Tabata

Tabata

Mentor

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2008
Posts
20,334
Reaction score
23,940
TABATA
October 06, 2009 Siku ya Jumanne.
Background:
Nilikuwa nimemaliza zangu chuo MUCCoBS kozi ya BAF na kufanikiwa kupata GPA nzuri tu ya 4.2. Nilikuwa na matumaini na ndoto nyingi za mbeleni juu ya maisha yangu. Nilipenda sana elimu na nilitegemea kupata nafasi ya TA (tutorial assistant) chuoni hapo.

Wakati nangojea graduation ambayo huwa mwezi November, nilikuja Dar es salaam kumtembelea dada yangu ambaye alikuwa akiishi huku, Tabata! Naye ndo kwanza alikuwa na mwaka mmoja kazini ila kwa bahati (nzuri?mbaya?...sijui) alipata uja uzito na mshkaji mmoja hivi walisoma naye chuo.

Basi nikawa nakaa naye pale huku nikingojea siku zisonge.

October 06, 2009 siku ya Jumanne:
Siku hii alitakiwa kwenda clinic na kwa vile alikuwa karibu sana na kujifungua hakuweza kuendesha gari ikabidi nimsindikize kwenye zahanati moja pale Tabata nimeisahau jina.

Basi wakati namngojea nikaenda kukaa kwenye mabenchi Fulani pembeni pale kuangalia TV. Karibu yangu alikuwa amekaa binti mmoja mrembo sana kwa kweli. Sikufahamu yupo pale kufanya nini. Nilidhani na yeye kaja kumsindikiza ndugu yake labda.

Mimi bila hiyana nikaacha kuangalia TV nikaanza kupiga stori za hapa na pale. Tukakonekt vizuri na kuchangia changia mada iliyokuwa inaonyeshwa kwenye TV. Baada ya kama nusu saa dada naye akatoka ndani akaja tuondoke. Nikamwambia dada kama hutojali unipatie namba yako tuzidi kuwasiliana.

Baada ya siku ile tuliendelea kuwasiliana sana tu. Tulikuwa tuna chat mpaka ma saa sita ya usiku na ukizingatia sikuwa na kazi. Aliniambia yupo chuo mwaka wa tatu anasoma Sheria.

Moyoni nilihisi hapa nimepata mtu lakini kama nilivyofundishwa sikuwa na papara ya kumtamkia hayo. Bado ninakumbuka maonyo niliyopewa juu ya jiji hili la Daslam!

Baada ya wiki mbili hivi tulikutana for lunch posta..enzi hizo break point bado mpya kabisa. Tuliongea mengi about life.

Tabata:

Wiki moja kabla ya graduation nilimwambia naenda zangu Moshi wiki ijayo hivyo ningependa tuonane. Alikubali na kuja Tabata jioni. Tulikaa tukala na kupiga stori mpaka mida kama saa sita ivi. Nikatumia mbinu za medani za kivita kumshawishi kwamba kwenda hostel kwao mida hiyo ingekuwa ngumu ilhali tungeweza kuchukua tu chumba hapo asubuhi arudi chuoni. Of course, strawberry lips na contessa vilichangia kunisaidia kumfanya akumbali. Ila alikuwa amekataa sana mwanzoni.

Tulienda guest moja inaitwa MUNGU ANAKUONA GUEST HOUSE & RESTAURANT. Nikalipa pale tukaingia ndani.

Kazi ikaanza kuomba game ila haikuwa ngumu…long liiive govinder kumar! Basi purukushani za hapa na pale za kujiandaa na game na mimi kwa kuwa nilichanganya Contessa gin na White horse nikasahau kabisaaa matumizi ya kinga.

Nikaenda zangu graduation November na kurudi. Nikawa nimempotezea kabisa Yule binti kama ilivyo kawaida yetu baada ya kupata tunda.

Jana, March 17 2013 Jumapili:
SMS: "Ndugu yangu, kama umenichunia sawa ila mbona hata sikuoni tena hospitali?"
Nikashtuka hospitali? Si ikabidi nimpigie!!!
Ananiambia: "Si pale Tabata sikuoni ukija tena kuchukua ARVs"

Conclusion:
Kumbe benchi nililokuwa nimeenda kukalia ile siku lilikuwa la wagonjwa wa UKIMWI nay eye alikuwa akisubiri kuchukua dawa.
Mimi nikamwambia acha kunidanganya mbona wewe unaishi hostel Kigamboni na ninajua hivyo..yani huko kote hakuna dispensary?
Akaniambia wagonjwa wengi hawaendi kuchukulia dawa karibu na kwao kwa kuhofia kunyanyapaliwa hivyo alijua na mimi nipo kwenye foleni ya kuchukua dawa ndiyo maana hakuona umuhimu wa kunilazimisha kutumia kinga.

Nilishtuka...nikazimia…ndo nimeamka leo..

Wasalaam wapendwa,

Mentor.
 
Pole sana jamaa wewe !!
Umeponzwa na mambo mawili tu hapo, zinaa na pombe.
Hii iwe funzo kwa wote ambao wanaendekeza zinaa na pombe.

Sasa angalia neno la Mungu linavyosema kuhusu zinaa na pombe.

01 Wakorintho 06:18-20 inasema....
18 Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.
19 Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;
20 maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.

01 Petro 04:01-05 inasema....
1 Basi kwa kuwa Kristo aliteswa katika mwili wake, ninyi nanyi jivikeni silaha ya nia ile ile; kwa maana yeye aliyeteswa katika mwili ameachana na dhambi.
2 Tangu sasa msiendelee kuishi katika tamaa za wanadamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wenu uliobaki wa kukaa hapa duniani.
3
Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi, na karamu za ulafi, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali;
4 mambo ambayo wao huona kuwa ni ajabu ya ninyi kutokwenda mbio pamoja nao katika ufisadi ule ule usio na kiasi, wakiwatukana.
5 Nao watatoa hesabu kwake yeye aliye tayari kuwahukumu walio hai na waliokufa.
 
ingekuwa kweli hata vidole vyako visingetype hapa ni mavi na uharo tu ungekutoka kila ukikumbuk ausicheze na majibu hayo hohohohooooooooo
samahani usinitafute kuhusu mdogo wangu wewe Mentor wala usiniite shemeji tena usintake ugomvi
cc: Nicas Mtei
 
Last edited by a moderator:
::
Haa! Tabata
Mentor
Vipi utaenda kuchukua ARVs?
::
Inafundisha,Inaonya,Inaelekeza.
Thanks
=
 
Na neno linasema, "..kwa mtini mjifunze..." #natumai umejifunza jambo ndugu yangu...

Unajua sana kutunga story naftilia threads zako mule mule big up broda
Jipu, stori gani nimeshaandika ndugu yangu..au unanifananisha na CHAI CHUNGU?
hii ni ya kweli...
 
Last edited by a moderator:
Safi sana ndo faida ya kuparamia watu

Ndugu yangu usihukumu usije ukahukumiwa...bado nangojea majibu!!!

ingekuwa kweli hata vidole vyako visingetype hapa ni mavi na uharo tu ungekutoka kila ukikumbuk ausicheze na majibu hayo hohohohooooooooo
samahani usinitafute kuhusu mdogo wangu wewe Mentor wala usiniite shemeji tena usintake ugomvi
cc: Nicas Mtei

Shemeji Nivea hata majibu bado mmeshaanza kuninyanyapaa kweli??! Inawezekana sikuathirika maana tangu mwaka 2009 mpaka leo nadunda tu na afya tele...shemejiii!!!:crying:
 
Last edited by a moderator:
Suala la Ukimwi sio a kuchekana. uwe nao usiwe nao huwezi/hupaswi kumcheka mwenzio.
kama huna sio kua we ni mjanja nikuatu hujaupata, na kama umeupata sio kua wewe ni mjinga, ni kuatu
umekutana nao kwa kua upo katika jamii hii hii tuliopo sisi.unaweza kutulia sana akakuletea mwenzio....!
Tunachoweza kufanya ni kujifunza kurahisisha pale tunapoambiwa ka 'TUMEATHIRIKA"
Eee mwenyenzi Mungu uturehem na janga hili. Ameni.
 
Mh kizazi hiki kitaangamia sana!
Pamoja na uelewa mkubwa watu walionaom juu ya HIV bado mtu anathubutu kuweka maisha yake rehani.

Na hivi VIMWANA MOTO NA WAVULANA WATANASHATI MH HATARI KWELI KWELI!
 
Tabata siendi tena..Tabata siendi tena..Tabata siendi tenaa, kuna dogodogo nyingi!!

Nangojea majibu Tetra ndo nijue.

Ila Tabata sikanyagi tena huko kwa kina Mtambuzi et al...
Ha ha ha ha haaaaaam Mkuu Mentor, si ulinambia hii ishu ni siri yako siku zile ulivyonisimulia, yaani umeamua kuweka mambo hadharani....
Umenichekesha sana mpaka mbavu zinauma kwa kicheko, kumbe ni Tabata ni hatari eh............... LOL
 
Last edited by a moderator:
We Mentor wewe!hayo maishu yalikukuta au ni utunzi wa stori tu?em funguka banah.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom