Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,011
- 9,879
Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) imekanusha taarifa iliyochapishwa na gazeti la Mwananchi iliyosema wafadhili wajitoa dawa za UKIMWI.
TACAIDS imesema taarifa hiyo si ya kweli hakuna wafadhili waliojitoa, kwa kuwa hadi sasa mahusiano ya Tanzania na wafadhili yako vizuri.
Wamesema taarifa sahihi ni kuwa kwa muda wa miaka 8 fedha za wafadhili zilipungua kwa baadhi ya mambo ya mapambano ya UKIMWI na hiyo sio kwa Tanzania pekee bali nchi zote zinazotegemea wafadhili.
Kutokana na hilo, serikali iliunda Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti UKIMWI(ATF) ambao umewezesha serikali kununua septrin kwa miaka mitatu mfululizo.