Tabia hii ya kuchagua wabunge na wao kuhamia mjini lazima ife | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tabia hii ya kuchagua wabunge na wao kuhamia mjini lazima ife

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Shayu, Sep 20, 2011.

 1. Shayu

  Shayu Platinum Member

  #1
  Sep 20, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 506
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 180
  Hii tabia iliyojengeka kwa miaka mingi ya kuwachagua wabunge huku vijijini kwetu kisha wao kukimbilia dar es salaam lazima ife, lazima wanaharakati tupambane nayo, mbunge lazima aishi sehemu aliyochaguliwa lazima aishi na wananchi wake ayajue matatizo ya kila siku ya wananchi.

  Hii tabia inakera na inaonyesha jinsi gani wabunge wetu wasivyojali wananchi bali maslahi binafsi, Huu upuuzi lazima ukomeshwe, natoa wito kwa wanaharakati wote wazalendo kusimama kidete juu ya hili, kama mbunge amechaguliwa sehemu ambayo haina maji aishe huko huko apatae tabu na wananchi wake ili apate uchungu wa kuwatetea, mbunge wa bumbuli lazima aishi bumbuli sio dar, wa kigoma kaskazini hivyo hivyo nk, umefika wakati tunyanyuke na tupige hatua moja ya kizalendo kuwaadabisha wawakilishi wetu wapenda raha, sisi wananchi wa jamhuri ya muungano wa tanzania ndio wenye mamlaka ya mwisho juu ya nchi yetu na hatujachagua wabunge ili wale anasa bali watutumikie.

  Na safari za jk nje lazima tuziangalie upya lazima tuandamane, kujadili mwelekeo wa nchi yetu , tuna matatizo mengi nchini kwetu ambayo tunaona raisi wetu ameshindwa kutupa majibu sahihi.

  Tunahitaji jukwaa la pamoja kujadili matatizo yanayotukabili, umoja wetu unayumba sababu ya ubinafsi, kutowajibika kwa viongozi wetu, kushuka roho ya uzalendo miongoni mwa watu wetu, Raisi wa nchi hii ameshindwa kutatua matatizo haya ikiwemo suala la muungano. na wabunge wameshindwa ni wajibu wetu kutoa sauti yetu dhidi yao na kuwaambia tumewachagua kututumikia sio kustarehe sio kujipatia mali au kutafuta umaarufu

  Ni wakati wetu vijana wa taifa hili, ni wakati wetu! Taifa linakuhitaji, katika wakati kama huu wa sintofahamu, taifa linakuhitaji sauti yako inaweza kuleta mabadiliko dhidi ya unafiki wa wanasiasa uchwara, tujenge tanzania mpya yenye umoja, upendo na mashirikiano, NI SAUTI ZETU ZA PAMOJA TU KAMA WANANCHI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI ZITAKAZO TUOKOA

  Mapinduzi ya misri na tunisia yalikuwa ya wananchi wenyewe na sio wanasiasa walikerwa na tabia za viongozi wao za unafiki na ubinafsi na Tanzania ya leo tunajionea mambo haya, Tunanyanyuke na tunyanyue sauti zetu kabla mambo hayajaharibika, tupige kelele kwa nguvu zete UKOMBOZI, UKOMBOZI, UKOMBOZI, UKOMBOZI, lazima tutengeneze nguvu mabayo mamlaka itatuheshimu! Unyonge wetu ndio umetufikisha hapa, tumevumilia vya kutosha! Na Sasa ni wakati wetu.

  Vijana popote mlipo hii ni nchi yenu mna haki nayo, baadae ya nchi hii inawategemea nyie na ni jukumu la kila mzalendo akiona nchi yake ikiendeshwa sivyo kupiga hatua moja mbele ya kizalendo na kudai mwelekeo na dira sahihi, Mwelekeo wa nchi yetu sio! Kama ungesikia sauti yangu, ningekupigia kelele, ukombozi! ukombozi! ukombozi! Nchi yetu imekosa dira nami sijui who is incharge of this country!

  Vizazi vyetu vinakosa mwelekeo nami nalia kwa uchungu kama mwanamke anayetaka kuzaa! Umoja wetu ndio silaha yetu dhidi ya wasaliti, tuliowatuma kututumikia na kutugeuka na kutufanya watumwa wa kuwatumikia, Uhuru wetu mashakani, mioyoni mwetu umetoweka kama barafu iyayukakayo nami nalia kwa bwana wa majeshi, mungu mwenye nguvu ni hadi lini taifa hili litaendelea kuwa hivi? Tuna madini na kila kitu lakini maskini!
   
 2. Shayu

  Shayu Platinum Member

  #2
  Sep 20, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 506
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 180
  Woga wetu utatufanya tusiendelee lazima tupige hatua moja mbele ya kizalendo kudai haki zaidi, uhuru zaidi na uwajibikaji katika nchi yetu wenyewe.
   
 3. Shayu

  Shayu Platinum Member

  #3
  Sep 22, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 506
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 180
  ndipo tutakapofanikiwa.
   
 4. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #4
  Sep 23, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,688
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  mkuu ni kweli tupu wanatuyayusha sana hawa Wabunge we angalia Mbunge wa Mafia eti anapiga kelele kuhusu UDA cjui inamuhusu nini wakati Mafia hakuna usafiri wa uhakika. Lkn nina swal, hivi tukifanikiwa kumuondoa Jk ni nani atakaa madarakani?
   
 5. Shayu

  Shayu Platinum Member

  #5
  Sep 23, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 506
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 180
  Kazi ngumu tuna leadership crisis, huyo wa mafia anamatatizo badala aongelee matatizo ya mafia anaongelea shirika la usafiri la dar es salaam? Wabunge wetu wanataka sifa tuu hakuna cha maana , ngoja nikwambie ukweli hata tukiwaondoa ccm mambo yatakuwa yaleyale kwakuwa chadema hawana nidhamu pia hawana tofauti na ccm, tofauti iliyopo ni kwamba ccm iko madarakani wao hawako, CCM NA CHADEMA ni kama mbwa Wanaogombania nyama ukweli ni kwamba ukombozi wa kweli kwa nchi yetu bado, true leader talk about unity chadema hawaongelei hilo, kila chama chadema na ccm wanatumia kila mbinu katika siasa na hii ni alama ya uchu, lakini mimi nasema katika taifa hili kuna watu, watu bora wanaangalia tu mwelekeo unavyokwenda wakati ukifika wito wakizalendo utatufanya tu act kulikomboa taifa hili dhidi ya walafi, watu wanaotafuta umaarufu binafsi na utajiri kupitia utumishi wa umma.
   
 6. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #6
  Sep 23, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,053
  Likes Received: 7,259
  Trophy Points: 280
  Mtu kama Kafumu ukimuangalia tu si mtu wa kuishi Igunga kabisa yule!!
  Na mijitu bado itamchagua tu.
   
 7. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #7
  Sep 23, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Umekaa ukatafakari ukayaona hayo je ni bora ccm? Tafakari kwa zaidi maana naona kama umekurupuka
   
 8. Shayu

  Shayu Platinum Member

  #8
  Sep 23, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 506
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 180
  Mimi sio mtu wa mkumbo sawa? Ccm ni mbovu nakubali ndio maana chadema wanapata nguvu lakini chadema sio chama kitakacho tukomboa ,hawatokuwa tofauti na ccm, kama wewe ni mtu makini utaliona hilo can you put your trust on chadema? Issue we have katika nchi ni ukame wa viongozi, siasa yetu imekuwa unafiki na maneno ya kihuni yasiyojenga, wote chadema wana uchu na wala sio nia ya dhati ya kujenga nchi hii, wala kuleta watu wa taifa hili pamoja, Ni jukumu letu ku address matatizo yanayotukabili na kuwawajibisha wanasiasa kwa pamoja kwa kuwaambia nini tunataka, umoja wa nchi yetu unayumba, wanasisasa wanatugawa kwa personal gain, sitashangaa nchi hii ikidumbukia kwenye vita kwa jinsi hali ilivyo, viongozi wetu wahuni na hawawezi kumuongoza yeyote ikiwa wao wenyewe hawawezi kujiongoza, Tunahitaji mtu anayejiheshimu atakayetujengea jamii yetu sio viongozi wanaotukana jukwaani, Tunamatatizo mengi katika taifa hili hayo yote yanahitaji kiongozi makini na mwenye busara atakayetuleta pamoja, na kuileta social order iliyovurugika kabisa kwa sasa, nchi yetu ina viongozi wanaopiga domo lakini sio wawajibikaji, tunahitaji mtu atakayetuleta pamoja na kujenga uzalendo kwa watu wetu wote, tuunde upya mifumo ya nchi yetu na taasisi za kutoa haki zijengwe upya, Moyo wakujitolea ujengwe miongoni mwetu, we must have social bond.
   
 9. N

  NCHABIRONDA JF-Expert Member

  #9
  Sep 24, 2011
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 238
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kama na nyie akina dada siku hizi mmeanza kuwa na mawazo mazuri kama haya! basi kumbe tutafika. Big up sana.
   
 10. Shayu

  Shayu Platinum Member

  #10
  Sep 24, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 506
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 180
   
 11. wijei

  wijei JF-Expert Member

  #11
  Sep 24, 2011
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 469
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Nadhani huo ni mtazamo wako ambao vilevile unaweza usiwe sahihi.nadhani unafanya makosa kuwahukumu cdm=ccm.swala ni kwamba ccm wameshindwa kuongoza nchi,hata cdm wasingekuwepo ni kwamba watu tumechoka na hii misisiem.isipotaka kuondoka madarakani kwa njia ya demokrasia nadhani ya Tunisia hayaepukiki.
   
 12. Shayu

  Shayu Platinum Member

  #12
  Sep 24, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 506
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 180
  We can not have economonic prosperity if we doesn't have a social order, we must have social order first the economic prosperity will follow. Political party which will bring order in this country must have order within itself, THERE is no order in chadema, there is no wisdom in chadema , in this nation since mwalimu death we have lack of leadership, i don believe slaa or mbowe will bring economic prosperity and social order in this country. Ccm is the worse they are are corrupt, citizen are fed up with them, the only party they see is chadema becouse they say bad things abt ccm but that doesn't make them good, we wan't to hear from them discussing issues, this country face alot of challenges, unity collapsing, lack of social order nk what we need is the leader who will bring us together to solve our core issues face our generation. Chadema they don't do that, they travel each corner of our country taliking about ufisadi, ufisadi, Both ccm and chadema are all corrupt, they just fight for personal gain, nilisoma article moja humu ndani ya jf chadema wamejaa ndugu , jamaa na marafiki kwenye ubunge wa kuteuliwa kama ccm walivyojaa, kwahiyo tusijidanganye hapa, tatizo tulilonalo hapa ni uhaba wa viongozi na tunatakiwa tu address matatizo yanayotukabili kwa pamoja, tunaviongozi wasiowajibika kwa taifa, wala kwa jamii. wabunge wanaochaguliwa vijijini na kuhamia mjini wakiacha wajibu wao kwa taifa na kwa jamii, wakiishia dar es salaam kupata raha. Ifike wakati watu wa taifa hili tujifunze kujitolea kwa faida ya nchi yetu. Nchi yetu iko katika hali mbaya, ubinafsi unatutafuna, tunasahau majukumu yaliyotufanya tuwe taifa, yaliyotufanya tuwe wamoja, ni wajibu wetu kama wananchi kuongea ukweli na kuwawajibisha viongozi wa kisiasa, wanafiki waliojaa katika taifa hili, ili kurejesha upya mwelekeo na na heshima ya taifa hili.
   
Loading...