Tabia za boss wangu zinanikera

Inanitia hasira sana Mkuu baadhi yetu tunapokuwa na tabia za kijinga namna hiyo... Watu wanasahau tunatumia muda mwingi ofisini kuliko na familia zetu... kwa hiyo ofisi inapaswa kufurahiwa kwa kadiri iwezekanavyo... watu haohao wa ofisini ndio marafiki wetu wa karibu ndani na nje ya ofisi.....

Kuwa bosi kwa faa ujishushe sana na uishi katika uhalisia... wee fikiria kuna jamaa wanaripoti kwangu wana miaka zaidi ya 43 Mwingine ana 37 wengine rika langu.. nimewakuta kwenye idara mwaka mmoja uliopita... then nkapanda juu yao (mi sijafika hata 30)... kama sio Mungu kutupa hekima, kuthamini karama za wengine, Upendo na kujishusha huwezi kukaa hata mwezi na wandugu kama hawa... Maandiko yanasema ''Aliye MKUU katikati yenu na awe mtumishi wa wote' kinyume chake wakubwa wameendelea kutaka utukufu kwa kujiinua.....

 
Wa2 tu ofisini?

Hahah!!!

Ndio maana wanafanyiana tabia za ajabu ajabu, huenda walishatongozana hawa mmoja akachomoa sasa kifuatacho ITV ni kufanyiana visa...

Binafsi naamini lazima kuna chanzo haiwezi tabia hiyo kuzuka tu hivi hivi...
 
Nashukuru kwa ushauri wenu wadau.

Dada FaizaFoxy unapokuwa na bifu hutokaa uone zuri toka kwake, kuchelewa si kwa makusudi bali kutokana na foleni. Kukosea spelling ni kawaida make hakuna mtu anayeweza kufanya kazi ya kuandika the whole month bila kukosea spelling or digit hayo ni mapungufu ya kibinadamu.

Basi sasa yeye hutizama mpaka makosa ya nukta.

Sihitaji kutongozwa naye.
 
Last edited by a moderator:
Asante kwa ushauri wako ndugu Tized nitaufanyia kazi.
 
Last edited by a moderator:
Una mikasa miingi sana wewe

Mara una boyfriend sijui hana akili mara sijui nini
Leo umekuja na kisa cha bosi

Pole kwa mikasa!!
 

Hizo tabia za boss wako hujakosea hata kidogo kuwa ni za kike. Hata hivyo zigeuze tabia zake kama kichekesho wakati ukijipanga vizuri na utendaji wako wa kazi. Inaonyesha hana la kukufanya kukuondosha ndio maana ana vent hasira na dissappointment zake kwa kujaribu kukudhalilisha.
Muone mpuuzi atachoka huyo!
 
LA MSINGI ASIKUKATE MSHAARA basi wewe fanya kazi accordingly basi yatosha habari zingine atajua yeye
 
Mzungumzaji akiwa mjinga wewe msikiliozaji vaa akili, sasa kama bosi wako kawa na tabia za kike wewe vaa za kiume ili umieleze tabia yake sii nzuri na haina hatma nzuri katika kazi, hata kama ukitoka wewe akaja mwingine kwa tabia hiyo mambo hayawezi kuwa tofauti ivo ajirekebishe, na kwakuwa mko katika ofc moja hamna budi kujadili matatizo yenu na yakabaki kuwa ya kiofsi na sio maada za kufungulia vikao mtaani.


Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Pole dada kwa mafuriko ya matatizo yanayokukuta!

Kwa kweli huyo boss naweza kum-term mtot wa kiume aliyekulia katika familia yenye watoto wa kike weeeengi!

Halafu hata kwenye makuzi yake, hakuwa na interaction na jinsia yake.

Btw, ulishawahi kumwambia lolote kuhusu vitu vinavyokukera japo kwa indirect speech? Najua itakuwa ngumu.. But itabidi ummezeshe ukweli!
 
Rekebisha mapungufu uliyonayo ili Bosi wako akose cha kukusema..

Be the change you want to see.
 

Nadhani amesikia huyu mleta uzi. Pamoja na kulalamika sana kuhusu boss wake, inaelekea huyu cashier naye hajatulia; ni 'mcharuko' fulani.
 

Wanawake wana mambo yakusikitisha kidogo,eti wamejipa hakimiliki ya tabia, kwamba tabia hii ni ya kike n.k.
 
huyo boss kimeo, ila jitahidi usifanye uzembe wowote ktk kazi..
 
Ni mrefu but nahisi akili zake fupi ndio zinazomuendesha

BADILI TABIA hebu nifafanulie nivunjeje ukimya?

Kwanza usithubutu kumsema bosi wako kwa yoyote

Pia mweleze unavyojisikia

Ila mie ningepata boss anayenuna mbona ingem-cost hehehe
 
Last edited by a moderator:
Kwa sababu wakati unaomba kazi ulienda mikono yako ikiwa nyuma na sasa baada ya kupata kazi unatembea huku mikono iko mbele. Kuchelewa kazini, kuchelewa kurudi mapema kazini baada ya lunch na kutokuwa makini kazini ni baadhi ya mambo yanayowaudhi sana maboss wengi. Jirekebishe wewe She.
 
Una mikasa miingi sana wewe

Mara una boyfriend sijui hana akili mara sijui nini
Leo umekuja na kisa cha bosi

Pole kwa mikasa!!

Ndugu, sio kila thread inayoandikwa humu inamface mwandishi. Nyingine zinawekwa kwa niaba, zingine zinawekwa ili zitoe fundisho fulani, zingine ili kufurahisha wasomaji n.k

Asante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…