Wazalendo,
Si Tabora tu; inabidi kila mtu achangamkie maendeleo ya mkoa anaotoka, tufanye ushindani wa kimaendeleo kuendeleza mikoa pale panapowezekana. Nafikiri wengi hapo mikoa hii iliwasomesha shule za msingi, sekondari tena bure tuu! Hii ni mojawapo ya giving back to community" wekeni zile "investment" huko, (zile mnazotaka kuleta Tanzania baada ya kupata dual citizenships). Maana it takes a little kufanya watu waje kwa wingi na kukuza mji. Ukianzia huko Mtwara kwa kina Mkapa, Mrope, na rest of M, M, M's; mmesomeshwa na shule huko, sasa fanyeni shughuli za kuendeleza miji sio kusubiri SERIKALI tuu, Serikali huyu atafanya mangapi???
Na yie akina Katembo, Kifaru, Kasungura, Kifaru, Komba ,Simba na the rest of everyone mwenye jina la Wanyamawanyama, Ndegendege n.k. Huko mna madini ya kutosha tu, zaidi ile Magnesium; sasa angalieni mtaitumiaje kunufaisha Tanzania, na Songea yenu; pia huko kunatoa kahawa nzuri sana kama vile Kilimanjaro, sijui kwanini Kilimanjaro ndio iko kwenye ramani na Tanzania na ndio inapeta zaidi yenu.
Akina Shelukindo, Shekifu, Shemdasi, Shem nini sijui, tafuteni wenzenu wote wenye kuitwa She, She, na angalieni mtafanyaje pia, Lushoto being the one best area conducive for production of fruits, mtafanyaje ku-take advantage ya hiyo hali kuendeleza huko milimani na Tanzania kwa ujumla!
Inanikumbusha Profesa Ngware pale UD used to say, akisihi wanafunzi, "mtakapo maliza shule, tafadhali kama huna cha kufanya mjini rudini kijijini kwenu ukasaidie kuharakisha maendeleo ya kwenu", alisema "msibakie kung'ang'ania Dar es Salaam, maana mpaka sasa wenyewe tumeshatosha na kubanana, sasa mrudi kwenu hatutaki fujo". People used to get offended, lakini alikuwa na point.
Hii pia imenifanya nifikirie, hivi, mikoa tofauti imetoa watu tofauti, kuna need ya mimi mwenyewe kufanya utafiki na kuandika kitabu kufuatilia kile kilichoanzishwa na Dk.Bundara, labda, wachagga ndivyo walivyo, au wasukuma ndivyo walivyo, ama wahaya ndivyo walivyo-Inashangaza kuna mikoa ina rasilimali zote, na maendeleo yanakuwa madogo ama hamna, wakati sehemu nyingine yenye zile rasilimali zile zile, maendeleo yapo ya haraka haraka, KULIKONI??? Il'l update on my findings!
Na mwisho, while niko na sprit yaku-give back, ndugu zangu mlio-graduate from UD, It's about time, tuanze kusaidia Chuo Kikuu, (if you don't already do), nina-organize a society ya Alumni, kazi itakuwa ni kutoa misaada ya hali na mali pale panapowezekana. Someting like, Kisura Foundation, inatoa scholarship, inajenga nyumba za kulala, inanunua vitabu n.k. Especially nyie mliosoma bure pale UD, return, au to put it lightly, please give back, maana madeni mliokopeshwa mmegoma kulipa! Changia hata kitabu basi aah.
Asanteni.