Taarifa za mikopo midogo midogo ya kibiashara!

Narubongo

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
2,567
2,000
mkuu, nilisikia muda kidogo kwamba wangeingia bongo, branch zao zipo wapi?

nimeweza ku confirm location zao, Equity bank kwa dar wapo quality centre (pugu road) na nyingine posta wapo PSPF plaza karibu na ppf. Ni bank nzuri sana kwa mikopo ya wafanyabiashara wadogo na wakulima, niliongea muda mrefu sana na wafanyakazi wao na kweli niliwakubali.
Target yao ni watu wa kipato cha chini hata kama una biashara ya maandazi watakuthamini
 
Dark City

JF-Expert Member
Oct 18, 2008
16,269

Ahsante sana kaka,

Interest yao ni asilimia ngapi na wana masharti gani? Kwa mfano wanahitaji nini kama security??

DC
 
Manyovu

Member
May 20, 2011
78
125
Asanteni kwa michango mizuri na ushauri wa wapi pa kupata mikopo ya biashara. Naamini itasaidia kwa wale ambao tunafikiria kuongeza mitaji kwenye biashara tulizokwisha kuanzisha na zile tunazofikiria kuanzisha.

Ushauri wangu tu ni kuwa ikiwezekana mtu afanye biashara zaidi ya moja kwani kuna kupanda na kushuka na ukiwa na biashara zaidi ya moja anagalau zitasaidiana.

Swali dogo tu lililoko nje ya mada, hivi tuna benki au taasisi zinazotowa mikopo ya kujenga nyumba Tanzania kwa kiwango cha mil 100 mpaka mil 150
 
Ahsante sana ndugu kwa maoni na ushauri wako. Naamini wadau wataufanyia kazi!!

Kuhusu mikopo ya nyumba...ni kweli kuna benki zinatoa ila sina details. Nitajaribu kulifanyia kazi.

DC
 
Dark City

JF-Expert Member
Oct 18, 2008
16,269
2,000
nimeweza ku confirm location zao, Equity bank kwa dar wapo quality centre (pugu road) na nyingine posta wapo PSPF plaza karibu na ppf. Ni bank nzuri sana kwa mikopo ya wafanyabiashara wadogo na wakulima, niliongea muda mrefu sana na wafanyakazi wao na kweli niliwakubali.
Target yao ni watu wa kipato cha chini hata kama una biashara ya maandazi watakuthamini

Nimefuatilia na kuambiwa kwamba bado wanakamilisha taratibu za kibenk kabla hawajaanza kazi rasmi. Watakuwa kwenye business baada ya miezi 3-4.

Babu DC
 
KANCHI

JF-Expert Member
Sep 3, 2011
1,535
1,225
Wana jf hata me nilikuwa nahitaji mkopo wa nyumba wandugu benki zipi zinatoa mikopo yenye riba nafuu?
Mia.
 
LiverpoolFC

JF-Expert Member
Apr 12, 2011
11,041
2,000
Dark City!

Hakika upo makini ktk ukombozi wa Mtanzania yeyote yule mwenye kutaka kujikwamua katika hatua moja kwenda kwingine!

Mi nafikiri ni wakati mwingine tena wa MwanaJF yeyote aliye kama Mi binafsi kutafakari kwa makini THREAD hii na kurudi upya kwa namna ajuavyo kwa Dark City!

Hongera sana na hakika uko MAKINI!

Pamoja Daima DC!
 
NINAHASIRA

Member
Nov 5, 2010
58
0
kaka mimi nilichikua kamkopo kangu AccessBank hakika hawana masharti mengi na wanatoa mikopo kuanzia laki 1, na kwa muda mfupu kabisa! mi nadhani ni wakati wa kwenda kuwatembelea hawa jamaa wako vizuri kwa wajasiriamali tofauti na mabenki ambayo umeyataja hapo juu,. Kwa sasa NMB si ya makabwela tena ndo mana wanaitwa NMB PLc kwa sasa.
 
