Tabia ya uchafu inakera sana kwenye mahusiano

ladyfurahia

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2011
Posts
14,758
Reaction score
9,592
Mwadela mayo mnaendeleaje mabestito wangu nimewamiss sana,

Imenibidi leo niingie tena hapa kutoa dukuduku langu la moyo kwani imenishangaza sana tena sana Jumapili iliyopita mabestito wangu wa ukweli nilikwenda mahali fulani kwa mabest wangu kuwajulia hali nilipofika mlangoni aghalabu kama si kushangaa sana jamani nikakutana ana na ana na kinyesi mlangoni, nami kwa haiba nyembamba nikakiruka na kubisha mlango na kukaribishwa ndani.

Kuingia tu mule ndani nikaonana nao wenyewe hawana habari kuwa mambo si shawari mlangoni pao, wameketi wanakodolea mimacho TV sijui kipindi gani kiilikuwa kinaendelea , kuangalia vyema mezani jamani niilishangazwa sana na kuona ukoko wa chakula huku wenyewe hawana habari kwa kwelil ilinipa simanzi nikajisemea moyoni hawa wanandoa wako hapa wenyewe wanaenjoy huku uchafu umewakalia kila kona ni nini hiii jamani.

Basi bila ajizi ikanibidi niage kiaibu aibu kwani niliona hapa sasa shida, wapendwa wangu wangu kwanini nimeleta kisa hichi hapa nimetaka tujiifunze kwa kisa hichi hapo juu mambo ya afya hususani afya zetu na sehemu tuishizo au sehemu zitungukazo wapendwa msijesema kwanini leo LADYF nimesema hivi imenikera kuona baadhi ya wanandoa hasa watoto wa kike kukaa mahali au eneo la home kwako likiwa limezingirwa na uchafu.

Hivi hatujui kuwa uchafu unaleta magonjwa jamani hivi kwanini hutaki kufanya usafi haata wa nguo zako jamani, imenibdi niwape somo kidogo hapa kwa wale ambao wamezoea kuwa wachafu wajirekebishe kwani chafu unakera na ni mfumuko wa maradhi mabaya, mabestito ambao mko kwenye mahusiano au ndoa jirekebisheni.

Ukiona mwenzio mchafu basi ongea nae kwa upendo na atajirekebisha uchafu mwingine uko kwa wanaume jamani usiombe mwanaume akuvulie nguo huo uvundo utakaotoka hapo utadhani kinyesi kimeoza miezi 7 kumbe ni misoski au manguo ya ndani hayajafua miezi sasa sasa hapo bestito wa kiume unamkomoa nani kama sio kujikomoa wewe mwenyewe na kujipa magonjwa yasioyoponyeka.

Na hii tabia kadhalika iko hata upande wa pili wa wanawake jamani acheni kuwa wachafu kwani uchafu huleta magonjwa na ni adua mkubwa sana kwako wa maendeleo ukiwa unaumwa utawezaje kufanya kazi , utawezaje kujiendeleza, mabestito tabia ya uchafu ni dhambi.

Wasalaam Lady f Y
 
Haya mama, nadhani watakuwa wamekusikia, watajirekebisha....
 
Hayo ni maisha walioyachagua. Hakikisha nyumbani kwako ni kusafi kama unavyotaka.
 
Hapo kwenye upande wa wanaume kuwa wachafu mbona umetumia maneno makali sana ama kote ulikuwa unazuga zuga tu lengo lako lilikuwa ujumbe huo kwa wanaume...Ok point taken madam.
 
Mwadela mayo mnaendeleaje mabestito wangu nimewamiss sana,

Imenibidi leo niingie tena hapa kutoa dukuduku langu la moyo kwani imenishangaza sana tena sana Jumapili iliyopita mabestito wangu wa ukweli nilikwenda mahali fulani kwa mabest wangu kuwajulia hali nilipofika mlangoni aghalabu kama si kushangaa sana jamani nikakutana ana na ana na kinyesi mlangoni, nami kwa haiba nyembamba nikakiruka na kubisha mlango na kukaribishwa ndani.

Kuingia tu mule ndani nikaonana nao wenyewe hawana habari kuwa mambo si shawari mlangoni pao, wameketi wanakodolea mimacho TV sijui kipindi gani kiilikuwa kinaendelea , kuangalia vyema mezani jamani niilishangazwa sana na kuona ukoko wa chakula huku wenyewe hawana habari kwa kwelil ilinipa simanzi nikajisemea moyoni hawa wanandoa wako hapa wenyewe wanaenjoy huku uchafu umewakalia kila kona ni nini hiii jamani.

Basi bila ajizi ikanibidi niage kiaibu aibu kwani niliona hapa sasa shida, wapendwa wangu wangu kwanini nimeleta kisa hichi hapa nimetaka tujiifunze kwa kisa hichi hapo juu mambo ya afya hususani afya zetu na sehemu tuishizo au sehemu zitungukazo wapendwa msijesema kwanini leo LADYF nimesema hivi imenikera kuona baadhi ya wanandoa hasa watoto wa kike kukaa mahali au eneo la home kwako likiwa limezingirwa na uchafu.

Hivi hatujui kuwa uchafu unaleta magonjwa jamani hivi kwanini hutaki kufanya usafi haata wa nguo zako jamani, imenibdi niwape somo kidogo hapa kwa wale ambao wamezoea kuwa wachafu wajirekebishe kwani chafu unakera na ni mfumuko wa maradhi mabaya, mabestito ambao mko kwenye mahusiano au ndoa jirekebisheni.

Ukiona mwenzio mchafu basi ongea nae kwa upendo na atajirekebisha uchafu mwingine uko kwa wanaume jamani usiombe mwanaume akuvulie nguo huo uvundo utakaotoka hapo utadhani kinyesi kimeoza miezi 7 kumbe ni misoski au manguo ya ndani hayajafua miezi sasa sasa hapo bestito wa kiume unamkomoa nani kama sio kujikomoa wewe mwenyewe na kujipa magonjwa yasioyoponyeka.

Na hii tabia kadhalika iko hata upande wa pili wa wanawake jamani acheni kuwa wachafu kwani uchafu huleta magonjwa na ni adua mkubwa sana kwako wa maendeleo ukiwa unaumwa utawezaje kufanya kazi , utawezaje kujiendeleza, mabestito tabia ya uchafu ni dhambi.

Wasalaam Lady f Y

Wee ni mnafki rfk mkuda kwa mwenzio. Mio huwa mdomo wangu nauvuaga chupi kwa mtu mwenye maswala hayo, biibiwee siondoki nimevimbiwaaa kbsaa namchana liveee natembea mbeleee kwake siendi teena ili ajue nilipachukia na mtu wa nyumba ya dizaini hiyo hata kama nazimia mayi kwake ctak acha nifee..
 
Back
Top Bottom