Tabora imechelewa ama imecheleweshwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tabora imechelewa ama imecheleweshwa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Hossam, May 10, 2012.

 1. Hossam

  Hossam JF-Expert Member

  #1
  May 10, 2012
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 2,367
  Likes Received: 246
  Trophy Points: 160
  Ni sawa sisi Wanyanyembe, na kwa hakika hakuna awezaye kuleta mabadiliko Tabora au kuamua kukubali mabadiliko kwa faida ya Wanatabora na Watanzania kwa ujumla ila sisi wenyewe, lakini jee, Tabora haikupewa elimu sahihi ya uraia kwa wakati ama imechelewa kukubaliana na upepo wa mabadiliko?

  Maana ni Tabora hii imewaelimisha wengi viongozi wetu, ni Tabora hii imekuwa ikikumbukwa kihistoria kama business center enzi zile za 1890s na hata nusu ya kwanza ya karne ya ishirini.

  Tabora ina kila rasilimali zenye kuweza kuipaisha na kuifanya kinara wa maendeleo Tanzania, tupia macho misitu yetu uone mbao safi na asali, ona udongo wenye rutuba uwezao kuotesha mazao yote yote, sasa kwa nini tuko mkiani?

  Hivi ni blanket la alfajili ya usingizi mtamu wa uzembe na wa kuzuia kuchangamka ama ni fikra potofu za wakoloni na kuogopa kivuli zimetufikisha mkiani?

  Jee ni kweli mzigo mzito wa ujinga mpe mnyamwezi? Sina hakika kama tumecheleweshewa ama kutokukubali mageuzi ya kweli, kama asubuhi imefika basi tuamke wajameni.

  G Kassanga.
   
 2. james chapacha

  james chapacha JF-Expert Member

  #2
  May 10, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 942
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Ni KHANGA,KOFIA na FLANA vinawachelewesha kuamka!
   
 3. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #3
  May 10, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Mkuu kasanga usiwe na hofu kabisa kwani sasa tunajitahidi kuwahimiza wanatabora ijapokuwa tupo mbali ila hata kwa njia ya mitandao ili 2015 tuweze kufanya mabadiliko ya muhimu( fundamental changes) pia kwa analysis yangu ndogo nilofanya ni kwamba tabora itakombolewa kutokana na wimbi la vijana ambao kila mwaka wanagradurate 4m4 shule za kata, pia wanafunzi kutoka hivyo vyuo kama saut,teku,uhaziri na watu ambao si wageni wa hapo wenye hali ya mabadiliko┬┤.
  My outlook:
  ni vyema elimu ya urai ikazaniwe hasa kwa kuwekeza kwa wanafunzi vijana wote pamoja na makundi mengine ya kijamii.

  Shardcole@Tabora1
   
 4. patience96

  patience96 JF-Expert Member

  #4
  May 10, 2012
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 1,187
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Gwawipa! Kikulacho ki nguoni mwako mkuu! Tafakari, chukua hatua.
   
 5. mluga

  mluga JF-Expert Member

  #5
  May 10, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 678
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kassanga, Kassanga, Kassanga, huko nenda taratibu hebu mtafute MKONONGO SIKONGE ha ha ha ha ha huyu atakupa jibu
   
 6. Mkereketwa_Huyu

  Mkereketwa_Huyu JF-Expert Member

  #6
  May 11, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 5,124
  Likes Received: 1,210
  Trophy Points: 280  Sikia, tuko karne ya 21 siyo tena ya 19. Tabora mamwinyi ni wengi mno na sehemu yeyote ile Africa inayoendekeza mila hizi za kimwinyi hazina maendeleo, mfano wa Tabora na Kigoma, Zanzibar, Tanga, Mtawara, Lindi, Pwani, n.k. Na ujinga mwingine wa Tabora walionao ni kwamba wameweka nyuki ndiyo rasilimali za ule mkoa. Yaani wananchi hawawezi kulima mpaka nyuki wao wa kubahatisha washibe, si upuuzi huu? Eti mtu mzima unategemea nyuki ndiyo msingi wa maisha yako, jamani?
   
 7. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #7
  May 11, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Si Tabora tu iliyocheleweshwa kwa makusudi kabisa. Tazama Kigoma, Mtwara, Tanga halafu jiulize what do they have in common? jibu ni 83 vs 17 bila kukisia.
   
 8. brazilian

  brazilian JF-Expert Member

  #8
  May 11, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 607
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hebu fikiria kwa vihela vidogo, t-shirts na kofia watu wanampa ubunge Rage ma Munde. Unategemea mabadiliko hapo? endeleeni kucheza bao, draft na pool table mpaka Yesu atakaporudi. Hebu angalia kata kama Ng'ambo, Isevya, Chemchem kulivyo na njaa.
   
 9. Mwana Mtoka Pabaya

  Mwana Mtoka Pabaya JF-Expert Member

  #9
  May 11, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 11,763
  Likes Received: 8,034
  Trophy Points: 280
  And what does it mean in our language; Arabic culture that makes people lazzy?

  Au ukosefu wa elimu na utashi wa kuitafuta ulioletwa na uwepo wa hao waarabu during colonial era?
   
 10. Hossam

  Hossam JF-Expert Member

  #10
  May 11, 2012
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 2,367
  Likes Received: 246
  Trophy Points: 160
  Mkuu salute kwa changamoto yako lakini nina neno zaidi, sio kwamba Tabora itegemee nyuki tu japo kwa hakika inaweza kutegemea nyuki na kuwa mkoa Tishio Tanzania, ona asali ya Tabora ni bora na kumbuka mkoa una mapori makubwa yapatayo hekta 2.5 milion, nyuki wamo mote humo. Kama serikali leo ingeliona hili nakuapia wangepiga marufuku ulimaji wa Tumbaku huku ambao umeanza toka 1963 ukitafuna hadi sasa hekta 0.5 million. Kama kungekuwa na processing plant kubwa, tofauti na pale Nyuki Center waliyoiua lao hii Tabora ingekuwa na mchango mkubwa kwenye GDP na hata forex tungekuwa nazo kubwa, hivi sio uchumi wa Norway unaobebwa na Magogo yaani mbao!?

  Ni sawa umeleta changamoto lakini hakiyamungu nakuapia hata utalii Tabora ingekuwa tishio, tuna kaburi la Mtemi Milambo the Napoleln of East Africa, tuna Ugalla Game Reserve, tuna Dr Livingstone monuments, na tuna the German Boma, ni mengi mkuu.
   
Loading...