Tabia ya kuegemea magari ya watu

Tabia ya kuegemea magari ya watu

watu washaanza kutetea magari yao ya mkopo kwakuwa sasa benki zinadai na zinafilisi , unanyima hata watu wasiegemee ndinga yako,
 
huyyu hate home inaonekana bado yuko miaka 25 iliyopita au 30 enzi za baba kufungia TV kabatini [ wengi Tv walikuwa wanazionea kwa jirani ...],,,,alafu ikaja TV kuwa sitting room lakini kwenye grill la chuma kama bar,alafu ikaja tv kuwa kwenye kabati la mbao linafunguliwa wazee wakirudi ..
Ikaja enzi sasa ya kati kati kabla hajaingia mkapa ...mwinyi anakaribia kutoka TV inakuwa sitting lakini imefunikwa na Kitambaa cha kufumwa na mama , .....ikaja sasa TV angalau zinakua mbili nyumbani .......sasa nyumba nyingi middle class kila room ina TV FLAT ..

Genesisi
umenikumbusha marehem dingi
 
hahahaah
Wasamehe Mkuu
Nilishawafuma watoto wa kike wakipiga picha kwenye Gari langu
Lakini Pia nilishawafuma Vijana wakichukua masefie ktk Chombo yangu
Ndiyo Maisha yetu Ndugu, Tuvumiliane.
 
Huo ni unyanyasaji, fanya tathimini upya na usithamini sana kitu ambacho hakita kuzika.
 
hahahaah
Wasamehe Mkuu
Nilishawafuma watoto wa kike wakipiga picha kwenye Gari langu
Lakini Pia nilishawafuma Vijana wakichukua masefie ktk Chombo yangu
Ndiyo Maisha yetu Ndugu, Tuvumiliane.

Inaonekana una gari zuri sana. Na mimi naomba selfie kwenye gari yako mkuu.
 
Hii tabia ya kuegemea magari ya watu hovyo hovyo tu ipo sana hasa hasa jijini Dar Ee Salaam. Umepaki gari lako, salama bin salmin kutoka na kurudi unakuta Jitu limeegemea garil lako, tena kwenye taa, halijui hata bei ya taa wala rangi. Hii tabia ni kero sana naomba ikomeshwe.
Inategemea na gari.....sasa kama unayo passo na wewe utalalamika kweli au unatania
 
Kukosa kwenu magari au kuwa mafukara ndio mumshushie mdau matusi?

Tabia ya kuegemea magari ya watu si nzuri. Kuna ulazima gani wa wewe na hayo makalio yako yaliyokuzidi uzito kiasi unatafuta pa kujisapoti kwenda mjini?

Nendeni mkaegemee yale ya zimamoto, yale ndio ya wote.
 
Tabia mbaya ni tabia mbaya. Haijalishi kama ni vits ya kwanza ya mkopo ambayo haijafikisha mwezi au la. Heshimu mali ya mtu huna haki ya kumpangia.

And while we are on the subject respect my personal space too. If you are behind me in a queue back up a little, I don't need to hear you breathing.
Wewe lazima umeishi kulee....bongo hamna ustaarabu huo. Nilipata shida sana siku za mwanzo,foleni benki mtu anakukaribia hadi anakugusa unabaki unamuangalia hata msg hapati....watu hawaheshimu mali ya mtu na unaweza kusoma hata michango yao ya dharau kwa aina fulani ya gari. Kama vits,passo ni yake usiegemee heshimu mali yake.
 
Wamenikwangulia rangi sana sana na sarawili za jeans, zipu wakigeuka zinakwangua rangi. Ni tabia mbaya sana kusema ukweli japo watu wanaona mwenye gari anajidai. Niliwahi kukuta wamelia hapo chips na soda gari wameigeuza meza.....
Kuna watoto nilikuta wamefanya gari langu ubao wa shule.....wamekwangua 1+1=2, 2+2=4......
 
huyyu hate home inaonekana bado yuko miaka 25 iliyopita au 30 enzi za baba kufungia TV kabatini [ wengi Tv walikuwa wanazionea kwa jirani ...],,,,alafu ikaja TV kuwa sitting room lakini kwenye grill la chuma kama bar,alafu ikaja tv kuwa kwenye kabati la mbao linafunguliwa wazee wakirudi ..
Ikaja enzi sasa ya kati kati kabla hajaingia mkapa ...mwinyi anakaribia kutoka TV inakuwa sitting lakini imefunikwa na Kitambaa cha kufumwa na mama , .....ikaja sasa TV angalau zinakua mbili nyumbani .......sasa nyumba nyingi middle class kila room ina TV FLAT ..

Genesisi
nimecheka hadi kichwa kinauma!
 
Wewe lazima umeishi kulee....bongo hamna ustaarabu huo. Nilipata shida sana siku za mwanzo,foleni benki mtu anakukaribia hadi anakugusa unabaki unamuangalia hata msg hapati....watu hawaheshimu mali ya mtu na unaweza kusoma hata michango yao ya dharau kwa aina fulani ya gari. Kama vits,passo ni yake usiegemee heshimu mali yake.
Hahahaha....."hata msg hapati" mwingine anajikata kucha kwenye public transport,ilibidi nishukie njiani kwanza
 
Hahahaha....."hata msg hapati" mwingine anajikata kucha kwenye public transport,ilibidi nishukie njiani kwanza
Kuna namna mtu akikuangalia unapata msg.....sasa wengine hawajui hio na ukimwabia tu ugomvi!
 
Watu mnaotoa povu wengi wenu hamjua kero ya hii tabia ya mtu kakaa mahala kaweka limwil lake kwenye bonet ya gari. Hii tabia hata mimi inanikera sana kwanza nimeshanyoosha bonet kama mara 5 hivi mtu anakaa gar zenyewe zina bodi nyepes yye analala hapo. Kwakwel mm nikimkuta lazima nimpe kubwa
Kumbuka pia uongo ni Mbaya...
 
Hahahaha....."hata msg hapati" mwingine anajikata kucha kwenye public transport,ilibidi nishukie njiani kwanza
Hii mara ya mwisho hata wiki mbili haijapita kwenye fastjet, mtu katoa nail cutter kabisa mfukoni, sijui kaipitishaje. Nasikia clipping sound kutazama mtu na heshima zake hana habari.
 
Gari la kwanza na uzeeni lina heka heka duh nakumbuka nili park karibu na dirisha ili usiku niwe naliona.
 
Back
Top Bottom