Mama Joe

JF-Expert Member
Mar 30, 2009
1,504
1,225
Asante sana kwa kutuletea hii topic, binafsi nimeelimika sana. Nina swali, iwapo mimi mfanyakazi nimechukua mkopo bank na nimepangiwa au kuchagua kulipa laki saba kwa mwezi. sasa ktk kuutumia mkopo wangu kwenye biashara nimeacha kazi na kusimamia biashara. Je inawezekana bank ikakubali kupunguza kiwango cha kurudisha kwa mwezi ili nimudu kulipa bila kuathiri biashara yangu? Mkopo ni wa kujengea nyumba.
 
Ahsante sana kamanda,

Unajua hapa JF wapo baadhi ya watu wanahitaji taarifa kama hizi ila ni ndugu kuzipata. Tuendelee kusaidiana!!

...Sasa wewe, ... hujabaki peke yako huko LSC???

Babu DC!!
 
Dark City

JF-Expert Member
Oct 18, 2008
16,269
2,000
kaka mimi nilichikua kamkopo kangu AccessBank hakika hawana masharti mengi na wanatoa mikopo kuanzia laki 1, na kwa muda mfupu kabisa! mi nadhani ni wakati wa kwenda kuwatembelea hawa jamaa wako vizuri kwa wajasiriamali tofauti na mabenki ambayo umeyataja hapo juu,. Kwa sasa NMB si ya makabwela tena ndo mana wanaitwa NMB PLc kwa sasa.

Ahsante sana,

Nitawafuatilia ili taarifa zao niziweke hapa pia...Ila niliwahi kuongea nao na walionekana kana kwamba wanatoa mikopo ya chini ya 10m...Kwa mkopo ambao ni zaidi ya hapo, walionekana kupwaya!!
 
Dark City

JF-Expert Member
Oct 18, 2008
16,269
2,000
Asante sana kwa kutuletea hii topic, binafsi nimeelimika sana. Nina swali, iwapo mimi mfanyakazi nimechukua mkopo bank na nimepangiwa au kuchagua kulipa laki saba kwa mwezi. sasa ktk kuutumia mkopo wangu kwenye biashara nimeacha kazi na kusimamia biashara. Je inawezekana bank ikakubali kupunguza kiwango cha kurudisha kwa mwezi ili nimudu kulipa bila kuathiri biashara yangu? Mkopo ni wa kujengea nyumba.

Poa MamaJ,

Nakushauri ukaongee na ila nadhani itakuwa ngumu kupunguza marejesho ya mwezi. Hata hivyo huwa ni wepesi na hakuna tatizo kama unataka kuongeza marejesho ya mwezi...Mfano unataka kurejesha laki 8 badala ya 7, hawana tatizo kabisa...Nimewahi kufanya hivyo na sikuwaomba ruhusa!!

Babu DC!!
 
Mama Joe

JF-Expert Member
Mar 30, 2009
1,504
1,225
Ok DC nashukuru sana kwa hili, kifupi nilichukua muda na collateral ilikuwa ni mshahara, sasa juzi wamekuja kutambia habari ya top up, ila ningependa deni lao liishe mapema na niwe free kutoingia ktk ajira.
Tuliwauliza kuhusu hilo na wamejibu kuwa wanatuongezea hata muda wa marejesho usogezwe mbele ikiwa tunachukua top up. Kutokana na jibu lako nashukuru sana nadhani ni bora nisichukue kabisa na ni bora niendelee na Saccos ambayo nimeishaanza kuweka taratibu. Interest zao pia ni kubwa mno. Asante sana
 
Ni kweli NMB wanaruhusu top up baada ya kulipa kwa muda (nadhani miezi 10) ila bado interest zao ni za hatari.

Kuna jamaa yangu alichukua top up na kufuta deni la zamani. Alichukua 30mil ambazo atazilipa kwa miaka 4. Pamoja na interest, insurance charges na processing fees, jamaa atalipa zaidi ya 42mil (>33% of interest). Hii ni pesa nyingi sana kwa mtu wa kawaida anayetaka kujikwamua.

Sikushauri uchukue kwao mkopo wa muda mrefu kwa NMB na banks nyingine zenye utaratibu kama huo.

Babu DC!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom