Shayu
Platinum Member
- May 24, 2011
- 608
- 1,653
Hii tabia iliyojengeka kwa miaka mingi ya kuwachagua wabunge huku vijijini kwetu kisha wao kukimbilia dar es salaam lazima ife, lazima wanaharakati tupambane nayo, mbunge lazima aishi sehemu aliyochaguliwa lazima aishi na wananchi wake ayajue matatizo ya kila siku ya wananchi.
Hii tabia inakera na inaonyesha jinsi gani wabunge wetu wasivyojali wananchi bali maslahi binafsi, Huu upuuzi lazima ukomeshwe, natoa wito kwa wanaharakati wote wazalendo kusimama kidete juu ya hili, kama mbunge amechaguliwa sehemu ambayo haina maji aishe huko huko apatae tabu na wananchi wake ili apate uchungu wa kuwatetea, mbunge wa bumbuli lazima aishi bumbuli sio dar, wa kigoma kaskazini hivyo hivyo nk, umefika wakati tunyanyuke na tupige hatua moja ya kizalendo kuwaadabisha wawakilishi wetu wapenda raha, sisi wananchi wa jamhuri ya muungano wa tanzania ndio wenye mamlaka ya mwisho juu ya nchi yetu na hatujachagua wabunge ili wale anasa bali watutumikie.
Na safari za jk nje lazima tuziangalie upya lazima tuandamane, kujadili mwelekeo wa nchi yetu , tuna matatizo mengi nchini kwetu ambayo tunaona raisi wetu ameshindwa kutupa majibu sahihi.
Tunahitaji jukwaa la pamoja kujadili matatizo yanayotukabili, umoja wetu unayumba sababu ya ubinafsi, kutowajibika kwa viongozi wetu, kushuka roho ya uzalendo miongoni mwa watu wetu, Raisi wa nchi hii ameshindwa kutatua matatizo haya ikiwemo suala la muungano. na wabunge wameshindwa ni wajibu wetu kutoa sauti yetu dhidi yao na kuwaambia tumewachagua kututumikia sio kustarehe sio kujipatia mali au kutafuta umaarufu
Ni wakati wetu vijana wa taifa hili, ni wakati wetu! Taifa linakuhitaji, katika wakati kama huu wa sintofahamu, taifa linakuhitaji sauti yako inaweza kuleta mabadiliko dhidi ya unafiki wa wanasiasa uchwara, tujenge tanzania mpya yenye umoja, upendo na mashirikiano, NI SAUTI ZETU ZA PAMOJA TU KAMA WANANCHI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI ZITAKAZO TUOKOA
Mapinduzi ya misri na tunisia yalikuwa ya wananchi wenyewe na sio wanasiasa walikerwa na tabia za viongozi wao za unafiki na ubinafsi na Tanzania ya leo tunajionea mambo haya, Tunanyanyuke na tunyanyue sauti zetu kabla mambo hayajaharibika, tupige kelele kwa nguvu zete UKOMBOZI, UKOMBOZI, UKOMBOZI, UKOMBOZI, lazima tutengeneze nguvu mabayo mamlaka itatuheshimu! Unyonge wetu ndio umetufikisha hapa, tumevumilia vya kutosha! Na Sasa ni wakati wetu.
Vijana popote mlipo hii ni nchi yenu mna haki nayo, baadae ya nchi hii inawategemea nyie na ni jukumu la kila mzalendo akiona nchi yake ikiendeshwa sivyo kupiga hatua moja mbele ya kizalendo na kudai mwelekeo na dira sahihi, Mwelekeo wa nchi yetu sio! Kama ungesikia sauti yangu, ningekupigia kelele, ukombozi! ukombozi! ukombozi! Nchi yetu imekosa dira nami sijui who is incharge of this country!
Vizazi vyetu vinakosa mwelekeo nami nalia kwa uchungu kama mwanamke anayetaka kuzaa! Umoja wetu ndio silaha yetu dhidi ya wasaliti, tuliowatuma kututumikia na kutugeuka na kutufanya watumwa wa kuwatumikia, Uhuru wetu mashakani, mioyoni mwetu umetoweka kama barafu iyayukakayo nami nalia kwa bwana wa majeshi, mungu mwenye nguvu ni hadi lini taifa hili litaendelea kuwa hivi? Tuna madini na kila kitu lakini maskini!