu hii ya 5, angekuwa hakugombea ubunge hyo elimu yake isinge mpa hiki cheo, awamu ya wanaharakati kukamata fursa za ajira serikali, degree masters ni mbwembwe tu kwa awamu hii.
 
image.jpeg

Huyu ndio Luhende Pius Gerald,Mkuruganzi mpya wa Wilaya ya Itigi Mkoani Singida.Luhende alizua mjadala kwenye mitandao ya kijamii kwa kusemekana kuwa ni msomi wa ngazi ya Cheti cha Hotel Management na ni meneja wa City Style Hotel pale Sinza.

Leo Rais amesisitiza apigwe picha yeye na huyo wa Sinza na zisambazwe.Punde italetwa picha ya cheti chake cha Masters alichoonyesha hadharani Ikulu Dsm ili kukata mzizi wa fitna.

Kila la kheri Luhende....Salamu kwa watu wa Itigi na Singida kwa ujumla
 
UKAWA leo wameaibika hadi basi.
Ushauri wangu ni kuwa atafute wanasheria awaburuze mahakamani magazeti,radio na Tv zote zilizotangaza kuwa yeye ni meneja wa baa mwenye cheti cha hoteli menejimenti na awadai fidia ya mabilioni kwa kumdhalilisha.

Hii itasaidia vyombo vya habari kuwa makini kabla ya kuchapisha habari
 
Ushauri wangu, ajipange atekeleze ilani ya chama cha mapinduzi. Miezi minane imeshapotea hivyo.
 
Hivi kiwa msomi ni lazima uwe na machapisho?

Kwa imani yangu naamin kuwa msomi ni yeyote kwanza anaye jua kusoma na kuandika lugha yake ya taifa na kuielewa na pia anajua kuhesabu na kukokotoa hesabu za kawaida kama +, - /, * na pia anakuwa mbunifu na mwenye mawazo chanya kwa maendeleo yake binafsi,na ya jamii yake na ya watu wanao mzunguka na taifa kwa ujumla. Huyo kwangu mimi ndiyo huwa namuona msomi,

Usomi kwangu sio vyeti vya degree,masters ,PhD nk.maan wapo wengi wenye vyeti hivi lakin wanaprove failure kwa mambo hata madogo na ambayo hayahitaji vyeti kila uchwao utadhan hawana elimu kabisa hata ya awali zaid ya utu uzima.
Kama maprof wa TZ
 
Ukisikia Halmashauri wengine wanaona ni kataasisi kadogo sana, na mtu yeyote anaweza kujifunza jinsi ya kuongoza. Tukijikwaa tusiulizane nani mchawi wa maendeleo yetu. Ukiangalia CV ya huyo msomi unajiuliza, je inajitosheleza kiuzoefu?
Nadhani awali walishaweka vigezo vya kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri na walikuwa na sababu zinazojitosheleza. Hilo walilifanya baada ya misuguano mingi na mamlaka za uteuzi zikafikia muafaka wa kuainisha vigezo.
Lakini leo tunaleta siasa kwenye taaluma na taratibu za ukweaji wa madaraka. Tusiseme sana, ngoja tusubiri sie yetu macho na masikio.
Watu wameendekeza ukada wameteua maDED majingamajinga ndio yanafanya mambo ya kipumbavupumbavu
 
Kuwa mwalimu wa ngazi ya secondari sio kigezo cha kuto pewa madaraka. Hoja ya msing je?? Walio pewa madaraka hayo wana kidhi na wana uwezo wa kumudu majuku yao katika nafasi hizo walizo pewa? Na ili uwezw kujua utendaji wake huwezi kutumia kigezo cha kuwa mwalimu wa sec kuwa atashindwa kutekeleza majukumu yake, nadhan hapa upo wrong.huenda utendaji kazi wake ni zaid ya hicho cheo kipya alicho pewa sasa ambacho wewe unaona kimempwaya.
Bado unamtetea tena huyu mpumbavu mwenzako
 
