Uchaguzi 2020 Tabora: TAKUKURU kuwakamata Wanasiasa walioanza Kampeni kabla ya muda, Aden Rage kashadakwa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Salaam wakuu,

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mkoani Tabora, imewaonya wanasiasa wote wanaofanya Kampeni kabla ya muda wa kisheria waache mara moja kufanya kampeni na kutoa Rushwa kwani ni kinyume cha Sheria.

Hivyo wataanza kukamatwa sababu Wanavunja Sheria.

Habari kwa kina...

TAKUKURU YAMTUHUMU ISMAEL ADEN RAGE KUFANYA KAMPENI KABLA YA WAKATI

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, TAKUKURU mkoani Tabora ilimshikilia Mkurugenzi wa Voice of Tabora FM Redio, Ismael Aden Rage, Mei 23 kwa tuhuma za rushwa na kuanza kampeni kabla ya wakati

Rage ametoka kwa dhamana Mei 24, ametuhumiwa kuwakusanya wapiga kura na viongozi wa CCM ngazi ya kata na Matawi kwa lengo la kuwashawishi wampigie kura

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Tabora, Mussa Chaulo amesema, kufanya kampeni kabla ya wakati ni kinyume cha sheria namba 11 ya mwaka 2007

Chaulo amewatahadharisha wenye nia ya kugombea kutowahonga watu pesa ili wapigiwe kura, pia wasivunje sheria kwa kujifanya kampeni kabla ya wakati

#JFSiasa #Rushwa #JamiiForums #Kampeni
IMG-20200525-WA0016.jpg
IMG-20200525-WA0017.jpg
 
Wakiachwa mtasema wameruhusu uundwaji mpya wa makundi ndani ya chama.....................
 
Mbwa kala mbwa!
Msomali hana nafasi katika utawala wa msukuma.

Alisikika mlevi mmoja wa gongo mitaa ya Kanyenye (Tabora) akisema hayo.
 
Back
Top Bottom