Tabia za wanaume Wasambaa: Binti yangu kakolea kwa Msambaa

Mzee, ss haya mambo ya Ukabila yanatokea wapi? mbona unafanya ongea mambo kama sio mtu mzima? wanasema mtu mzima dawa sasa mtu mzima wewe sijui umegeuka sumu? haya chamsingi huyu kijana kama wanapendana sidhani kabila ni tatizo hata kidogo, USIDHARAU kabila la mwengine hata kidogo kwa sababu na wewe pia kuna vitu kabila lako wanafanya makabila mengine wanaona kituko,ww ni mtu mzima na mtu mzima anaongea kwa Busara hekma na anafikiri kabla hajaongea.........
 
mzee mwenzangu watoto wakipendana hii biashara ya kuangalia rangi,kabila,uraia etc achana nayo,so long as wanapendana acha waoane,mi wanangu washanambia katu hawataolewa bongo hii,mi nawaangalia tu,wanasema wanaume wa kibongo wazushi.
 
Wengi wao ni wavivu na hawana akili za kujituma. Inawezekana wa binti yako akawa tofauti na wengine.
 
Kwanza Mpwa umetutukana sana kwa kutuita wacheza ngoma, kuandika kwamba you are not offending anybody bado haiondoi maana kwamba hujatu-offend, ni sawa na mtu akuite mpuuuzi kisha akwambia sina maana wewe ni mpuuzi, so naomba paweke sawa hapo mahali; haya sasa kwenye swali la msing sasa; mlete tu binti yako, hakuna wanaume wakarimu kama Wasambaa, I swear it, kwao binti yako anakua binti yao, they will treat her as thier own daughter, hawana mambo ya ajabu ajabu japo pia sio wote ila walio wengi wako huko au umesahau kuwa Civilization ilianzia kule, ok, kwakusaidia zaidi nipe mahali mchumba mtarajiwa anapotokea kama ni Mlalo/Bumbuli/Mtae/Lushoto Mjini na baadhi ya maeneo mengine ujue umepata.

This is serious na sio uongo, uliza yoyote atakwambia, si unakumbuka kuwa ni wasambaa hawa ndio wamempa Ben Mkapa, Jaka Mwambi, Mkuchika, JK, Sumaye na wengine weengi maeneo? hio ndio nature yao. I am proud of it japo tunabaki kuwa maskini

zebu sikia hii rafiki "MILIMA YA KWETU"-SUPER RAINBOW - BongoCelebrity heri ya mwaka mpya mjomba
 
Tanga ndipo mapenzi yalipozaliwa usijali binti yako yupo katika mikono salama

Sent from my HTC Incredible S using Tapatalk
 
kaka, ni bora kakuletea mchumba mapema - usitizame ni kabila gani, awe mtarabu na heshima yake na aweze kulea bint yako kwa hali na mali. Ni bora kuliko angalikuletea mimba/katoto bila ya mdoa. Hongera in advance mkuu..
 
kwani wewe mwenyewe ni kabila gani hasa hadi uwaponde wasambaa kama wacheza ngoma?
Tanga kuna makabila mengi, ila unawajua wagosi wa ndima?
 
Wengi wao ni wavivu na hawana akili za kujituma. Inawezekana wa binti yako akawa tofauti na wengine.

You are wrong! usiwafananishe wasambaa na wadigo.
Nenda kariakoo kuna mtaa wa wasambaa ndio utajua ni wachakarikaji namna gani.
Kweli usilolijua ni kama usiku wa giza.
 
Mpe tu ila hujasema wewe ni kabila gani ? ni wapole na wachapa kazi ila wana wivu sana .swala la kuvaa msuli sio kweli ila ngoma wakati wa mavuno tunaitwanga kweli kweli ila hawapendi maneno maneno nyumbani warudipo .avumilie ndugu wa mume .
 
Mmh Sweetlady kama hawajui kutunza wake sasa huo ukarimu wanamfanyia nani?

Mi naambiwa eti wasambaa ni maarufu kucheza ngoma na kuvaa misuli tu, si watu wa kujibidisha kwenye kazi za kimaendeleo.

Acha mambo ya kusikia. nenda kariakoo kuna mtaa wa Wasambaa, hapo utawajua ni watu wa ina gani. Sio watu wa kucheza ngoma kama wazaramu na wakwere. Nina wasi wasi utakuwa umeambiwa mkweo ni ******/mzaramu wewe akili zako zikaenda kwa wasambaa,
 
kaka as long as he loves your daughter with all his heart and he will treat her right hamna haja ya kubagua makabila
 
Mapenzi ya kweli hayajali umri, cheo, utajiri umaskini wala KABILA. Mwanao alivyompenda alijua kuwa ni msambaa, na ana vigezo vyake ambavyo huyo msambaa unaemdharau yeye ameviona na ndo vilivyomfanya ampende hadi akamleta kwako.
Acha ukabila na kumnyima mwanao uhuru wa kupenda. Au ulitaka kumchagulia wewe mume wa kumuoa?
Utamfanyai maamuzi alafu aje akulaumu baadae.
Ubaya au uzuri wa mtu si kabila lake, bali ni mtu mwenyewe
 
mpe mwongozo ndugu yangu. Siku hizi watoto wanasoma shule za garama sana aisee, usikubali apotee kihivyo. Uhangaike kusomesha mtoto afu aje aishie kuolewa na mcheza ngoma? No haiwezekani! Bora asiolewe kabisa.
kwa kweli
 
Mapenzi ya kweli hayajali umri, cheo, utajiri umaskini wala KABILA. Mwanao alivyompenda alijua kuwa ni msambaa, na ana vigezo vyake ambavyo huyo msambaa unaemdharau yeye ameviona na ndo vilivyomfanya ampende hadi akamleta kwako.
Acha ukabila na kumnyima mwanao uhuru wa kupenda. Au ulitaka kumchagulia wewe mume wa kumuoa?
Utamfanyai maamuzi alafu aje akulaumu baadae.
Ubaya au uzuri wa mtu si kabila lake, bali ni mtu mwenyewe

brooklyn; kwa maisha ya kitanzania huu ndio ushauri unaokufaa.
 
wanapenda mke zaidi ya mmoja na kila wanakoenda kutafuta maisha hua wanaoa so mikoa yote aliyozunguka kutafuta maisha ujue ameecha mke huko na kamuaga naenda kuangalia life mji mwingine mpka ndio kamkuta bintiyo
 
Akina mgosingwe wanasifika kwa kupiga ulabu sana, sijajua madhara mengine, ila wengi wao wanakuwaga wafupi, na watu wafupi nadhani fujo zao unazijua.
Am out!
 
wewe baba mtu unaonekana una mwili mkubwa akili kijiko cha chai **** wewe unachaguwa kabila???kama haumtaki msamba muowe ww big 4 nothing
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom