Yaani hata kama mtu hutatoa shukrani ila umjulishe tu alietuma kua hela imefika, lakini unakuta unamtumia mtu ikishafika ndio anapotea moja kwa moja hatoi shukrani wala hasemi kama hela imefika.
Hizo ni tabia za walio wengi waafrika tunatakiwa tubadilike ndiyo maana hata Wabunge wa CHADEMA walichukua posho na kuondoka bungeni bila kuhudhuria, bado tunasafari ndefu sana kufikia ustaraabu.
Tatizo mnakera mno ,unakuta mtu namba yako anaifahamu , majina yako unayotumia anayajua yote
Bado akituma hata dk kadhaa hazijapita anauliza umepata? Agrrr mnakera
Hatufundishi watoto kushukuru wanaposaidiwa. Wakiwa watu wazima hivyo hivyo, hawashukuru kwa kitu chochote. Kila kitu wanaona ni haki yao tu. Siyo kwako tu. Inatokea mara nyingi sana. Hata wanaojiita wasomi ni hivyo hivyo. It is sad.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.