Taarifa ya Post motum mauaji ya North Mara-Tarime

Ogwari

Member
Apr 14, 2011
26
15
UfuATAO NI TAARIFA HALISI TULIYOTOKA NAYO BAADA YA UCHUNGUZI WA WETU,
KWA KULINDA NA KUHESHIMU UADILIFU WA TAALUMA YETU YA KIAFYA.
KIAPO NILICHOAPA HUKO CHUONI (MEDICAL ETHICS)

1. Kile kinachoonekana katika vipimo/uchunguzi, ndicho kinachotakiwa
kuwekwa wazi kwa muhusika.

2. Sitakeuka wala kughiribu utu wa mtu kwa sababu zozote zile.

Hizo ni chache tu kati ya Medical Ethics nyingi, ambazo niliapa
kuzilinda na kuzisimamia.


POST MOTUM ROOM
Tulianza kazi hii saa 10:25 A.M hadi saa 16:57 P.M baada ya wafiwa
kuitambua miili ya ndugu zao.


1. Mwili wa Emmanueli Magige
P.M No 1-5-11
T.G.H
Entrance site: Left illiac cleft (upande wa kushoto wa juu ya nyonga)
Wound size: 0.5 cm diameter the wound was round.
Exit site: Lumber region back (juu ya kiuno kidogo karibu na uti wa
mgongo)
Wound size: 2.5 cm diameter

Positive findings;-
-Blood vessels/Nerves and sorounding muscles were destroyed.
-The clavicle bone was destroyed and blood clots was seen, ( mfupa
mkuu wa kiuno na nyonga uliharibiwa na damu nyingi ilivuja na
imeonekana imeganda humo)

But beneath the exit site, there was a cut wound, 2.5 cm diameter.
Lakini kulikuwa na alama ya jeraha kubwa linaloonyesha alama ya kuwa
kitu chenye ncha kali kilichoma, na hii ilileta hisia tofauti, polisi
walihisi kuwa aliangukia jiwe au kijiti kilichomchoma, kwa hili
tulibishana na tukaamua hakuna jibu la nini kilichoma, ila mimi
nilihisi na kusimamia kuwa alichomwa na singe ya bunduki, na ndipo
niliomba nguo zake zitafutwe ili tuzichunguze na tubaini ukweli, hata
hivyo hazikupatikana.


2. Mwili wa Chacha Ngoka
P.M No. 2-5-11

T.G.H

Entrance site: Right side of the body back 16 cm from illiac (usawa wa
bega chini na juu ya kiuno, nyuma ya mwili.
Wound size: 0.3 cm diameter
Exit site: In 5th intercoastal muscle right side, 2cm from the nipple.
Wound size: 5cm diameter

Positive findings
Major blood vessels were destroyed
Midle and right lobe of liver were destroyed led to rasaration
In the Trachea, blood clot was seen.


3. Mwili wa Chawali Boke.
P.M No. 3-5-11.
T.G. H
Entrance site: Occipital bone 8cm from the Pinna, (Kisogoni sm 8
kutoka sikio la kushoto)
Wound size: 0.2 cm diameter
Exit site: In parietal bone ( kwenye paji la uso pembeni kidogo)
Wound size: 5cm diameter
Positive findings;-
The brain and inner part of the head was destucted, blood clotts was
seen, this was due to blood aspiration.


4. Mwili wa Mwikwabe Marwa Mwita
P.M No. 4-5-11
T.G.H
Entrance site: Left illiac cleft (upande wa kushoto juu ya nyonga)
Wound size: 3.5 cm diameter
Exit site: It was not pass through, it remained intact.
Wound size: None

Positive findings;-
There was worse destruction of;-
-Femoral artery
-Femoral vein
-Sorrounding muscles
- Fructure of illiac bone ( mfupa wa nyonga na uzazi)
- Piece of lead was seen lying deeply inpsoas muscle, sorrounded by
bone fragments

Msimamo wangu kimaadili na na kibinadamu;-
1. Polisi walikusudia kuua na sio kudhibiti watu waliowaita wavamizi,
kwani kwa mjibu wa force law, hawakutakiwa kupiga risasi sehemu yoyote
tofauti na miguuni.
2. Polisi waliwapiga risasi watu waliokuwa wakikimbia kutoka eneo
hilo, kwani risasi zote zimepenya kwa upande wa nyuma wa mwili na
zikatokea upande wa mbele wa mwili.
HIVYO wananchi hawa hawakupambana na polisi, bali walipigwa risasi
wakiwa wanakimbia, ndio sababu ya risasi zote kuingia sehemu za nyuma
za miili yao.
Mungu watazame waja wako na uwalinde na yote aliyoyaandaa SHETANI.
 
Shukrani kwa taarifa! ila inaonekana vyombo vya usalama vipo kulinda maslahi ya wawekezaji na si usalama wa raia! Hii ndiyo Tanzania yetu!! Mungu Ibariki Tanzania na Watu Wake
 
hii imewekwa humu na Dr. G. Nyakirungu aliyeshiriki kufanya hiyo post moterm, sasa nafikiri umeamua kwa makusudi kuwachosha mods kuziunganisha hizi nyuzi
 
Back
Top Bottom