Namfahamu shija ni msomi sana. Jamaa yuko smart. Niklikuwa naye pale chuo kikuu tukifanya degree yetu ya kwanza pamoja. Ni mtaratibu, mtu makini na asiye na papara.
We jamaa ni.muongo sana huyo jamaa amejitanabaisha hana sifa hivo ulizompamba.
Tatizo mmeendekeza ukada wa kuchagua watu kwenye vyeo vyenye changamoto bila kufata vigezo.
Mojawapo ya kigezo cha kuteuliwa nafasi ya uongozi serikalini ni kufikia cheo cha Principal kwenye kada yako na lazima uwe umefanya kazi serikalini kwa.muda wa zaidi ya miaka 12.
Ofisi ya menejimenti ya utumishi wa umma ilikuwa ina pool ya watendaji wazuri waliokuwagroomed ili wawe viongozi. Na ambao wamefanya kazi kwa zaidi ya miaka 12.

Jiwe kaingia madarakani kawatupilia.mbali kaamua kuweka maded wake kama huyu kisa ukada na ukabila.
Namshangaa sana mwalimu wangu Dr Ndumbaro na material yake ya meritocracy in promotion and appointment anakubaliana na upuudhi anaolazimishwa kuteua watu kisa ukada kweli njaa mbaya hata kwa wasomi.
Sasa ona matokeo ya vitu wanavyofanya
 
UKAWA leo wameaibika hadi basi.
Ushauri wangu ni kuwa atafute wanasheria awaburuze mahakamani magazeti,radio na Tv zote zilizotangaza kuwa yeye ni meneja wa baa mwenye cheti cha hoteli menejimenti na awadai fidia ya mabilioni kwa kumdhalilisha.

Hii itasaidia vyombo vya habari kuwa makini kabla ya kuchapisha habari
Sasa huyu mpuudhi mwenzako ndio ataburuzwa mahakamani
 
LUHENDE PIUS GERALD SHIJA MKURUGENZI MPYA WA ITIGI.

* Pius alimaliza Sekondari O' level Kilosa Sekondari ( 1990- Kizunguzi), akaenda form six kisha diploma, akawa mwalinu wa sekondari.

* Mwanzoni mwa miaka ya 2000 akawa Mkaguzi wa shule huko shinyanga. 2005-2007 Alikuwa akisoma diploma in education management and administration (ADEM-BAGAMOYO).

* Mwaka 2008 akaenda ARUSHA UNIVERSITY, alipomaliza akapelekwa ukaguzi kanda ya Tabora-Kigoma.

* Mwaka 2013 Alianza Masters of Education in educational planning and administration- JORDAN UNIVERSITY.

Mwaka 2015 alihamia ukaguzi kanda ya mashariki. Na aligombea ubunge jimbo la Kishapu akashindwa kura za maoni.

**************************

Duh

Hii ni shule au mahangaiko?

This guy is a zero brain!

I'm sorry,deal with it!
 
Sasa kuna uaomi gani hapo?
LUHENDE PIUS GERALD SHIJA MKURUGENZI MPYA WA ITIGI.

* Pius alimaliza Sekondari O' level Kilosa Sekondari ( 1990- Kizunguzi), akaenda form six kisha diploma, akawa mwalinu wa sekondari.

* Mwanzoni mwa miaka ya 2000 akawa Mkaguzi wa shule huko shinyanga. 2005-2007 Alikuwa akisoma diploma in education management and administration (ADEM-BAGAMOYO).

* Mwaka 2008 akaenda ARUSHA UNIVERSITY, alipomaliza akapelekwa ukaguzi kanda ya Tabora-Kigoma.

* Mwaka 2013 Alianza Masters of Education in educational planning and administration- JORDAN UNIVERSITY.

Mwaka 2015 alihamia ukaguzi kanda ya mashariki. Na aligombea ubunge jimbo la Kishapu akashindwa kura za maoni.

**************************

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom