Taarifa Ya EU: SMZ Yabwatuka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taarifa Ya EU: SMZ Yabwatuka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Junius, Aug 14, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Aug 14, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imeionya Jumuiya ya Nchi za Ulaya (EU) na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania kutoiingilia kabisa mambo yake ya ndani na pia imeuponda utafiti wa kisiasa kuhusu mbio za urais wa Zanzibar mwaka 2010 uliofanywa na kampuni ya the Steadman Group kwa kuuita ni wa kitapeli.

  Onyo hilo kwa EU na kupondwa kwa utafiti ulioonyesha kubashiri kukubalika kwa wagombea wa urais huku Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad na Waziri Kiongozi wa awamu ya tano Dk Mohamed Gharib Bilal wakikabana koo, limetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Kiongozi Hamza Hassan Juma katika mkutano wake na waandishi wa habari ofisini kwake Vuga Mjini hapa jana.

  Juma alisema Zanzibar ina mamlaka yake kamili ya kikatiba na kisheria na hivyo haiongozwi kwa shinikizo la mtu au jumuiya yeyote kutoka nje au ndani ya nchi.

  Alisema kampuni ya Steadman Group juni 18 mwaka huu iliiomba ofisi ya Waziri Kiongozi ifanye utafiti juu ya masuala ya kiutamaduni na kiuchumi lakini kwa makusudi wamekiuka taratibu na kufanya utafiti wa kisiasa kinyume na ombi lao la msingi.

  “SMZ haiongozwi kwa kumuogopa mtu au kwa shinikizo lolote,ina katiba yakae,sheria zinayosimamia masuala mbalimbali na upana mkubwa wa maendeleo ya demokrasia ‘Alisema

  Waziri huyo wa Nchi Ofisi ya Waziri Kiongozi alisisitiza kuwa SMZ ina utawala wake kamili ikiwemo pia na sheria inayosimamia uchaguzi ambayo iliyopitishwa na BLW kama chombo cha kutungia sheria.

  ‘hatuongozwi na EU wala AU,sisi ni nchi yenye kuheshimu sheria zake na kufuata utawala bora,demokrasia na kuheshimu haki za binadamu,EU wanatakiwa wafanye utafiti wa kutosha huko Pemba kabla ya kutoa shutuma”Alionya

  Alieleza kuwa mazingira mazima ya zoezi la uandikishaji katika daftari la kudumu la wapiga kura huko Pemba yanakwamishwa na wanasiasa wa vyanma vya upinzani wanaowachochea wafuasi wao wavunje na kukiuka sheria jambo ambalo alidai kamwe halitavumiliwa na vyombo vya serikali.

  Hata hivyo amemtupia lawama nyingi Katibu Mkuu wa chama cha Wananchi CUF Maalim Seif na kumtaja kama ni mtu mmojawapo anayefanya mikutano ya hadhara ya uchochezi ili kuhatarisha amani katika kisiwa cha Pemba.

  “serikali haitamtazama na kumvumilia mtu yeyote ambaye ataamua kuvunja na kukiuka sheria,vitambulisho vya ukaazi vinatajwa katika sheria ya uchaguzi hivyo kila anayetaka kuandikishwa ni lazima awe na sifa ya ukaazi wa miaka mitatu mfululizo”Alifafanua

  Kuhusu utafiti uliofanywa na Steadman Group aliubeza na kusema ni utafiti uliojaa utapeli ambao ulikiuka maudhui yaliotajwa na wahusika wakati wakiomba kibali cha kuendesha zoezi hilo la utafiti katika visiwa vya Pemba na Unguja.

  Waziri Juma alisema juni 18 mwaka huu kampuni hiyo iliwasilisha barua ikiomba kufanya utafiti juu ya masuala ya hali ya kiuchumi na kiutamaduni na siyo kutafuta kura ya maoni kuhusu mbio za urais mwaka 2010 na kuupotosha umma.

  “SMZ inaitaka kampuni hiyo kuomba radhi kupitia vyombo vya habari kuhusu upotoshaji wa habari uliofanyika kwamba Seif Sharif Hmad ndiye anaeyekubalika kwa nafasi ya urasi wa Zanzibar”

  Alisema kwa kukiuka mantiki ya ombi lao la awali katika kuendesha kwao utafiti walioukusudia ni wazi kampuni hiyo itakuwa imeidanganya serikali,ofisi ya waziri Kiongozi na kuupotosha umma.

  Aidha nakala ya barua ya kampuni ya Steadman ya juni 18 mwaka huu iliyotumwa kwenda kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Kiongozi Zanzibar inaoyesha kuomba kufanya utafiti juu ya masuala ya uchumi na utamaduni ili kupata maoni ya watu na kuweza kufahamu sekta zipi wangependelea serikali ya Tanzania kuboresha.

  Alipotakiwa ataje athari zilizomepatikana kutokana na matokeo ya utafiti huo alisema zimeutikisa mfumo wa siasa za zanzibar na pia kuwapotezea mwelekeo na matarajio watu wenye kui ya kuwania urais kwa kufanya utabiri wa kitapeli.

  “hata Naibu Katibu Mkuu wa CUF Juma Duni Haji pengine alikwa na nia ya kuwania urais ili ashindane na Seif inawezekana amekatishwa tamaa,lakini pia si msingi wa ombi la kampuni husika bali kilichofanyika ni hadaa na utapeli”Aliongeza

  Katika hatua nyingine Waziri Juma alibainisha kuwa SMZ kamwe haitamkamata Maalim Seif Sharif Hamad na kumuweka kolokoloni licha ya kufanya kwake uchochezi wa makusudi ambao ni kosa la jinai.

  Alisema Maalim Seif anachochea wafuasi wake ili wavunje sheria na kusema atazidi kufanya hivyo bila kuchoka kwa kutegemea akamatwe ili apate umaarufu wa kisiasa jambo ambao SMZ kamwe halitafanya.

  “hatuna mpango wa kumkamata Maalim Seif na kumfikisha kortini,yule atamalizika kidogo kidogo mpaka wananchi watampuuza,ni jamaa yetu,mwenzetu,analipwa maslahi yake na SMZ hakuna wa kumkamata na kufanya hivyo ni kumjenga”Alisisitiza.

  SOURCE: ZANZIBAR YETU WEB BLOG.
   
 2. M

  Msengi Kiula Senior Member

  #2
  Aug 14, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 121
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Kazi kweli!
   
 3. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #3
  Aug 14, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Huyo jamaa tayari anaonekana kupuuzwa kule. Wanaomshabikia ni wale wale wasiojijua ambao wanaishi Dar , Tanga, Mombasa. Somali na UK raha mustarehe. na hawajui kinachoendelea haswa kijiweni, na hawaielewi hali halisi ya wale (watoto wetu) wanaozinga kokochi na (mama zao) wanaolima mihogo Shumba na Chanja-Njawiri.
   
 4. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #4
  Aug 14, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Hawa jamaa ndio wanaopigania uhuru wa zanzibar kutoka Tanzania teh teh teh kazi iko.
  Ama walikuwa wanatikisa kiberti mbona Pinda alipobwatuka ngoma zote zimekaa kimya na mchezo ukarudi neutral du
   
 5. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #5
  Aug 14, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Lakini waliotowa maoni ya kukubalika kwake(Maalim) hawatoki UK wala huko unakosema ni Wazanzibari hao hao wa Chanja-Mjawiri, Mjimkongwe, Mlandege, Rahaleo, Kwa hani n.k, wala Synovate hawakwenda Mombasa na UK kutafuta maoni hayo, naona jamaa yangu Hamza anatapatapa, kapewa kazi ya Shamhuna ya kumuandama Maalim Seif, atamuweza wapi, wakati Nyerere kashindwa!!!
   
 6. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #6
  Aug 14, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  MkamaP umenichekesha sana maneno yako hayo.
  Hawa jamaa wa CCM na SMZ nadhani ni wapuuzi .Yaani wakienda kuomba pesa EU na kwingineno huwa hawajui kwamba wanaweza kuacha kuomba nakujiendesha ? Wakitumia mabavu wakiambiwa wanasema wasitishwe ? Kauli hizi wamezipata kwa Membe.Yaani wana ongea huko Vuga badala kuwaita watu wa EU na wawakilishi wengine na kuwa onya .Kweli kazi kubwa hapa .Kule mkoani mtu kufanya utafiti mtaani lazima waziri kiongozi aambiwe ? Jamaa hawa wamekamatwa kubaya wanafyatuka kuanzia bara hadi kisiwani .

