Tabia za Mama Mkwe ndio tabia za Mkeo..Chukua hiyo kubali au kataaa

MR LINKO

JF-Expert Member
Aug 20, 2016
3,034
3,481
Kwa utafiti wangu mdogo niliofanya nimegundua kwamba tabia za mama mkwe ndio tabia za mkeo upende usipende. Kwa hiyo kama una mpango wa kuoa usiishie kumchunguza mchumba wa kike ambaye wakati wa uchumba anakuwa anaishi maisha ya kuigiza bali pia hangaika kumchunguza mama mkwe.

Kwanini mama mkwe?

1. Mama mkwe ndie aliyemlea mkeo mtarajiwa kwahiyo mchumba wako atakuwa ameiga na kufundishwa kuwa na tabia kama mama yake

2. Mara mwanamke anapoolewa Mshauri mkuu ni mama yake mzazi(napenda uamini hili) kwahiyo maisha yake kwenye ndoa yatategemea ushauri wa mamaye

3. Ikitokea mfarakano kwenye ndoa na kama mwanamke ndio tatizo mama mkwe ndie mtu pekee anayeweza kumbadilisha mkeo katika njia sahihi.

Molembe pia alishawahi kusema hivi;
 
Hapo siyo kweli.kuna mademu hawachukuagi tabia za nzuri za mama zao wanachukua za mitandaini usije jidanganya na hilo.so hata kama mama mkwe ana tabia bomba binti anachota ya mtaani.so tabia ya mke ni ya kwake.


Ila kama mama mkwe ana tabia mbaya .mtoto anachukua hiyo tabia mbia kwa haraka zaidi.so ukiona mamamkwe yuko dakika mbili mbele ujue mtoto atakuwa dakika tatu mbele
 
Kuna ukweli but it's not always the case. Mfano mzuri ni sisi, yaani mama yetu angekuwa ndio baba watu wangesema alisingiziwa
Wamama wa enzi zetu lkn hawa wa digitali walio bize 24/7 kutafuta chapaa kuliko uangalizi wa watoto ni sawa na bure tu.

Wanapataje huo muda nakati majukumu yao ktk malezi wamewakabidhi housemaids???
 
Somehow nakubaliana na ushauri wako.
Pia kitu vha kuzingatia zaidi ni Status ya ndoa ya wazazi wa binti.

Kama wazazi wake bado wamedumu kwenye ndoa hiyo ni indicator nzuri sana. Kama mama wa binti kaachika kwa mumewe usidhani Binti ataona Thamani ya ndoa.
Hizi formula zenu kwenye mapenzi zinawa cost sana vijana,Kuna wengine maisha ya wazazi wao kwenye ndoa ndio yanawafanya wasitamani ndoa kabisa au awe anaishi kwa machale kwenye ndoa upendo nusu nusu so hamtokua na furaha na kuna wengine kulelewa na mzazi mmoja kunamfanya ajifunze athari zake na akiingia kwenye ndoa anailinda kwa gharama yeyote ili wanae wasipitie maisha aliyoishi
 
Back
Top Bottom