Taarifa za mikopo midogo midogo ya kibiashara!

da mikopo hapa bongo ina masharti magumu kishenzi aisee

Ni kweli mkuu,

Nilikuwa naongea na jamaa mmoja kutoka Denmark, alikopa nyumba ambayo wanalipa kwa miaka 30 na malipo yao kwa mwezi ni kama Euro 2000. Riba ya jumla ambayo wanatakiwa kulipa ni kati ya 4-8%

Kwa hapa Bongo, mikopo ya muda mrefu inakuwa na riba ya zaidi ya 30!

Ndiyo maana wakubwa zetu hawajui kwa nini bado tuko maskini!!

Babu DC!!
 
kuna mtu yeyote mwenye mkataba wa mkopo kati ya bank ya posta na mwombaji mkopo (ambaye ni mfanyakazi))?

Naona hii bank tumeisahau kabisa. Zamani ilikuwa inasaidia sana kwani walikuwa wanaruhusu kuchukua pesa tawi lolote nchini. Ilisaidia sana wanafunzi!

Ngoja tusubiri kama kuna mdau anaitumia au anamjua mtu anayetumia hii bank au ana mkopo kutoka bank ya posta basi atatujuza.

Babu DC
 
Ni kweli mkuu,

Nilikuwa naongea na jamaa mmoja kutoka Denmark, alikopa nyumba ambayo wanalipa kwa miaka 30 na malipo yao kwa mwezi ni kama Euro 2000. Riba ya jumla ambayo wanatakiwa kulipa ni kati ya 4-8%

Kwa hapa Bongo, mikopo ya muda mrefu inakuwa na riba ya zaidi ya 30!

Ndiyo maana wakubwa zetu hawajui kwa nini bado tuko maskini!!

Babu DC!!

hata hapa bongo ukikopa dolla $ riba yake ni ndogo sana knye less than 3% kwa mwaka. tatizo fedha za madafu hazina dhamani ndio maana mnapigwa riba ya juu
 
Nilitembelea nchini Marekani karibuni nchi ambayo miaka michache nilikuwa nakula vitabu vyao. Kwa udadisi tu niliamua kwenda bank kuulizia wanafanyeje ukopeshaji wa pesa. Niliambiwa mkopo wa secured money ni free under one year period. Zaidi ya mwaka wanaanza charge kidogo za riba lakini haizidi 3%. Lakini bank za bongo ni mtindo mmoja tu kana kwamba unawekeza rehani ya nyumba.

NIliporudi kuwaeleza maofisa wa bank fulani (jina kapuni) waliniambia wao wakati mwingine wakakopa pesa huko majuu ndio maana riba huwa juu sana ili kufidia kotekote. Hoja hii haijaniingia vizuri katika mikopo ya mabeni kwa mabenki kimabara.

Just curious, ni benki gani hiyo ya Marekani iliyokuambia secured money wanatoa free under one year period?
 
Naona hii bank tumeisahau kabisa. Zamani ilikuwa inasaidia sana kwani walikuwa wanaruhusu kuchukua pesa tawi lolote nchini. Ilisaidia sana wanafunzi!

Ngoja tusubiri kama kuna mdau anaitumia au anamjua mtu anayetumia hii bank au ana mkopo kutoka bank ya posta basi atatujuza.

Babu DC

Bank ya posta kwa wafanyakazi wa tz ndo mkombozi kwani riba yao ni 19.2% Pa.
 
Nakubalina na wewe...Ni vigumu kupata bank ambayo inatoza interest ya 3% kwa USD!

Wasiwasi wangu ni kwamba kuna watu wanapenda kuweka post humu JF kufurahisha kijiwe ila hawajui ukweli wake. Mmoja wetu kwenye hii topic amepost information kuwa alienda benki moja Marekani kuulizia wakamwambia akikopa hela na arudishe ndani ya mwaka hatalipa riba. Nimeuliza ni benki gani naona bado hajatuambia. Sasa hiyo inawezekana vipi? Nafikiri atakuwa aliongea na mtu akamwambia kuna kitu kama hicho ila hakuelewa vizuri maana yake ni nini. Nasubiri atupe jina la benki ili nieleze ninachofikiri alielewa vibaya.

Hiyo riba ya 3% per year ukikopa hela kwa dola haileti mantiki. Tunasubiri jina la benki tuthibitishe. Wewe fikiria ukiweka hela kwenye account ya dolla say NBC, wakati unatoa ukizitaka kwenye dola inabidi ulipe fee! Sasa hela zako na unalipa fee. Ukikopa hela wakupe mkopo halafu ulipe only 3%.

Nawasilisha.
 
Equity tumeanza jamani, njoo uone tofauti, Equity ndoo hii hapa, mikopo yetu ni ya masharti nafuu sana, mikopo kuanzia midogo mpaka mikubwa, hatuna ubaguzi, njoo tukusikilize, njoo tukujali, karibu nyumbani kwako Equity Bank.
kwa sasa tuko quality centre hapa kwa manji, posta jengo jipya nyuma ya PPf Tower na arusha.
mwezi ujao tunapplan for kariakoo na mwanza coming soon.
 
Mkuu embu tupe dondoo Equity mokopo yake ikoje kwa si wajasiriamali? Naweza kopa kuanzia ngapi hadi ngapi? Riba ikoje? Na kwa muda gani?
 
siku hizi mabenk yanapandisaha riba kimya kimya, nilikopa stanbic bank kwa riba ya 22% personal loan nashangaa miezi miwili iliyopita makato yameongezeka kuuliza wananiambia riba imepanda hadi 28% hii siyo fare hata kidogo.

wamenivunja moyo sana natamani kuwakimbia na mkopo wao
 
Back
Top Bottom