Sababu zitakazopelekea Mkeo awachukie Nduguzo

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,879
SABABU ZITAKAZOPELEKEA MKEO AWACHUKIE WAZAZI NA NDUGUZO!

Anaandika, Robert Heriel.

Katika jamii wapo Wanawake wanaochukia Wakwe zao, wapo wanaochukia Ndugu za mume.
Zipo sababu zinazopelekea MKE achukukie Ndugu za mume na Wakwe zake. Hata hivyo wapo Wanawake ambao wanachuki tuu na vijiba vya Roho, yaani Hawana sababu ya maana wala Hawana Baya walilofanyiwa. Ni Roho tuu za korosho zinazowasumbua. Hata hivyo kundi hili ni wachache Sana. Wanawake wengi wenye chuki huwa na sababu Fulani.

Zifuatazo ni miongoni mwa Sababu zitakazopelekea Mkeo AWACHUKIE NDUGUZO na Wazazi wako;

1. DHARAU WAKATI WA UTAMBULISHO na BAADA YA UTAMBULISHO.
Hakuna apendaye dharau. Hasa kinadada ni viumbe visivyopenda dharau. Chuki nyingi za Wake zetu chanzo chake ni dharau kipindi tunawapeleka wake zetu kuwatambulisha Kwa wazazi na Ndugu zetu.
Waafrika wengi hupenda kuchagulia Vijana wao Wanawake Fulani wa kuoa. Sio ajabu ukipeleka mchumba nyumba wazazi na Ndugu wakawa wanamthaminisha Mchumba wako kimaumbile na kihadhi kuona kama anakukidhi au hakukidhi ilhali wewe uliyempeleka umeshaona kuwa anakufaa.

Dharau za nduguzo au wazazi wako ndizo zitaamsha chuki Kwa Mchumba wako ingawaje hatasema. Mkeo ni kweli huenda sio nzuri lakini haiwahusu, huenda Hana umbo zuri, Hana Elimu nzuri na pengine katokea katika familia Maskini, yote hayo hayawahusu.
Wazazi na nduguzo kumuona Mkeo kama ameolewa na wewe ili apate unafuu. Yaani amezifuata Pesa zako. Huku wakitoa maneno ya kashfa jinsi walivyokulea Kwa taabu na kukusomesha mpaka ukafika hapo. Hayo ni majigambo na vitisho. Hayana maana yoyote Ile. Kwahiyo kama mumemsomesha, hiyo Pia ina-apply Kwa Sisi wanaume.

Sio Kwa Wake zetu pekee hata Kwa Sisi wanaume. Huwezi penda Wakwe zako na mashemeji zako au na Ndugu wa upande wa MKE ikiwa wanakudharau, wanakutolea matusi, kejeli na vijembe.
Lazima Watu wajifunze kuwa na upendo na kutenda HAKI.
Mnasema Wake zetu hawapendi Ndugu zenu lakini muda huohuo Ndugu wa mume wanadharau za rejareja Kwa MKE unafikiri nini kitatokea.

Unakuta Ndugu wa mume wanasema Yule Mwanamke ndiye anakula Pesa za Kijana wetu, sasa mlitaka ale Nani. Alafu mbaya zaidi usikute huyo mwanaume mwenyewe Pesa anamaliza Kwa starehe zake, iwe pombe na anasa za Malaya. Unafikiri MKE atajisikiaje?

2. Mwanaume kutokutenda Haki.
Mwanaume lazima afundishwe upendo na Haki.
Lazima mwanaume ujue Haki zako, Haki za Mkeo, Haki za Watoto wako, Haki za wazazi wako na Haki za nduguzo.
Ukltakaposhindwa kumtendea Haki Mkeo ukiwapendelea zaidi Wazazi au Ndugu zako lazima chuki zianze.
Lakini Pia ukishindwa kuwatendea Wazazi wako Haki, ukashindwa kuwaheshimu kama inavyotakiwa lazima wakuchukie.
Lazima uchore mipaka ya Haki ndani ya Familia.
Baba kama kichwa cha familia unaposhindwa kutoa Haki lazima familia idondoke. Na lazima Wanawake wakusumbue.
Kikawaida Wanawake ni Watu wanaopenda kutikisa kibiriti au kibuyu kuona kama Haki imejaa au ipo nusu. Dada, Mama zako na Mkeo lazima wakutikise wajue kiwango chako cha Haki. Hivyo matokeo you're utakayoyatoa ndio yatajibu kuwa wewe ni MTU wa namna gani.

Kuna Haki zifuatazo ndani ya familia
A. Haki ya Nafasi
Nani wa Kwanza, wapili, watatu, wanne l, watano n.k.
Nafasi zitakuwa kama ifuatavyo
i. Mungu
2. Mume
3. MKe
4. Watoto
5. Wazazi (pande mbili)
6. Ndugu ( Pande mbili )
7 marafiki.
Itifaki hiyo itazingatiwa Kwa kila kitu. Kuanzia maamuzi, wajibu na majukumu.

B. Haki ya Huduma.
Kwenye familia Mume anaowajibu wa kumhudumia Mkewe na watoto. Huo ni wajibu na majukumu ya Mume.
Huduma zipo nyingi, kuna Huduma za kiuchumi, kimwili, kihisia, kiroho na Kiakili, kiulinzi n.k. yote hayo ni majukumu ya Mume.
MKe Pia anaowajibu na jukumu la kumhudumia mumewe, ikiwa ni pamoja na kumhudumia kimwili, kiroho, kihisia, na Kiakili.

Huwezi mhudumia mzazi zaidi ya Mkeo au Mumeo. Hiyo sio Haki. Hata kisheria hakuna kitu kama hicho.
Au huwezi hudumia Ndugu zako zaidi kuliko Mkeo au Mumeo hiyo ni dalili kuwa hujitambui na hujui maana ya Familia.

Huwezi mhudumia mungu zaidi ya Mkeo au Mumeo huo ni wendawazimu. Mungu anasehemu yake na familia inasehemu yake. Ndio maana hata kwenye zaka na sadaka mungu alitaka 10 percent.

C. HAKI YA MATUMIZI YA MALI
Ni Haki ya Mkeo au Mumeo Kutumia Mali au nguvu au Akili za wanafamilia Kwa manufaa yake au yako au familia Kwa ujumla. Ndugu au wazazi wanakosa Haki hiyo Kwa sababu wao sio sehemu ya familia yenu.
Ni kama wewe huwezi kwenda Kwa wazazi wako ukajiuzia nyumba ya familia ya Baba yako bila idhini ya Baba na Ndugu zako.
Halikadhalika wazazi au Ndugu zako Hawana mamlaka ya kuja kwako na Kutumia Mali za familia yako watakavyo.

Sio tuu MKE hata mtoto wako anauwezo wa kumzuia Ndugu au mzazi wako(Bibi au Babu yake) kutotumia Mali za familia.

Mwanaume unaposhindwa kujua mipaka ya wanafamilia utajikuta katika hali ya kutokutenda HAKI.

Mzazi hata kama amekuzaa Hana mamlaka ya kumtukana Mkeo, kumtolea maneno machafu na kumdhalilisha.
Au Mama au Baba mkwe wako hata kama kamzaa Mkeo Hana mamlaka ya kukutukana, kukutolea maneno ya karaha, na kuingilia mipaka yako.
Huwezi wapenda Wakwe wenye vijitabia vya kuingilia familia yako, au kukudharau Kwa hali au maumbile yako.

Taikon sio MTU wa unafiki, na napenda Watu Wasiwe Wanafiki. MTU kama anakuletea dharau za kipuuzi, iwe ni Mama au Baba mzazi, iwe Baba au Mama Mkwe au Ndugu. Usimfumbie macho, usimchekee chekee. Usijigonge gonge kwake. Nawe mpuuze, mdharau, Achana naye. Dawa ya Moto siku zote ni Moto.

3. Kumkataa Mkeo.
Wakati WA uchumba sio ajabu wazazi na nduguzo walionyesha hali ya kutomkubali Mkeo. Wengine hasa Dada zako walienda mbali mpaka wakawa wanamsakama Mkeo. Unategemea Mkeo atawapenda hao Ndugu zako waliomkataa?
Bahati nzuri Mkeo hawezi chukia Ndugu zako zote, lazima kuna nduguzo ambao atakuwa anapatana nao. Unafikiri ni Kwa nini?
Hata ni Mimi huwezi nikataa tena Kwa kashfa za kijinga na dharau alafu ATI baadaye nikuchekee chekee, unafiki wengine hatuna.

Ninafahamu wanaume kibao ambao tangu waondoke ukweni hawajarudi tena kisa na mkasa ni dharau na kukataliwa kijinga jinga.
Alafu ukishaanza kufanikiwa walewale ndio wanakuwa wakwanza kujichekesha.

Ninachotaka kukisema, ni kuwa Kabla ya chuki nyingi jua wema ulitangulia, ingawaje sio kila chuki ilitanguliwa na Wema.
Ukiona Mkeo au Mumeo anachukia Ndugu zako au wazazi wako Fanya uchunguzi Kwanza uangalie kisa ni nini. Je anauhalali wowote wa kuchukia?
Kisha andaa Mpango wa Usuluhishi na maridhiano ikiwa Kuna Ndugu au mzazi ndiye mwenye Makosa basi aombe Radhi.
Au ikiwa MKE ndiye mwenye Makosa aombe Radhi.
Au ikiwa Mume ndiye Mwenye Makosa basi aombe Radhi.

Hakuna ambaye hatakiwi kuomba msamaha. Iwe ni Mama au Baba au Mume au MKE au Kaka au Dada. Kama umekosea omba Radhi. Kusema Mzazi hakosei au Mwanaume hawezi kuomba Msamaha hicho ni KIBURI.
Kama hutaki kuomba Msamaha basi usikosee. Lakini kama unakosea sharti uombe Msamaha bila kujali nafasi yako.

Kama jitu halitaki kuomba msamaha licha ya kuwa limekosea bila kujali nafasi yake, hadhi yake, umri wake na mahusiano uliyonayo naye, MTU huyo akae mbali na wewe. Muweke mbali kabisa.
Hao ndio Watu wanaopenda kuabudiwa, linakosea lenyewe alafu linataka wewe ndio uombe Msamaha, pumbavu!

Mimi Taikon kama Baba na kama Mume, na kama Babu ajaye sioni Shida kuomba Msamaha ikiwa nimekosea, iwe Kwa mke wangu, au hata mtoto niliyemzaa mwenyewe nikamtunza akakua, wazazi wangu, Ndugu, jamaa na marafiki na watu wote. Kama nimekosea lazima niombe Msamaha, ila sio lazima kusamehewa.

SABATO NJEMA

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Back
Top Bottom