FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,506
- 123,777
Nadhani kuna wakati kichwa chako kinapata moto eeehhhhh
Ulitaka kiwe baridi kama chako? ngoja nikisha kufa.
Nadhani kuna wakati kichwa chako kinapata moto eeehhhhh
Nchi hutembeleana, wanapokuja hapa wakuu wa nchi za nje, hao wa Uingereza wameshakuja hapa pia, unafikiri kwanini?
Dunia hii utafanya maendeleo kwa kutegemea yako tu, hata China wanakaribisha wageni kuwekeza.
Ukiona hao viongozi wa mataifa yalioendelea wanakuja hapa ujue wamekuja kusaini mikataba ya kuhamisha rasilimali zetu, wanyama, gesi, madini.
Na wewe hutaki? kaa nazo uone zitakusaidia nini? utakufa na malaria tu ambayo mpaka leo hujapata ufumbuzi wa uhakika mpaka waje hao hao wa kutoka nje.
Tazama ulivyovaa, sasa hivi niambie ni nini cha Tanzania? tazama mawasiliano unayotumia sasa hivi, niambie ni nini cha Tanzania? sasa nenda kavae madini yako ufiche tupu, nenda kabebe gas yako uwasiliane, nenda kaandae wanyama wako usafirie, si huwa mnasafiri na fisi nyinyi? unangoja nini?
Kwa taarifa yako miaka ya 80, tulikuwa na viwanda vyetu vya kutengeneza nguo! MWATEX, URAFIKI na vingine vingi.Tulikuwa na kiwanda cha kutengeneza viatu BORA, Tulikuwa na kiwanda cha kuchonga almasi TANCUT, tulikuwa na viwanda vingi lakin serikali hii tukufu IKAVIPIGA MNADA KWA BEI ZA KUTUPA!!!
Hat hujui unachokiongea. Hayo mawe ya kuchongea almasi na mitamnbo uliitengeneza wewe? hivyo viwanda vya Mwatez na Urafiki ulivijenga wewe na mashine za Kitanzania? fikiri kidogo, kama jibu ni sio, ina maana lazima ukawabembeleze walete hivyo viwanda, ukita usitake, hauna ujanja wowote zaidi ya kulimwa tu ukipenda usipende.
Tumia akili dada yangu, leo hii pamba tunaiuza ikiwa ghafi, korosho inauzwa ghafi, katani inauzwa ghafi.iliwabidi hao wazungu wako waje kununua vitu ambavyo tayari vimechakatwa.lakini leo hii hata mchanga kutoka machimbo ya madini yanapakiwa ktk makontaina yanapelekwa kwa wazungu,
Tumia akili dada yangu, leo hii pamba tunaiuza ikiwa ghafi, korosho inauzwa ghafi, katani inauzwa ghafi.iliwabidi hao wazungu wako waje kununua vitu ambavyo tayari vimechakatwa.lakini leo hii hata mchanga kutoka machimbo ya madini yanapakiwa ktk makontaina yanapelekwa kwa wazungu,
Hivyo viwanda vya kuchongea almasi tukitumia fedha zetu kununua baada ya kuuza mazao yetu baada ya kuyathamanisha na kupata fedha za kigeni, siyo leo kila kukicha tunaenda kupiga magoti kwa wazungu kuomba misaada
Hiyo pamba mtambo wa kuifanya nyuzi mpaka iwe kitambaa unaifanya wewe? na hayo yote mengine?
Fikiri japo kidogo, huna uwezo wa kutengeneza viwanda vyako mwenyewe, ukipenda usipende, hizo korosho dawa za kuulia wadudu unatengeneza wewe? gari za kubebea hayo mazao yako unaunda wewe? vipuli unaunda wewe?
Huna huna huna. Halafu leo hutaki Rais afanye mahusiano na nchi wenye-navyo vyote hivyo, japo akabembeleze uuziwe na ufundishwe kuvitumia tu mpaka hapo akili yako itakapofunguka (baada ya miaka elfu moja kuanzia leo) ili ujitengezee mwenyewe. Bila wao hayo mazao yako utayafanyia nini? kalime na jembe la mkono uone raha yake. Kama litakutosha hata vya kula wewe mwenyewe tu licha vya kubakia uviuze nje.
Unaongelea mika ya 80? unaijuwa dhiki tuliokuwa nayo miaka ya 80? au unajiandika upuuzi tu, miaka ya 80 hata sukari ilikuwa lazima tukae foleni na tunapata kilo moja kwa kaya moja kwa wiki moja. Unalijuwa hilo?
Magari yalikuwa jumapili hakuna kutembea, foleni ya mafuta ya gari, watu hawana hata nguo za kuvaa, viraka mpaka makalioni. Unaijuwa wewe miaka ya 80? tafadhali usitukumbushe huko tuliokuwepo, ilikuwa ni dhiki ambayo ushukuru mungu hukuwepo kuiona.
Hivi huwa mnafikiri kutumia nini?
Usitukane wakunga na uzazi ungalipo.
Ulikuwa unanunuwa kwa fedha ya nani? wewe kweli hamnazo. Kiwanda cha almasi toka lini kilikuwa mali ya Serikali ya Tanzania, nna uhakika hilo swali ni gumu sana kwako.
Kununuwa? unajuwa kisa cha Tiny Rowlands wa Lonrho na Nyerere? kama hujui uliza tukueleze. Nna uhakika hukuwepo unasikia porojo tu za mitaani.
Jiulize hovyo viwanda vyako vyote, na pamoja na vilivyotaifishwa kwanini vilishindwa na vikafa?
Jiulize, kwanini Tanganyika ilikuwa nchi ya kwanza katika Afrika kusafirisha mazao ya shmabni nje lakini miaka 7 tu baada ya Uhuru ikaanza kuwa omba omba wa chakula?
Jiulize kwanini Tanganyika ilikuwa ya kwanza duniani kwa zao la mkonge lakini miaka 7 tu baada ya uhuru likaanza kufa na kuwa si zao tena na mashamba ya mkonge yakabaki mapori?
Nna uhakika hayo maswali kwako ni kitendawili usichoweza kuwa na ufumbuzzi nacho.
Viwanda vyote vimekufa sababu ya ufisadi wa viongozi wa serikali kujali matumbo yao badala ya kuangalia maslahi ya wananchi.......
Hakuna masharti ya kuwakubali mashoga na kuwatambua kabla hatujapata misaada? Tafadhali mwenye kujua anijuze.
Mashoga wamejaa Tanzania, wewe huwajui mashoga wa Tanzania? pitia hapa ujionee:
HUU NDIO MTANDAO MZIMA WA KUJIUZA MASHOGA TANZANIA, KWA KILA MKOA. ~ the HOOD InfoTainment
Tanzania Gay Access | - For the love of Gay Men in Tanzania!
Young Tanzanians Gays: mambo hadharani.......
https://www.google.co.tz/search?q=T...hannel=sb&gws_rd=cr&ei=efU6U5j-I7Pn7AbZnoHwDQ
Hoja yako dhaifu, Membe alishasema hatutawatambua rasmi mashoga na ushoga, watabaki kuwa ni dhambi Tanzania. Hulijui na hilo?