Kama najua napaswa kuwalipia wangapi sina haja kukusubiri uniulize.
Nisipokuambia na wewe ukaona jamaa hajipapasi mdai ili ajipapase.
hahaha siwapendi makonda mmetunyanyasa enzi tunasoma acheni tuwadharau ni haki yenu mpaka mnyoooke tu ina diamond'voice
Hivi nyie mnajua kama baba zenu wanataka hesabu ile ile bila kujali umebeba madent wangapi!
Katika kuhakikisha hesabu inatimia inabidi tupunguze idadi yenu nyie madent na nauli zenu za robo bei.
sheria ni wanafunzi watano sometime nyie mnasukuma watoto afu hambebi hata mmoja
"Una mia nikupe mia mbili?"
Aa we kibokoKonda katoa kichwa nje huku matako yake yanaonekana na kavaa boxer chafu
Kabisa mkuuKuna abiria anakuwa na chenji kamili ila nauli anatoa buku 10. Mi huwa nawakomeshaga kwa kuwapa sarafu nyiingi, hapo utakuta anasema nirudishie hiyo nikupe chenji.
Kumbe makusudihahaha siwapendi makonda mmetunyanyasa enzi tunasoma acheni tuwadharau ni haki yenu mpaka mnyoooke tu ina diamond'voice
Kwa uzoefu wangu na kazi ya ukonda ni mara chache sana kukuta abiria ambao wapo pamoja kimaongezi kila mmoja kulipa nauli yake...tena utasikia anamwambia mwenzake ngoja tu nilipe.......lakini hata hivyo kuna haja gani ya kumtukana mwenzio kwa swali kama hilo wakati jibu lake ni jepesi tu...otherwise uwe umeshavurugwa tangu huko kwako.....na ukaamua kuzihamishia hasira zako kwa konda..........Mkuu kuna haja gani ya kuuliza ukate wangape pindi unapopewa hela kubwa? Ni lazima kumlipia mtu?
Ni kweli kuna baadhi ya abiria ambao huwa wanawakera makonda pamoja na abiria wenzao lakini kwa ujumla makondakta wamezidi kuwa kero.
Mmekaa kituoni muda mrefu,watu wamejaa halafu inakuja daladala unamsikia konda anasema wapande wembamba tuu.
Nafikiri alisema hana hela ndogo kwasababu alikuwa amezificha mbali ili pengine asiibiwe na akawa amebakisha hiyo elfu tano kwa ajili ya nauli na mambo mengine madogomadogo.KikulachoChako umenikumbusha enzi hizo, nilikuwa konda wa ruti ya Kimara Posta, siku ya siku mama mmoja akapandia Akiba, nauli ilikuwa 200 tu kufika posta (route yote ilikuwa sh 300).
Wakati wa kushuka mi namdai nauli yeye ananidai chenji eti anadai kanipa sh 5,000/-, mi nikamwambia sijapokea chochote kutoka kwako, abiria wengine wakaanza kunishambulia eti sisi makonda ndo tabia zetu, sasa yule mama nikamuuliza ilikuwaje kwanza utoe hela kubwa vile kwa sh 200 tu, akasema hana hela nyingine yoyote na kwa hasira akataka kuvua nguo eti nimsachi.
Baada ya abiria kupiga sana yowe nikamwambia suka peleka gari central police, tulivyofika tukatoa maelezo ya kina, kuja kumsachi yule mama alikuwa ana sh 500 kama ishirini hivi kazichimbia kwenye mfuko wa nguo ya ndani. Tulimwacha police na sijui nini kiliendelea.
Nafikiri alisema hana hela ndogo kwasababu alikuwa amezificha mbali ili pengine asiibiwe na akawa amebakisha hiyo elfu tano kwa ajili ya nauli na mambo mengine madogomadogo.
Ukimwambie asiongeze abiria wengine ndani kuna joto "anakwambia ungepanda friji"
Anakudnganya kuna siti ukipanda unakuta hamna ukimuuliza anakujibu "ungekuja na stuli toka nyumbani"
SINA IMANI NA UKAWA
Abiria wa namna hii ni wasumbufu kwakweli, na hii haina maana kwamba abiria wote ni wastaarabu.Huwa tunakutana na ile mtu anakupa hela unahangaika kutafuta chenji, ukishampa anakuambia kata wawili, sasa kwa nini hukusema mwanzoni?
Kukwepa hii adha inabidi nikuulize mapema.
Gongo la mboto - mnazi mmoja wanakuuliza una hamsini??Unampa hela ya nauli anakuuliza,"una 100???"
Kama hauna unasubirishwa chenchi na usipodai hupati hiyo100
Wengine bila aibu et 100 tu unadai?