Taarifa ya tume ya Corona imetoa mapendekezo zaidi kuliko hali halisi ya ugonjwa kwa sasa nchini

Siku hizi ukiwa na smart phone na bando kisha ukawa na access yakuingia kwenye mitandao ya kijamii basi unakua mtaalamu wa kila kitu!

Unakua unajua kazi za kila mtu zinapaswa kufanywaje na kwa usahihi gani kuliko hata kujua kazi zako wewe mwenyewe zinavyopaswa kufanywa na kwa usahihi gani!
 
WEWE UNASEMAJE?SOCIAL ISSUES

Katika mjadala unaoendelea wa kamati iliyoundwa kwa ajili ya kushughulikia suala la Corona wadau wengi wanadai kamati imeonesha udhaifu mkubwa sana. Ripoti yao imeacha mambo muhimu sana na yanayogusa ishu nzima ya korona nchini.

Kamati iliyoundwa ilijumuisha wasomi wakubwa na wanaoaminika lakini bado kazi yake haikuwa ya kuridhisha. Yaani hata ule tu utaratibu wa jinsi utafiti unavyofanyika haukufuatwa.

Baadhi ya mambo ambayo hayakujibiwa na ripoti na yanagusa hisia za wengi na yanayofanya ripoti ionekane haijakamilika ni kama haya hapa chini. Mambo haya kamati haikuyazingatia japo ni mambo nyeti kwa nchi yetu.

Kamati ilipaswa kueleza hali ya corona nchini kwa siku hizo zilizopita ilikuwaje

Kamati ingeeleza hali ya corona kwa sasa nchini iko vipi

Pia ingeeleza athari au madhara ya kiafya ambayo tumeyapata hadi sasa kwa kushindwa kufuata njia za kisayansi kwa muda mrefu.Tumepata madhara au vifo kiasi gani. Hii ingesaidia kujua tupo katika hatari kiasi gani.

Kamati ingetueleza njia zilizotumika kufanya utafiti. Kama wamekutana na wagonjwa wa corona au waliokwisha ugua wakapona. Au madaktari wanaouguza wagonjwa wa corona n.k.
Kwa kuwa watu walikuwa wakitumia nyungu basi ilitegemewa wao waje na sababu zao za kwa nini watu wasitumie nyungu bali wapate chanjo. Wangeeleza madhara ya kutumia nyungu na wangesema kama watu waachane nazo maana hazisaidii. Hakuna sababu waliyoieleza ya kwa nini tupatiwe chanjo na siyo kuendelea na nyungu. Huo ni udhaifu wa ripoti
Katika utafiti wao wangeanza na njia ambazo jamii tayari ilishaanza kuzitumia waoneshe mapungufu yake ili kuwashawishi watu watumie njia mpya sasahivi.

Wangetueleza jinsi walivyozifanyia utafiti chanjo hizo wanazozipendekeza za corona na zina usalama kiasi gani. Wanasema tutumie chanjo hizo je wamefanya utafiti gani kuhusu hizo chanjo hadi kututhibitishia usalama wake ilihali nchi zingine zinasitisha na kusitasita kuzitumia kutokana na athari hasi.

Halafu wangebainisha wazi ni chanjo gani tuitumie kama nchi ambayo ni salama zaidi badala ya kupokea maelekezo kutoka WHO ambayo kwa sasa haiaminiki tena maana inanunulika na kutumika kufanikisha ajenda za kishetani. Inamaana kamati hajifanya utafiti wowote lakini wanataka watanzania watumie chanjo hizo?

Wangeeleza athari zitokanazo na kutumia chanjo hizo ili watu wajue na wafanye uamuzi. Siyo kweli kuwa hazina athari kabisa. Siyo tu kuwaambia watu watumie pasipo kueleza athari zitakazoletwa na chanjo hizo .Suala hapa siyo kupinga uagizaji wa chanjo ila ni namna chanjo hii ilivyoharakishwa upatikanaji wake bila kupata muda wa kutosha kuitafiti Kama ina madhara kwa afya. Huo ni udhaifu mkubwa wa kamati hiyo. Kama kamati haikupendekeza aina ya chanjo ya kuitumia hapo inamaana tusubiri kuchaguliwa na wanasiasa, WHO au tuige kutoka mataifa mengine.

Na kama kweli chanjo hizo zinafanya kazi kwa nini wazungu wanawazuia waafrika kwenda ulaya na marekani? Kwani wao si wamechanjwa? Why waogope? Maana nasikia watu wote hata wototo wanachanjwa huko kwao. Kamati iende ikakae tena au iundwe nyingine, ni maoni. Wasomi wametuangusha sisi WANYONGE Afya ni kitu nyeti sana kuliko misaada ya kifedha toka kwa wazungu

Baadhi ya wabunge wametahadharisha madhara ya kukurupuka linapokuja suala la chanjo. Chanjo si kama dawa zingine za kutibu maradhi. Chanjo ni viumbe hai (virusi vya corona) wanaopandikizwa ndani yako lakini wakiwa wamepunguzwa makali ili wauchochee mwili kujijengea kinga yake. Mwili ukijenga uwezo huo na kupigana na viumbe hao na kuvishinda basi unakuwa umejijengea kinga ya kudumu dhidi ya viumbe wa aina hiyo mbeleni.Mwili hutunza kumbukumbu, endapo utashambuliwa tena siku zijazo utaachilia kinga iliyotumika kupambana na adui wa kwanza na akashindwa endapo wanafanana na wasasa.

Sasa endapo kama chanjo iliyotengenezwa ikawa na athari mbaya kwenye mfumo wa genatics itaathiri vizazi vyote baada ya hapo. Wanaweza kuanza kuzaliwa binadamu wa ajabu ajabu. Siyo kitu cha kuharakisha,au dharula kutokana na unyeti wake. Kinahitaji muda wa kutosha kufanya utafiti.

Nilikuwa najaribu tu kuwaza kwa sauti. Shea ili iwafikie wahusika tupone.
__________________

Shea na marafiki katika magroup mbalimbali.
Unaweza kukuta huyu kibwengo hajui chochote kuhusu sayansi, afya wala misingi ya tafiti lakini ndio mshauri.

Hivi sijui kwanini wabongo tuko hivi. Kitu hata kama hukijui utalazimisha kukijibu na kukiongelea hivyo hivyo yaani.
 
Unaweza kukuta huyu kibwengo hajui chochote kuhusu sayansi, afya wala misingi ya tafiti lakini ndio mshauri.

Hivi sijui kwanini wabongo tuko hivi. Kitu hata kama hukijui utalazimisha kukijibu na kukiongelea hivyo hivyo yaani.
Hatari sana,na hawa ndio wanao ipotosha jamii,hiyo kamati hata kama ingekuja na majibu ya aina gani watu kama hao hua hawakosekani,hapo ukute yupo chini ya mti wa muembe anatafuna muhogo mbichi huku akikosoa wasomi na ki tecno chake.
 
1. Kamati ingeelezaje wakati hamkuwa mnatoa data
2. Hali ya sasa hivi itaijuaje wakati bado hampimi kutoa data...
Kuna watu humu wanasema huko hospitali madaktari wanajua uhalisia wa corona na kuna watu wanasema ndugu waliugua corona na wengine wamefariki, sasa basi kamati ingeanzia huko hata kama hakuna takwimu ila wangejua nini kinaendelea huko mahospitalini.
 
Back
Top Bottom