TABIA ya kuficha hela sio nzuri

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,554
44,725
Kuna mdada aliuza nyumba millioni 60 maeneo ya ubungo Kama mnavyojua kifo Ni anytime yule dada akaumwa ghafla akafa baada ya Kama week mbili.huwezi amini hela zimetafutwa kote zimekosekana bank account zote hakuna hata shilingi sijui inaonekana alizificha sehemu na hakumwambia yoyote kaacha watoto wawili hawana hili Wala lile.inawezekana hata alizifukia sehemu zinajiozea.

Kuna kisa kingine Tena Kuna baba alinunua nyumba kisiri Siri bila kumwambia mke wake akawachukua na familia akawapeleka kwenye hiohio nyumba akajifanya amepanga hio nyumba analipia Kodi ya mwaka.

Siku ya siku huyo mbaba akafa kamwacha mke anasubiri mwenye nyumba aje wamekaa miezi sita hawajaona mwenye nyumba akija mpaka baadae marafiki wa mume wake wakamwambia ukweli kuwa hio nyumba Ni yao.

Yule mama hakuamini akashikwa na stroke na yeye akafa pale pale

Kimsingi yako matukio mengi Kama haya ya kuficha utajiri unakuta mtu una mihela huko sijui ya ufisadi au yatokanayo na money laundering unakaa nayo Kama Siri siku ukifa hata watoto wako hawapati chochote kwa sababu account ya ulipozificha hizo pesa za uharam hakuna anayeijua.

Maisha ya sirisiri mwisho wake huwa mbaya utaishia kufa kwa pressure.
 
Huyo dada wa ubungo mlijuaje kama kaficha? Je kama alihonga

Siyakukothamela Sonini na nini
 
Back
Top Bottom