Taasisi za ma-first ladies Tzania ni ulaji wao tu?

M-bongotz

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
1,734
405
Waungwana hili jambo linanitatiza sana kwa kweli, kuna hizi taasisi zinazoongozwa na wake wa marais hapa Tanzania, mfano tulikuwa na EOTF enzi za mama Anna Mkapa sasa tuna WAMA inayoongozwa na Shostito Mama Salma Kikwete, kinachonisumbua ni kwamba hizi taasisi huwa zinaanziwa kuwatafutia ajira kina mama hawa au vipi maana najiuliza EOTF imekwenda wapi, inamaana bi mkubwa aliondoka nayo walipohama ikulu ndipo mwenzake akaja na WAMA sasa jamani kwa utaratibu huu si ina maana hizi taasisi ni mali zao binafsi, kwanini mama Mkapa hakumwachia bi Salma ile taasisi aiendeleze?..
Kinachonisikitisha sasa ni kwamba taasisi hizi zinapokea misaada mingi toka kwa wahisani sasa kusipokuwa na uangalizi mzuri wa karibu kina mama hawa si wanaweza kufuja misaada hata isiwafikie walengwa?, nionavyo mie ni kwamba hii ni njia ya kuwatafutia ma-wife kitu cha kuwakeep busy na hakuna lolote jingine, huu ni ulaji wao tu..nyie mwaonaje?
 
Wajameni kuna mtu ambaye hajui utamu wa madaraka na uchungu wa kuondoka madarakani? Na hapa kama mama nyereere yupo atakuwa amelazimishwa. Ni sawa kanasa huu ni ulaji. Baba wetu wataafia alikuwa nanachomewa viazi ikulu sasa hivi sijui kunaendeleaje
 
jamani, ni vizuri mkajua kuwa zile ni taasisi zilizosajiliwa kama taasisis zisizo za kiselikali zikiwa na malengo mbalimbali.

kama taasisi nyingine, hazifungamani moja kwa moja na ikulu au madaraka ya rais. katika sajili, hazisajiliwi kama asasi za wake za marais, bali kama asasi huru zikiwa na bodi za wadhamini na timu za uendeshaji tofauti kwa mujibu wa sheria.

kwa maelezo haya, hakuna uwezekano wowote wa kurithishana ama kupokezana uongozi wa taasisi hizi kama iilivyo kwa wadhifa wa rais. hata mama salma akiondoka ataondoka na taasisi yake na mwingine akija ataamua mwenyewe kama atabaki kumchomea mzee viazi nyumbani au naye ataanzisha taasisi ya kumuweka bize.
 
...kwa maelezo haya, hakuna uwezekano wowote wa kurithishana ama kupokezana uongozi wa taasisi hizi kama iilivyo kwa wadhifa wa rais. hata mama salma akiondoka ataondoka na taasisi yake na mwingine akija ataamua mwenyewe kama atabaki kumchomea mzee viazi nyumbani au naye ataanzisha taasisi ya kumuweka bize.

Asante Mgombea Ubunge
 
jamani, ni vizuri mkajua kuwa zile ni taasisi zilizosajiliwa kama taasisis zisizo za kiselikali zikiwa na malengo mbalimbali.

kama taasisi nyingine, hazifungamani moja kwa moja na ikulu au madaraka ya rais. katika sajili, hazisajiliwi kama asasi za wake za marais, bali kama asasi huru zikiwa na bodi za wadhamini na timu za uendeshaji tofauti kwa mujibu wa sheria.

kwa maelezo haya, hakuna uwezekano wowote wa kurithishana ama kupokezana uongozi wa taasisi hizi kama iilivyo kwa wadhifa wa rais. hata mama salma akiondoka ataondoka na taasisi yake na mwingine akija ataamua mwenyewe kama atabaki kumchomea mzee viazi nyumbani au naye ataanzisha taasisi ya kumuweka bize.

Wake za viongozi sio lazima wawe na NGOs ili kuwakeep busy, kwani kutunza familia vizuri ni shuhuri tosha!! CHUKUA MFANO WA MKE WA MAKAMU WA RAIS, MAMA MWANAMWEMA SHEIN; yeye hana NGO lakini she keeps herself busy taking care of her family!!Hawaanzishi hizi taasisisi ili wawe busy bali ni njia ya kujiongezea ulaji wao na familia zao full stop.
 
I see it as just business at the state house! Period!

I agree with U sir.
Ukiangalia hata katika website ya WAMA, majina ya wajumbe wa bodi ni ya akina mama vigogo wa serikali na sisiemu, ambao wengine hawana uadilifu kabisa wa kuwa wanachama, achilia mbali ujumbe wa bodi.
Gonga hapa uwajue vema.
 
Nadhani Taasisi hizi zitaenda kutoa misaada kwa akina mama walioathirika na mfuriko pia. Hata kama walikuwa hawakumbuyki kuwa huko pia kuna wanawake, basi tumewakumbusha sasa.
 
Nadhani Taasisi hizi zitaenda kutoa misaada kwa akina mama walioathirika na mfuriko pia. Hata kama walikuwa hawakumbuyki kuwa huko pia kuna wanawake, basi tumewakumbusha sasa.

Kichuguu you are kidding!
Sitarajii kwamba WAMA au EOTF watapeleka chochote Kilosa kwenye mafuriko. They are not that generous!
 
IMG_7503mbrl2.jpg

Na kwanini hawa viongozi na waroho wengine wanapenda sana kuitumia hii jamii ya watu(pichani) kama namna ya ku'outsource misaada ya fedha toka kwa wafadhili?. And if you look out to what they actually get IN RETURN, out of the price of humanity they pay, ni peanuts!

Wanatumika kupigwa picha tu, mwisho wa siku wanapata zero!
 
jamani, ni vizuri mkajua kuwa zile ni taasisi zilizosajiliwa kama taasisis zisizo za kiselikali zikiwa na malengo mbalimbali.

kama taasisi nyingine, hazifungamani moja kwa moja na ikulu au madaraka ya rais. katika sajili, hazisajiliwi kama asasi za wake za marais, bali kama asasi huru zikiwa na bodi za wadhamini na timu za uendeshaji tofauti kwa mujibu wa sheria.

kwa maelezo haya, hakuna uwezekano wowote wa kurithishana ama kupokezana uongozi wa taasisi hizi kama iilivyo kwa wadhifa wa rais. hata mama salma akiondoka ataondoka na taasisi yake na mwingine akija ataamua mwenyewe kama atabaki kumchomea mzee viazi nyumbani au naye ataanzisha taasisi ya kumuweka bize.

Nothing kujulikana hapo!

Huwezi kutumia jina la 'first Lady' (ambalo hata ktk katiba halimo), ukasafiri kwa kutumia pesa za serikali halafu ukasema eti ni own initiatives.

Kule nje wanakotoa misaada wao hudhani kweli tuna kitu kiitwacho 'First lady' ktk mfumo wa siasa. Hutoa misaada kwake na kuishia saloon na kununulia vitenge na vilemba.
 
Back
Top Bottom