Taarifa ya serikali bungeni kuhusu vurugu za Mtwara

Taarifa ya serikali bungeni kuhusu vurugu za Mtwara

Hivi tujiulize, kwanini Mh Pinda kaingia mitini kutoa taarifa ya serikali bungeni kamuachia waziri ambaye watumishi wake wanafanya biashara ya bangi????



Kama utakumbuka vizuri,baada ya vurugu za awali Mh. Pinda alitoa tamko la serikali kuwa mchakato umesitishwa na serikali imeamua mapendekezo ya wana mtwara yafanyiwe kazi..... Unadahani atasema nini leo!!!!
 
Na Lydia Churi.
SERIKALI YAAPA KUWASAKA WAASISI WA VURUGU MTWARA
Serikali imelaani vikali vurugu zilizotokea Mtwara na imeapa kuwasaka waasisi wa vurugu hizo ndani na nje ya Mtwara.
Akitoa kauli ya Serikali Bungeni kuhusu vurugu zilizotokea Mtwara jana, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Emmanuel Nchimbi ameliambia Bunge kuwa wote waliohusika kupanga, kushawishi, kuandaa na kutekeleza vurugu hizo hawataukwepa mkono wa sheria.


Katika kauli hiyo ya Serikali Waziri Nchimbi amesisitiza kuwa watanzania wanalo Taifa moja ambalo maliasili zake ni za watanzania wote hivyo tabia iliyoanza kujengeka ya kila eneo kutaka inufaike peke yake na mali za eneo husika italigawa taifa vipande vipande.
Alisema baadhi ya taasisi za kiraia na vyama vya siasa kwa maslahi binafsi yasiyo na upeo mpana, vinaweza kudhani kuwa kuunga mkono madai ya namna hii ni kujiimarisha na kukubalika kwao kwa jamii lakini badala yake wataipasua nchi na kusababisha vifo vya maelfu ya watu pamoja na kulijaza taifa vilema na majeruhi.
"Wasaliti wa taifa hili wanafahamu maendeleo makubwa yatakayopatikana Mtwara na nchi nzima kutokana na rasilimali gesi, hivyo wanatumia vibaya ufahamu wetu mdogo kuhusu gesi na kuchochea upinzani dhidi ya mradi huu unaotarajiwa kuwakomboa watanzania" Alisema Waziri.
Alisema vita inayofahamika kama vita kuu ya Afrika katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo iliyopiganwa kati ya 1998-2003 msingi wake ulikuwa ni kupigia rasilimali, vita hii ilisababisha vifo vya watu milioni 5.4, magonjwa na njaa na kuhoji kuwa huko ndiko tunakotaka kulipeleka taifa letu.
Alisisitiza watanzania wanatakiwa kujua kuwa wanayo dhamana ya kuendeleza umoja amani na kuchangia maendeleo ya nchi na tofauti zinazojitokeza lazima ziendelee kuzungumzwa kwa uwazi, kuheshimiana na kuzingatia sheria na taratibu za nchi yetu.
Alisema raia mmoja, Karim Shaibu alifariki katika vurugu hizo na wakati huohuo askari wanne wa Jeshi la wananchi wa Tanzania walifariki baada gari lao waliokuwa wakisafiria kutoka Nachingwea kwenda Mtwara kupata ajali katika eneo la Kilimani Hewa. Askari wengine 20 walijeruhiwa katika ajali hiyo.
Waziri Nchimbi aliyataja madhara mengine yaliyotokana na vurugu hizo kuwa ni kuchomwa moto kwa Ofisi za Mahakama ya Mwanzo ya Mitengo, Ofisi ya CCM kata ya Chikongola, nyumba binafsi ya Mwandishi wa Habari wa TBC na ya Afisa Mtendaji kata ya Magomeni. Aidha katika vurugu hizo, nyumba za askari polisi wanne pamoja ofisi ya kata ya Chilongola zilivunjwa na kuibiwa vitu mbalimbali.
Jana majira ya saa 4 asubuhi kulitokea vurugu kubwa katika Manispaa ya Mtwara na viunga vyake zilizosababishwa na madai ya baadhi ya wananchi wa Mtwara kupinga usafirishwaji wa rasilimali gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es salaam. Makundi ya vijana waliokuwa maeneo ya Sokoni, Magomeni na Mkanaredi walipanga mawe makubwa, magogo na kuchoma moto matairi barabarani hali iliyoendelea kusambaa maeneo mengine.
RATE THIS ITEM 1 2 3 4 5 (1 Vote)
 
Inasomwa na Nchimbi badala ya PM,

Nawapongeza askari waliofanya kazi katika mazingira magumu kurudisha hali ya amani

ANAENDELEA

Wana JF naomba kufahamu maana ya Amani kwa tafsiri ya SERIKALI YETU. Nashindwa kuelewa kabisa, je huwa wanaimanisha utulivu, ukimya, kuzuia kuonyesha hisia au nini?
 
Serikali legelege na :A S-fire1:majibu legelege. Sasa wanatafuta Mchawi kwa kusema kuna vyama vya siasa na hasasa za kiraia vinahusika. Sasa kwa nini asivitaje na aeleze vinahusika vipi. Kama ni hatua zichukuliwe. Huko mtwara si ngome yao hao magambas. Kama anataka kuota joto ya jiwe kama waziri wa mambo ya ndani aende huko Mtwara aone cha mtema kuni. Kama hajui akmuulize James Mbatia.
 
Wana JF naomba kufahamu maana ya Amani kwa tafsiri ya SERIKALI YETU. Nashindwa kuelewa kabisa, je huwa wanaimanisha utulivu, ukimya, kuzuia kuonyesha hisia au nini?

Kwa tafsri ya amani kwao ni utulivu, kutohoji na kunyenyekea maamuzi ya watawara. Mfano ukihoji kwa nini north mara imebaki magofu, Kwa nini muaji kamuanda yuko huru, mnachukua hatua zipi kwa walioficha pesa zetu Usswiss, iweje twiga wetu wasafirishwe mchana kweupe kwenda uarabuni....imekuaje watoto wa wakubwa wawe milionaire ghafula.....tiss iko wapi kuchunguza na ku-ditect mapema udini, ugaidi.....watakuita mchochezi na mwalibifu wa 'amani'.

Amani kwao ni mwanvuli wa kuedeleza utawara wa kujuana, kujirimbikizia mali.....

Mfano Nchimbi anasema taifa aliwezi kugawanywa kwa raslimari. Hajiulizi iweje Mtwara/kigoma wameendelea kuwa mikoa maskini...hajiulizi iweje dar-kigamboni ktk miaka ya hivi karbuni iwe centre ya kila kitu....hajiulizi iweje wapo wanaolala njaa huku yeye chakula anamwaga....hajiulizi kwa nini elimu ni mbovu huku watoto wao wakipata elimu nzuri.....ayo kwake ndo amani, ndo kuifanya tanzania iwe moja.

Ninacho kiona hapa ni kutiwa upofu wa macho na ganzi kiakiri ili mambo yaalibike na baadae tuanze kujiuliza nani amefanya haya.
 
Huna tofauti na viongozi wako walio panic, nakutoa majibu ya mkato mkato wewe na lazima u come from one of the elite families that think hii nchi ni ya KWAO PEKE YAO
yes!!!! i am coming from one of the country's most ELITE FAMILY. my grand father was one of the people of this country who contributed everything he had to the LATE MWALIMU NYERERE to help him on the struggle for independence.
my parents were low ranked civil servants who turned to be poor farmers after retirement, and my self i am just one of the hustlers of this nation who earns his daily bread through sweat and wounds, scars and blood, hunger and thirst.
BUT I AM GIFTED with very strong mind that can not be easily brainwashed through religious fanaticism,tribal conflicts and political parties views. for me , my country comes first and the rest can follow. I don't care about anyone who thinks that being opposite to CDM means coming from the family that benefits from the ruling system.
as far as i understand,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, this country can not be given to dogs and jackals
 
Nashangaa wazee wa matukio hawajafika wakati ndio wanakuwaga wa kwanza kufika wamebaki kusemea pembeni. bila shaka wanajua chanzo.
 
Back
Top Bottom