  Zanzibar hawana jeshi wala polisi .Amri zote Dar leo jamaa anasemaje ?Kweli kajisahau huyu .
   
 7. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #7
  Aug 14, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Huwezi ku claim sovereignty kwa dhati wakati bajeti yako inasaidiwa na wageni kwa kiasi cha kusikitisha.
   
 8. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #8
  Aug 14, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Unajuwa walivyomsakam pinda nahisi alisema sasa mtajijuu na muone moto wa Sheikh Seif ,sasa ngoma zote zimelowana hazidundi tena ,wametulia tuli
   
 9. T

  T_Tonga Member

  #9
  Aug 14, 2009
  Joined: Jul 24, 2007
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  uwaziri wa kupewa una matatizo yake hawa smz wana ubavu gani wa kuwa hawaogopi eu ndio wanao wagawia pesa wao na kaka yao hakuna bajeti yoyote tz biya ya wao hemu jaribu kushindana nao uone na sio unakurupuka tu na kusema mtafanya nini nye smz huko sasa ni kutapatapa tu mambo magumu tangu lini vifaru na majeshi kwenye uchaguzi hilo ndio kila siku mnafanya lakini mna mwisho wenu wewe waziri mzima huna unalolijua unatumiwa lakini ujue iko siku ya smz kumalizika
   
 10. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #10
  Aug 15, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Koh koh koh.....MMhm!
   
 11. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #11
  Aug 15, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Viongozi wa kibongo huwa wanataka kusifiwa tu, wakiambiwa ukweli ambao hauwasifii basi hugeuka mbogo.
   
 12. M

  Magezi JF-Expert Member

  #12
  Aug 15, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  CCM wote ni sawa tu hakuna cha JMT wala SMZ mawazo yao ni mamoja.
   
 13. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #13
  Aug 15, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Si nilisema wanamuogopa????
   
 14. a

  akili Member

  #14
  Aug 15, 2009
  Joined: May 5, 2008
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mheshimiwa Rais Kikwete peleka viongozi wa Zanzibar shule ya diplomasia wajue nini kinafaa kuzungumzwa hadharani na nini faraghani kwa kiongozi wa nchi kama kweli ni nchi au hawajui hili?

  Angalia huyu aliyelipuka hivi:
  "Keep off Zanzibar's voters roll, donors told," swali laja je na donors nao wakisema:
  "Keep off donors' money, Zanzibaris told," nani ataonekana mjinga kuliko mwininge?

  Akili kichwani mwako. Lakini ndiyo matunda ya hamnazo kuchangua hamnazo!
   
 15. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #15
  Aug 15, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kwanini huwi mkweli? Kwanini nyie CCM anapotajwa tu mnakurupuka? Hebu waachieni wananchi waamuwe.
  Unajuwa kwa mtu mzima kuwa muongo si jambo zuri. Hata kama mgombea wa CCM huwa anashnda (juu ya udanganyifu mkubwa) huyu jamaa huwa anapitwa kwa kura chache sana, sasa hiyo kupuuuzwa mnakokwita kunakujaje.
  Mbona sote tu watu wazima na tuhoji kiutu uzima.
  Yaani kama chuki inauwa basi huyu jamaa angekwishaoza kwa chuki ya watu kama Pakacha.
   
 16. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #16
  Aug 15, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  " Kwa suala la utaifa wa Zanzibar..... mimi na Karume letu moja" Seif Sharif Hamad
   
 17. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #17
  Aug 15, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  WEWE HUWAJUI HAO! Damu ,jasho lakini mpango wao utikie kwani kushindwa kwa mipango michafu ndio Kaburi lao!
   
 18. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #18
  Aug 15, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Yale yale ya 2000 na 2005 yanataka yajirudie tena 2010.

  Hakika hakuna uongo usio na mwisho.
   
 19. Eqlypz

  Eqlypz JF-Expert Member

  #19
  Aug 15, 2009
  Joined: May 24, 2009
  Messages: 4,069
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo Seif Sharrif Hamad anagombea tena mwaka 2010?
   
 20. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #20
  Aug 15, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Zamani alipokuwa na Madevu
   
Loading...