mitindo huru
JF-Expert Member
- Apr 26, 2016
- 1,607
- 1,596
Hizi salam ziwafikie mkuu wa mkoa wa Dar ndugu Paul Makonda, mkuu wa wilaya ya ilala ndugu Mushi, mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya ilala ndugu Msongela Nitu Palela na pia meya wa wilaya ya ilala ndugu Charles Kuyeko, kwamba Tabata - Kinyerezi Mwisho ni sehemu hatari na inapaswa kuangaliwa kwa ukaribu kabla hayatokea maafa ya kutisha eneo lile kama ifuatavyo.
Tabata - Kinyerezi mwisho kuna stendi isiyo rasmi na pia kuna soko lisilo rasmi linahudumia idadi kubwa ya watu wa Kinyerezi na pia maeneo ya karibu kama Kifuru, Kibaga n.k.
Na pia ifahamike kuwa Kinyerezi ni moja ya eneo la wilaya ya ilala lililopimwa hivyo kuna eneo la stendi kwenye ramani ambalo hadi leo halijaendelezwa hadi leo bila taarifa na sababu yeyote na pia kwa sababu eneo la kinyerezi lilipimwa hivyo lina eneo rasmi ya soko ambalo limejengwa msingi na kuezekwa ila halina vyoo na hakuna huduma ya maji hali inayowafanya wafanyabiashara washindwe kuhamia katika soko hilo.
Lengo la kuandika taarifa hii ni kuwajulisha hatari kubwa inayoweza kutokea katika eneo la Kinyerezi Mwisho lisilo rasmi ambalo watu wanatumia kama stendi ya basi na pia soko kwa sasa, ilihali eneo hilo ni hatari kwa sababu ni eneo lililo chini ya nguzo za umeme zenye umeme mkubwa unaotoka katika mitambo ya kinyerezi ya kuzalisha umeme kwa njia ya gasi, kwani inakadiriwa umeme unaopita pale ni zaidi ya KWH 200,000 hadi KWH 2,000,000 hivyo endapo waya mmoja ukikatika utaleta maafa makubwa kwa watu wa eneo lile.
Wito wangu ni kuomba serikali ichukulie hili jambo kwa ukaribu sana kabla hayajatokea maafa makubwa pale Kinyerezi sababu kinyerezi imepimwa hivyo kuna eneo rasmi la stendi na soko , kwa hiyo hakuna sababu ya kuwaacha watu waendelee kutumia eneo la sasa kama stendi na soko ambalo ni hatari sababu ya umeme mkubwa unaopita pale juu.
Ni vizuri serikali ichukue mapema hatua ya kuwaamisha watu pale Kinyerezi mwisho ili waende eneo rasmi la stendi na soko ambayo ni salama zaidi kuliko kinachofanyika sasa.
Picha zinaonesha hali halisi ilivyo sasa pale Kinyerezi Mwisho sehemu isiyo rasmi kwa biashara na stendi

Attachments
-
1474488847070.jpg31.3 KB · Views: 148
-
1474488854024.jpg32.1 KB · Views: 111
-
1474488860500.jpg33.1 KB · Views: 112
-
1474488868840.jpg28.1 KB · Views: 108
-
1474488884111.jpg21.8 KB · Views: 104
-
1474488893263.jpg19.6 KB · Views: 90
-
1474488901571.jpg22.6 KB · Views: 89
-
1474488915090.jpg22.4 KB · Views: 85
-
1474488922900.jpg20.2 KB · Views: 94
-
1474488931706.jpg35.3 KB · Views: 90
-
1474488943253.jpg30.4 KB · Views: 88
-
1474488975840.jpg28.8 KB · Views: 86
-
1474488986031.jpg30.6 KB · Views: 84
-
1474488997260.jpg36.9 KB · Views: 90
-
1474489008941.jpg24.9 KB · Views: 88
-
1474489037571.jpg29.5 KB · Views: 92