Tabora: Dk Slaa ataja orodha mpya ya mafisadi!

Status
Not open for further replies.
wanaJF mlioko Tabora tuhabarisheni kinachoendelea katika mkutano wa kimapinduzi ulioko tabora,na "the second list of the shame"

Yap! yap...... hiki ni kizazi cha dotcom tunahitaji uwazi zaidi na kufaidi kwa pamoja keki ya taifa na si watu wachache na familia zao!!!!!!!!!!!
 
Saturday, 16 April 2011
Fidelis Butahe

WAKATI Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikijivua gamba kwa kuwataka wanaotuhumiwa kwa ufisadi wajiondoe wenyewe kwenye uongozi wa chama hicho, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbroad Slaa leo anataja orodha mpya ya mafisadi ndani ya chama hicho tawala ili nao waunganishwe katika orodha hiyo.

Mkurugenzi wa Organaizesheni na Mafunzo wa Chadema, Singo Bensoni aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa Dk Slaa atataja majina hayo leo mkoani Tabora katika mkutano wa hadhara kama alivyofanya mwaka 2007, katika Viwanja vya Mwembeyanga, Dar es Salaam.

Alisema katika mkutano huo, Dk Slaa akiwa na viongozi wengine wa Chadema, atataja majina hayo ya mafisadi ili kuipa CCM wakati mzuri wa kuwatambua na kuwachukulia hatua kama kweli ina nia njema ya kujivua gamba.

Hii ni changamoto mpya kwa CCM ambayo tayari imenyooshea kidole genge la mafisadi lililoko ndani ya chama hicho na kuwapa siku 90 watuhumiwa hao kujiuzulu ili kukinusuru.

Bensoni aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa orodha hiyo mpya ya mafisadi inayotarajiwa kutajwa leo, ni kubwa kuliko ile ya mwaka 2007.

“Ushahidi tunao ndiyo maana hata tuliowataja mwaka 2007 hadi leo hawajafungua kesi yoyote mahakamani. Wanasema kuwa wamejivua gamba. Gamba la CCM siyo uzee ni ufisadi,” alisema Bensoni na kuongeza: “Tutawakumbusha gamba wanalotakiwa kujivua ni lipi ili Watanzania watambue. Dk Slaa ataweka mambo hadharani katika mkutano huo akiwa pamoja Profesa Abdalah Safari na Mabere Malando.”

Alisema licha ya CCM kutoa siku 90 kwa watuhumiwa wa ufisadi wanaotajwatajwa, wapo ambao hawajatajwa kati ya waliotakiwa kujiuzulu kwa tuhuma za hizo. “Hapa sasa ndiyo watajua mafisadi ni kina nani. Tunataka kuwakumbusha gamba ni lipi.”

Alisema kuwa orodha hiyo ni mpya na ina tofauti na ile ya Mwembeyanga kwa kuwa tangu kipindi hicho mpaka leo kuna matukio mengi ya ufisadi yaliyoendelea nchini. “Ufisadi wa sasa ni mkubwa sana hivyo orodha itakuwa kubwa, ‘Ni ngoma nzito’ na tukimaliza kutaja orodha hiyo tutaendelea na mikutano yetu nchi nzima,” alisema Bensoni.

Akizungumzia hatua hiyo ya Chadema, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema: "Chadema wamefilisika kisiasa, walidhani wataitisha CCM kwa hoja ya ufisadi lakini sasa CCM ni chama safi. Kwa mabadiliko tuliyoyafanya, Chadema inatakiwa kucheza ngoma yetu (CCM) na siyo sisi (CCM) kucheza ngoma yao."

Nape alitumia fursa hiyo kuipongeza Serikali kwa uamuzi wake wa kukubali kurudisha muswada wa Katiba kwa wananchi na kuwapa fursa zaidi kujadili suala hilo.

Kutokana na urasimu wa CCM kutofatilia utendaji na kusoma nyakati viongozi wamekuwa na tabia ya chukua chako mapema na hilo nila siku nyingi. Ukiwa nacho unaongezewa asiekuwa nacha hata kile kidogo ananyanganywa. Watanzania wengi wanateseka kwa ajili ya hawa mafisadi, tunasikia mabilioni yanatolewa lakini kinachofanyika hakuna, hali ni ile ile ya kila siku haibadiliki na ukiangalia ninaweza kusema 80% ya watanzania wanafanya shughuli zao za kujiingizia kipato.

Dr Slaa ubarikiwe kwa juhudi zako na wanachadema wote, hii taa inayowashwa iwezekutoa mwanga kwa watanzania wote bila kujali tabaka lolote.
 
Nape, ina maana unakiri mlikuwa mnacheza ngoma ya CHADEMA kabla ya kuvua magamba?

Well done CHADEMA ... for keeping this guys in the restlesness state!!

Let them no rest.... untill they deliver what they promised!!

Let them always busy following what you are about to do ...

Let them reflect on themselves...

..make sure they never have a peacefull sleep till all Tanzanians have sound and deep sleep!!!

Weldone CHADEMA...Keep it up !!
 
Kwani CHADEMA hakuna mafisadi? Milioni 200 za kusaidia chaguzi za vyuo vikuu wamepata wapi wakati ruzuku yao ni milioni 100? Acheni kudanganya toto. Chama kisicho na ufisadi ni Demokrasia makini pekee inji hii. Hao CHADEMA tangu tumewapa ubunge hata kuja kutusikiliza wananchi kero zetu hawataki. Kazi ya kupiga kelele tu Bungeni na kuonyesheana vidole. Huyo Silaa mwenyewe ni fisadi asituzengue hapa
 
CCM wajanja na wanajua kucheza na akili za watanzania wakidhania kuwa watanzania wa leo bado ni bongo lala! Juzi leo nape kasikika akiipongeza serikali ya CCM kwa kuwa sikivu! UNAFIKI MTUPU! hivi serikali hii ingekuwa sikivu na yenye kufikiria ingeandaa muswaada kwa kingereza ikipata shinikizo na kusalimu amri ndio iitwe SIKIVU?! Mbona wakati wa kampeni vipeperushi na uzushi mwingine hawakuandaa kwa kingereza?!

CCM wameshindwa kuwawajibisha mafisadi na wamezidi kuwakumbatia tena kwa nguvu na bashasha, iweje leo wajifanye wamevua gamba wakati wameshindwa kutueleza wananchi pesa za EPA waliochukua ni kina nani na wamerudisha kina nani? Vipi kuhusu KAGODA ile kampuni iliyochota fedha zilizosemekana kuwaingiza madarakani wavua magamba ya wenzao? Wamevua gamba gani kwa kuwatosa wachache na kuwakumbatia wengine akiwemo fisadi namba moja.

Safi sana DR SLAA tuko nyuma yako taja mafisadi watafuna nchi yetu tuwaje maana hatuonei hurma wananchi tunaotaabika kwa umaskini.
Nahisi hawa watakuwemo...
1. Ra
2. El
3. ....
 
Hizi posti zingine zimepotea njia.
 
Katika kile ambacho hakikutarajiwa vijana wa tabora mjini wamekua na mwitikio mkubwa sana katika kuunga mkono mageuzi mji umetapakaa vijana walio valia magwanda ya kaki kama sare rasmi ya chama cha chadema na kila kona pikipiki tax na baiskeri zimetundikwa bendera za chadema watu wana hamu kubwa sana ya kumsikiliza dr W.P.Slaa.
 
tunamsubiri kwa hamu rais mtarajiwa vijana huku tupo imara sana kwa ajili ya ukombozi
nazani listi ya leo na NAPE pamoja na MAKAMBA wapo sasa sijui watajivua tena gamba?????
 
Chupi zaanza kulowana ndani ya vigogo wa serikali ya CCM! Mbele kwa mbele Dokta wa ukweli.

Wasaidie kuwataja, maana wenyewe wako dhaifu kuwataja!
 
Hakuna 'vikaragosi' humu ndani vilivyoanzishwa na Mukama/Msekwa vya kusema CDM wanataka kuleta fujo?

CCM kubalini -- the game is up -- hata mkileta hoja za kuletwa, ufisadi hautakiwi popote duniani.
 
CCM wajanja na wanajua kucheza na akili za watanzania wakidhania kuwa watanzania wa leo bado ni bongo lala! Juzi leo nape kasikika akiipongeza serikali ya CCM kwa kuwa sikivu! UNAFIKI MTUPU! hivi serikali hii ingekuwa sikivu na yenye kufikiria ingeandaa muswaada kwa kingereza ikipata shinikizo na kusalimu amri ndio iitwe SIKIVU?! Mbona wakati wa kampeni vipeperushi na uzushi mwingine hawakuandaa kwa kingereza?!

CCM wameshindwa kuwawajibisha mafisadi na wamezidi kuwakumbatia tena kwa nguvu na bashasha, iweje leo wajifanye wamevua gamba wakati wameshindwa kutueleza wananchi pesa za EPA waliochukua ni kina nani na wamerudisha kina nani? Vipi kuhusu KAGODA ile kampuni iliyochota fedha zilizosemekana kuwaingiza madarakani wavua magamba ya wenzao? Wamevua gamba gani kwa kuwatosa wachache na kuwakumbatia wengine akiwemo fisadi namba moja.

Safi sana DR SLAA tuko nyuma yako taja mafisadi watafuna nchi yetu tuwaje maana hatuonei hurma wananchi tunaotaabika kwa umaskini.
Nahisi hawa watakuwemo...
1. Ra
2. El
3. ....

Wakuu wana JF kutoka Tabora tujuzeni tafadhali orodha mpya ya Mafisadi nchini. Dr atahutubia saa ngapi?
 
Mbona nimesoma huku thread wakasema unarushwa na tbc au uongo?
 
yeeeeeeessssss!!!!!! Peoples power!!! Hadi kieleweke. Tamthilia ya sisiemu yafikia ukingoni!!!
 
Itakuwa vigumu sana kwa cdm kucheza ngoma ya ccm kwa sababu mchezesha ngoma wake amekumbatia nyoka wenye sumu ya kuliteketeza taifa hili, ngoma yao ni ile ya kutafuta dawa ya kuua hao nyoka siyo kuwavua magamba
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom