Taarifa ya Ikulu ya JK kuhusu Bomu la Zanzibar Ijumaa jioni

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Sep 7, 2011
3,295
2,500
Soma taarifa hii ya IKULU ya Dar es salaam kuhusu Bomu la Zanzibar

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za pole Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein kufuatia kuuawa kwa mtu mmoja na wengine sita kujeruhiwa akiwemo mhubiri wa amani ajulikanaye kama Sheikh Ahmed Haidari Jabir wa Zanzibar, kutokana na kurushwa kwa Bomu katika shughuli ya kidini iliyokuwa ikifanyika katika eneo la Darajani tarehe 13 Juni,2014, mjini Unguja.

‘Hicho ni kitendo cha kulaaniwa kwa nguvu zote na watu wote wapenda amani Bara na Visiwani, ni kitendo cha woga na kisicho na ustaarabu na wala hakikubaliki katika dunia ya sasa’ Rais amesema na kuongeza kuwa; ‘Hiki ni kitendo kilichofanywa na watu waoga, wasio na ustaarabu wa aina yeyote ile’.

Rais amekemea na kuwataka watu kuwa wastaarabu, wavumilivu na kuheshimu imani na mitizamo ya watu wengine hata kama hawakubaliani nao.

Rais amesema amesikitishwa zaidi na watu hao wasio na ustaarabu ambao wamefanya kitendo hicho cha kihalifu kwenye shughuli ya kidini ambapo ndipo mahali panapostahili Amani, Uvumilivu na Unyenyekevu zaidi kwa kuwa ni wakati ambapo binadamu anapofanya mawasiliano na muumba wake.

Rais Kikwete amelitaka Jeshi la Polisi kuwasaka na kuwafikisha mbele ya vyombo vya haki wale wote waliohusika katika tukio hilo lisilo la kistaarabu.

Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu-Dodoma
15 Juni, 2014
 
hiyo siyo tarifa ya ikulu unatunga vineno vyako unaita tarifa ya ikulu kwenda zako.
 
hii tarifa umetoa leo Rais leo hayuko dodoma danganya watoto wadogo.
 
Soma taarifa hii ya IKULU ya Dar es salaam kuhusu Bomu la Zanzibar

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za pole Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein kufuatia kuuawa kwa mtu mmoja na wengine sita kujeruhiwa akiwemo mhubiri wa amani ajulikanaye kama Sheikh Ahmed Haidari Jabir wa Zanzibar, kutokana na kurushwa kwa Bomu katika shughuli ya kidini iliyokuwa ikifanyika katika eneo la Darajani tarehe 13 Juni,2014, mjini Unguja.

‘Hicho ni kitendo cha kulaaniwa kwa nguvu zote na watu wote wapenda amani Bara na Visiwani, ni kitendo cha woga na kisicho na ustaarabu na wala hakikubaliki katika dunia ya sasa’ Rais amesema na kuongeza kuwa; ‘Hiki ni kitendo kilichofanywa na watu waoga, wasio na ustaarabu wa aina yeyote ile’.

Rais amekemea na kuwataka watu kuwa wastaarabu, wavumilivu na kuheshimu imani na mitizamo ya watu wengine hata kama hawakubaliani nao.

Rais amesema amesikitishwa zaidi na watu hao wasio na ustaarabu ambao wamefanya kitendo hicho cha kihalifu kwenye shughuli ya kidini ambapo ndipo mahali panapostahili Amani, Uvumilivu na Unyenyekevu zaidi kwa kuwa ni wakati ambapo binadamu anapofanya mawasiliano na muumba wake.

Rais Kikwete amelitaka Jeshi la Polisi kuwasaka na kuwafikisha mbele ya vyombo vya haki wale wote waliohusika katika tukio hilo lisilo la kistaarabu.

Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu-Dodoma
15 Juni, 2014

jibu liko hapa; "

Rais amekemea na kuwataka watu kuwa wastaarabu, wavumilivu na kuheshimu imani na mitizamo ya watu wengine". Kumbe keshawajua wahusika!!?? Tuna safari ndefu sana.
 
Hivi hiyo taarif inazuia vipi milipuki mingine isitokee? Mbona taratibu sasa nchi yetu tanaanza kuzoea mabomu na kuishi kwa wasi wasi? Ngoja niishie hapa nisije kutukana bure
 
.umma utaanza kuamini kuwa walipua mabomu hawa wana mkono wa serikali hii.....maana mbona hawakamatwi???waliorusha mabomu Arusha kanisani na mkutanoni na sasa Zenj....woote hawajakamatwa!!haiwezekani...kwani nchi hii imekua Afganistan..ama Somalia??ama Iraki??....amani gani inatangazwa na utawala huu?
 
Back
Top Bottom