Tabora kaibuka mama kama babu wa loliondo

NGUZO

JF-Expert Member
Jan 8, 2011
257
46
Wadau kuna mama mmoja Tabora ambaye amekoka anadai ameoteshwa kuponya watu magonjwa yote, hivi ninavyozungumza tayari kuna foleni kubwa ya wagonjwa wanasubiri kupata tiba.

Tofauti ya mama huyu na Mchungaji wa Loliondo ni kuwa, huyu anatoa kikombe cha maji ya kawaida baada ya kuyaombea. Haya karibuni Tabora.
 
Kama huyu mama ni Mlokole, Ngoja nimsikie Miss Judith kwanza ndo niamue kuja huko ama la!
 
Kama huyu mama ni Mlokole, Ngoja nimsikie Miss Judith kwanza ndo niamue kuja huko ama la!

Mark 16: 15Akawaambia, "Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.....mtaweka mikono yenu juu ya wagonjwa, nao watapona."

Hii ndiyo kanuni ya uponyaji wa Kimungu. Zaidi ya hapo ni uganga wa kienyeji.
 
Kuna mambo namalizia, muda si mrefu nitaoteshwa na mimi nianze kugawa vikombe.
 
inaonekana ni kweli babuu yangu mwasapile katumwa na Mungu mbona dawa yake inaigwa sana na kila mtu, yangu macho
 
wadau dada wa Tabora anaetibu kwa imani kuwa alioteshwa na bikira maria, anagawa kikombe kwa bei ni ile ile kama ya kwa babu kikombe @ 500, kwa picha zaidi bofyeni MICHUZI
 
Mbona haya makanisa yameanza kuombea maji siku nyingi. Kuna kanisa pale moshi wanaombea maji ya kilimanjaro! Yale yanayotengenezwa na bonite!
 
NGO zote sasa kukosa uraji kama kikombe cha bibi kinatibu nadhani wizara ya afya itapunguziwa zigo.
 
Jamani tuacheni utani hizi fotokopi za babu mwaisapile zitaipeleka nchi pabaya walikuwa wapi? Siku zote wameona babu kapata umaarufu ndo nao wameaanza acheni utani jeshi la polisi kamateni huyo sijui dada/mama mpigeni nondo afu ahojiwe kwa undani kama hamtaona anaikana anaikimbia hiyo dawa yake
 
Kwa wafuatiliaji wa mambo ya kiimani....!
chunguza wengi wanapoombea hawataji JINA LA YESU.... kitu ambacho inakubidi uweke big...very big question mark.....!
MBEZI BEACH ......KIBAO CHA SHULE....KWA MAGURUWE....nako kuna nabii FLORA.....fuatilia matumizi ya JINA LA YESU....!
USISTUSHWE NA MIUJIZA IFANYIKAYO KUWA NI KIGEZO CHA UUNGU WA HUDUMA....BALI TUZIJARIBU ROHO
 
Back
Top Bottom