Taarifa ya Ikulu ya JK kuhusu Bomu la Zanzibar Ijumaa jioni

jibu liko hapa; "

Rais amekemea na kuwataka watu kuwa wastaarabu, wavumilivu na kuheshimu imani na mitizamo ya watu wengine". Kumbe keshawajua wahusika!!?? Tuna safari ndefu sana.
Mkuu baada ya Kumaliza kusoma post yako hii na kuielewa nilijikuta nacheka ghafla ha ha ha ha ha ha ha ha :smile-big:
 
Soma taarifa hii ya IKULU ya Dar es salaam kuhusu Bomu la Zanzibar

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za pole Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein kufuatia kuuawa kwa mtu mmoja na wengine sita kujeruhiwa akiwemo mhubiri wa amani ajulikanaye kama Sheikh Ahmed Haidari Jabir wa Zanzibar, kutokana na kurushwa kwa Bomu katika shughuli ya kidini iliyokuwa ikifanyika katika eneo la Darajani tarehe 13 Juni,2014, mjini Unguja.

‘Hicho ni kitendo cha kulaaniwa kwa nguvu zote na watu wote wapenda amani Bara na Visiwani, ni kitendo cha woga na kisicho na ustaarabu na wala hakikubaliki katika dunia ya sasa’ Rais amesema na kuongeza kuwa; ‘Hiki ni kitendo kilichofanywa na watu waoga, wasio na ustaarabu wa aina yeyote ile’.

Rais amekemea na kuwataka watu kuwa wastaarabu, wavumilivu na kuheshimu imani na mitizamo ya watu wengine hata kama hawakubaliani nao.

Rais amesema amesikitishwa zaidi na watu hao wasio na ustaarabu ambao wamefanya kitendo hicho cha kihalifu kwenye shughuli ya kidini ambapo ndipo mahali panapostahili Amani, Uvumilivu na Unyenyekevu zaidi kwa kuwa ni wakati ambapo binadamu anapofanya mawasiliano na muumba wake.

Rais Kikwete amelitaka Jeshi la Polisi kuwasaka na kuwafikisha mbele ya vyombo vya haki wale wote waliohusika katika tukio hilo lisilo la kistaarabu.

Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu-Dodoma
15 Juni, 2014

Tunafahamu, issu ya Mabomu ni fear Propaganda za wana ccm ku pre empty strategies za wapinzani wakekote nchini!!!!! Amini usiamini.
 
Bado kidogo utaona Faizafoxy, Polite watatwambia hilo bomu limerushwa na MAREKANI
 
Strategies za ccm kuogopesha watu.ikumbukwe mwingulu kesho yake alisema na bado
 
Mkuu baada ya Kumaliza kusoma post yako hii na kuielewa nilijikuta nacheka ghafla ha ha ha ha ha ha ha ha :smile-big:

MKUU umecheka basi wewe maisha yako yana UHAKIKA MKUBWA! Mimi ambaye sina UHAKIKA wa MAISHA YANGU sina mahali pa kupata hicho KICHEKO, kwa hiyo ninabakia najiuliza hivi: Hiyo taarifa ina tofauti gani na taarifa yoyote inayoweza kutolewa na mtu wa KAWAIDA yaani kuonyesha maskitiko yake ingawa hana UWEZO WOWOTE WA KUFANYA ili hiyo mishetani ikamatwe!
 
Tunafahamu, issu ya Mabomu ni fear Propaganda za wana ccm ku pre empty strategies za wapinzani wakekote nchini!!!!! Amini usiamini.
Hata mimi naona haya mabomu ni mkakati wa watawala ama kuna watu ndani ya Serikali wanaotumia mkakati huu wapate kisingizio cha kuendelea na agenda zao.
 
Soma taarifa hii ya IKULU ya Dar es salaam kuhusu Bomu la Zanzibar

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za pole Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein kufuatia kuuawa kwa mtu mmoja na wengine sita kujeruhiwa akiwemo mhubiri wa amani ajulikanaye kama Sheikh Ahmed Haidari Jabir wa Zanzibar, kutokana na kurushwa kwa Bomu katika shughuli ya kidini iliyokuwa ikifanyika katika eneo la Darajani tarehe 13 Juni,2014, mjini Unguja.

‘Hicho ni kitendo cha kulaaniwa kwa nguvu zote na watu wote wapenda amani Bara na Visiwani, ni kitendo cha woga na kisicho na ustaarabu na wala hakikubaliki katika dunia ya sasa’ Rais amesema na kuongeza kuwa; ‘Hiki ni kitendo kilichofanywa na watu waoga, wasio na ustaarabu wa aina yeyote ile’.

Rais amekemea na kuwataka watu kuwa wastaarabu, wavumilivu na kuheshimu imani na mitizamo ya watu wengine hata kama hawakubaliani nao.

Rais amesema amesikitishwa zaidi na watu hao wasio na ustaarabu ambao wamefanya kitendo hicho cha kihalifu kwenye shughuli ya kidini ambapo ndipo mahali panapostahili Amani, Uvumilivu na Unyenyekevu zaidi kwa kuwa ni wakati ambapo binadamu anapofanya mawasiliano na muumba wake.

Rais Kikwete amelitaka Jeshi la Polisi kuwasaka na kuwafikisha mbele ya vyombo vya haki wale wote waliohusika katika tukio hilo lisilo la kistaarabu.

Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu-Dodoma
15 Juni, 2014

Yaani Rais wa nchi kazi yake ni kukemea?? !! ..
 
Sasa yeye JK kama Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri anachukua hatua gani dhidi ya watu hao? Au salamu kwa Shein ili iweje sasa? au Salamu hizi ili iweje? kwani Shein si Mkuu wa Majeshi au Mwenye Jukumu la Usalama wa Tanzania kimamlaka...au JK amesahau kuwa maeneo ya Ulinzi na Usalama wa Tanzania ni jukumu (lake) la mambo ya Muungano?

Tanzania inahitaji serikali inayojitambua na kiongozi makini mwenye kujua na kutambua mamlaka ya kazi yake. Kwani ukingalia ukubwa wa tukio na hiyo taarifa unaona kuna udhaifu mkubwa wa utekelezaji wa ki-mamlaka na licha ya kupwaya kiungozi lakini unaona ni kwa kiasi gani ombwe la uongozi na zinavyoathiri uendeshaji wa serikali na hata kufikia kuteteresha mfumo mzima wa mamlaka za Kikatiba nchini.
 
Soma taarifa hii ya IKULU ya Dar es salaam kuhusu Bomu la Zanzibar

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za pole Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein kufuatia kuuawa kwa mtu mmoja na wengine sita kujeruhiwa akiwemo mhubiri wa amani ajulikanaye kama Sheikh Ahmed Haidari Jabir wa Zanzibar, kutokana na kurushwa kwa Bomu katika shughuli ya kidini iliyokuwa ikifanyika katika eneo la Darajani tarehe 13 Juni,2014, mjini Unguja.

‘Hicho ni kitendo cha kulaaniwa kwa nguvu zote na watu wote wapenda amani Bara na Visiwani, ni kitendo cha woga na kisicho na ustaarabu na wala hakikubaliki katika dunia ya sasa’ Rais amesema na kuongeza kuwa; ‘Hiki ni kitendo kilichofanywa na watu waoga, wasio na ustaarabu wa aina yeyote ile’.

Rais amekemea na kuwataka watu kuwa wastaarabu, wavumilivu na kuheshimu imani na mitizamo ya watu wengine hata kama hawakubaliani nao.

Rais amesema amesikitishwa zaidi na watu hao wasio na ustaarabu ambao wamefanya kitendo hicho cha kihalifu kwenye shughuli ya kidini ambapo ndipo mahali panapostahili Amani, Uvumilivu na Unyenyekevu zaidi kwa kuwa ni wakati ambapo binadamu anapofanya mawasiliano na muumba wake.

Rais Kikwete amelitaka Jeshi la Polisi kuwasaka na kuwafikisha mbele ya vyombo vya haki wale wote waliohusika katika tukio hilo lisilo la kistaarabu.

Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu-Dodoma
15 Juni, 2014

Rais anakemea yamekua mapepo hayo, Nilitegemea kusikia Rais anaagiza hivi na vile.
 
Back
Top Bottom