Taarifa ya Nchimbi kwa wanahabari

Mimi kilichonishangaza zaidi ni ile aya ya mwisho kwamba kamati itatoa ushauri na kutafuta jinsi ya ushirikiano wa wanahabari, polisi na vyama vya siasa.

Inamaana ile kamati haikwenda kuchunguza kifo cha mwandishi wa habari?
 
Usichanganyikiwe mkuu hii ndo tanzania yetu inayoongozwa kwa nguvu za :A S-devil4: na sio uerevu na busara.

Yaani acha inaniuma sana ebu imagine Mwangosi ni mdogo wako, hawa jamaa wanataka tuanze kulipa mapigo! Nimekasirika sana
 
Mkakati dhalimu! haki zetu zimewekwa rehani kwa manufaa ya watu wachache. Kwa nini RPC nae hajaunganishwa na huyo mtu wao wa bandia kwenye mashitaka hayo?
 
Huyo mwendesha mashtaka ana mapepo? Daudi Mwangosi amekufa mikononi mwa askari-zaidi ya mmoja. Kabla ya kulipuliwa na bomu alipigwa vibaya na hao askari. Sasa kwa nini ni askari mmoja tu amechukuliwa hatua? Vipi wale walioshiriki kumpiga (bodily harm)? Na RPC yuko wapi maana ndiye aliyeruhusu haya yote yatendeke, tena mbele ya macho yake? Where is he? Pia ningetaka kujua huyo askari ni wa kituo gani? anatoka mkoa wa Iringa? kama jibu siyo alikuja hapo kwa amri ya nani na kwa nini?

Mambo mengine:

1. Barua ya waziri inakiri kuwa Daudi aliuliwa na bomu la machozi, sasa, ni lini msemaji wa jeshi la polisi atatoa apology kwa kusema kuwa marehemu aliuliwa na kitu kizito? when?

2. Vifaa vya kazi vya marehemu (camera na laptop) viko wapi? Kwanini haviongelewi hivi vitu?

3. Ni lini serikali itaenda kumuona mjane na kumpa formal apology maana sasa waziri anakiri kuwa Daudi aliuliwa na bomu la machozi la polisi?
 
Muuwaji wa Mwangosi tuu? Vipi kuhusu Police killers wengine lini watafikishwa mahakamani? Vipi kuhusu uwajibikaji, Mwema, Chigonja wanasubiri nini?
 
Kama utendaji wa wasaidizi wa JK ndio kama wa huyu Nchimbi, rais wetu ana taabu ndiyo maana anashindwa hata kucomment ataanzia wapi? Tatizo ni kwamba hata akisema awabadilishe atawapata wapi? Wabunge wa CCM ndiyo hao wanaoupata ubunge kwa njia chafu. Kitu kichafu ni kichafu tu matokeo yake ndiyo nchi inayumba kiasi hiki.
 
This is too low! Waziri hana busara hata ya kujua la kufanya na la kuwaahidi wananchi. Huyu Waziri kama hajaona ile video nadhani wana habari wamwite wamwonyeshe. Mbwembwe za RPC pamoja na askari walioanza kumpiga mwandishi wa Nipashe hadi marehemu Mwamgosi akaingilia kati ndiyo waliosababisha kifo cha Mwangosi (RIP). Japo kama mtu hujasome sheria lakini hapa unaweza kuona wazi kipo kipengele cha wazi cha kuwafikisha wale Askari wote waliokuwa kwenye tukio pamoja na RPC mahakamani.
Ukitaka kujua jinsi walivyozoea kuwahadaa wananchi, hapo faili litakaa kwa DPP kwa muda mrefu, halafu atakuja na jibu kuwa mashtaka hayakuwa sahihi na askari aliyefikishwa mahakamani hawezi kushtakiwa kwa sababu za kiufundi. Na hiyo itatokea kwa sababu wanaogopa kumfikisha yule RPC wa Iringa mahakamani. Sababu za kuogopa kumfikisha mbele ya sheria zinaeleweka kuwa alikuwa ametumwa jambo kubwa zaidi ya lililotokea, asije akamwaga mchele..............
Mungu ibariki Tanzania yetu.
 
Safi Nchimbi waeleze hawa wasio na hiyana hawajui zuri hata kushukuru kwa hatua iliyofikiwa hongera sana kazi nzuri big upppppppppppp

endeleeni kutiana ujinga hivyo hivyo. but mind you 2015 is just around the corner... tumbafu sana. eti hatua iliyofikiwa, just too low...
 
ujinga mtupu, eti migongano ya kikazi kati ya polisi na vyama vya siasa, anaweza kutuambia ni lini ccm iligongana na police?

dr nchimbi nadhani umo humu, utakuwa umepata feedback nzuri tu itakayokusaidia kufanya self assessment...
 
short term solution inayosababishwa na mahesabu yasio sahihi ya kisiasa kuiponya CCM HESABU SAHIHI ILIKUWA NI KUWAWAJIBISHA MWEMA, NCHIMBI, PAULO CHAGONJA NA KUWASHITAKI WAUAJI WOTE RPC WA IRINGA PAMOJA NA ASKARI WOTE WALIOSHIRIKI ILI KILA MMOJA AKAJINASUE KIHERIA KINYUME CHA HAPO NI UJINGA WA WATAWALA KUDHANI HIKI WANACHOKIFANYA KITAWASAIDIA
KUMSAIDIA NCHIMBI NA WENZAKE WALIOKOSEA NI KUKIADHIBU CHAMA, SIMPLE ! HATA HILO CCM HAWANA UWEZO WA KUELEWA?
 
Jiuzulu badala ya kujibaraguza huku na kule...Wewe, Mwema na Kamuhanda wote mnastahili mjiuzulu haraka sana.

 
Hawa wapuuzi kwa kweli; wanataka tuamini kuwa tatizo la mauaji ya Mwangosi lilihusu askari mmoja tu.
Mwnakijiji
Mbona jazba zimekuwa nyingi? Uchunguzi lazima uwe na mwanzo kama wameanza na mmoja si tatizo labda kwa ushauri mwanakijiji ulitaka waanze na wangapi? Ila tu kumbuka uchunguzi hautaishia kwa aliyeua utakapo kwenda mbali usije kesho ukaugeuka na kudai ni mbinu za serikali makini ya CCM kuua upinzani!

Chama
Gongo la mboto DSM
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom