Tabia za kishamba za mabasi ya mikoani

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ comments za huu uzi daah!! Sawa nitajirekebisha
 
Oyaaa!!mzee baba sikila mtu kalipa nauli take?mbonaa unatufokea Kama tumepewa lift.....usinipangie hi ni public transport Kama vipi panda ndegee,afu eti wa mikoani kwani uko jijini kwenu hakunaa watu Kama hao Tena ndo vishoiaa balaa,wanataka kujifanya wajuajii kupita kila mtu
 
...tens mbaya zaidi we we upon kiti cha dirishani yeye yupo kiti cha Upande was ndani!...kila kituo anakutuma were ndio Uwe na Kazi ya kukutuma umnunulie hiki ama kile. Wanaudhi....

Haha mwisho wa siku wote mnaonekana ndio wale wale πŸ˜‚


Let's meet at the top, cheers 🍻
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Sio tabia ya kishamba,ni tatizo lisilozuilika l.
 
2016 nikiwa safarini kutoka kampala naelekea dar, kufika maeneo ya dodoma akapanda mama mmoja mtu mzima na akakaa siti ya pembeni yangu ... baada ya muda kidogo akaniomba tuchange siti akae dirishani nikambania, asee! yule mama alitema mate mazito na ule upepo wa nje mate yote yakanasa dirishani .... kusema ukweli pozi lote la kuangalia mandhali ya nchi lilikata na ata njaa yote iliyeyuka .....
 
Umesahau wale wanaonunua mayai, wanayamenya alafu wanakula.

Ile shombo ya mayai ni noma sana.

Ikibidi, punguzeni tabia ya kula kula hovyo.
[emoji23][emoji23][emoji23]Ushuzi wa mla mayai je balaa lake?
 
Ruti za chato,bukoba,tabora nini kukuomba tiketi wanataka utaje majina yako tena kwa sauti ukiwapa tiketi waangaliewenyewe waandike wanakasirika eti si utaje tu. Mmoja keshaandika jina hujakaa vizuri anakuja mwingine kuangalia tiketi wanaboa sana
tabia iliyonikera hasa kwa mabasi ya kanda ya ziwa ni suala la kuombwaombwa tiket kila saa na kondakta wa basi
unakuta umeshaonesha mara ya kwanza uko zako umelala gafla mtu anakuamsha anaomba tena tiketi zaidi ya mara 3 WTF😎😎😎
 
Apia!

Hauna safari hivi karibuni?
 
Dar to mwanza, picha linaanza pale ubungo zinaingia familia tatu za ndugu zangu wasukuma (watu kama nane wakiwa na watoto wadogo).


Hawakukaa pamoja, wengine walikaa nyuma kabisa, wengine katikati. Kazi inaanza akina ngosha walipoamua kupiga story kwa lugha yao, yani jamaa yuko siti ya nyuma kabisa ila anapiga story na ngosha mwenzie aliekaa siti ya kati.

Balaa zaidi ni pale walipoanza kupasiana vikombe vya maji (walibeba maji ya kunywa kwenye ndoo ndogo ya lita kumi). Kikombe kinapasiwa toka nyuma kule mpaka kinamfikia mlengwa kule katikati.

Mara watoto wakaanza kuzurula ndani ya bus, toka nyuma kuja kati endivaisi vesa bila kusahau vilio vya hapa na pale. Kuna wakati nikahisi labda niko kwenye darasa la chekechea, kumbe niko kwenye bus asee!

Kusema kweli Mwanza nilifika, ila cha moto nilikiona.


Safari ya kurudi dar, najikuta nimekaa jirani na mbibi msumbufu. Anyway, hiyo ni story nyingine!
 
Nilishangaa sana jamaa aliponiomba ear phones asikilize muziki. Seriously unaomba earphones za mtu humjui hakujua. Niliona kama kanidharau, hivi unaanzaje kuomba earphones.
Ulimpa?
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] nimecheka sana eti walipanda na ndoo ya maji ya kunywa wanapasiana kikombe Cha maji[emoji14][emoji14][emoji14]

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…