Taarifa ya CCM

Taarifa ya CCM

security guard

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2011
Posts
799
Reaction score
603
Ijumaa iliyopita Mei 3, 2013 Msemaji wa kambi ya Upinzani Bungeni Masuala ya katiba na Sheria Ndg. Tundu Lissu katika hotuba yake pamoja na kuzishutumu taasisi zingine, lakini pia alitoa tuhuma kadhaa dhidi ya CCM.

Tuhuma hizo zilielekezwa kwenye maeneo kadhaa hasa yahusuyo suala la mchakato wa uundwaji wa katiba mpya unaoendelea nchini na ushiriki wa makundi tofauti katika mchakato huo.

Katika kuipa uzito hoja hiyo, Lissu alitoa malalamiko mengi dhidi ya CCM kwa madai kuwa tumeteka mchakato huo kwa kujaza Makada wa CCM katika Mabaraza ya Katiba yaliyoundwa kwenye ngazi ya kata hivi karibuni.

CCM Kama ilivyo taasisi yoyote makini na wenye uzalendo kwa nchi yao, katika mchakato wa uundwaji wa katiba mpya ina jukumu la kuwahamasisha wanachama na wasio wanachama wake kushiriki mchakato wa katiba nchini kutokana na kutambua umuhimu wake.

Tofauti ya CCM na Chadema katika hili ni, wakati CCM tunahamasisha watu washiriki kwenye mchakato wa katiba nchini, Chadema wao wanahamasisha watu wavuruge au wasishiriki kabisa mchakato huu.

Mfano mzuri ni jitihada zao za kuziria mchakato huu kwa visingizio vya kitoto kabisa. Juhudi zao za kumtaka Prof. Baregu, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, ambaye wao Chadema walimpendekeza kwenye tume, ajitoe kwenye tume zinafahamika na wala sio SIRI.

CCM inampongeza kwa dhati Prof. Baregu kwa uzalendo na ukomavu wa kisiasa aliouonyesha kwa kuwakatalia kujitoa kwenye tume na kuweka mbele masilahi ya taifa lake. Kukataa kwa Prof. Baregu kujitoa kwenye tume kwa hoja za kitoto kabisa za Chadema ilipaswa kuwa fundisho kwa vibaraka hawa.

Ilivyo fanya CCM, kuhamasisha wanachama na watanzania kwa ujumla kushiriki mchakato huo, ndivyo taasisi nyingine pia zilivyofanya. Zikiwemo taasisi za dini ambazo zimekuwa zikihamasisha zoezi hili kupitia mikusanyiko ya Ibada, Taasisi zisizo za Kiserikali yaani NGOs kwa kufanya makongamano na makundi mengine kwa kuendesha midahalo, dhambi kwa CCM inatoka wapi?.

Ifahamike kuwa mawasiliano na mjadala juu ya zoezi la mchakato wa uundwaji wa katiba mpya nchini hayakuanza jana ndani ya CCM, bali yalianza siku nyingi kwa Chama kuunda kamati iliyopitia na kuja na maoni ya CCM juu ya nini kiwemo kwenye katiba mpya.

Taarifa hiyo haikufanywa Siri. Iliwasilishwa mbele ya vikao kadhaa vya Chama na kisha kutangazwa kwa umma. Hivyo hoja kwamba mawasiliano ndani ya Chama juu ya mchakato huo wa Katiba nchini umelenga kuhujumu mchakato huo hayana maana yoyote, badala yake hoja hiyo imebeba mtazamo finyu wa wanasiasa wenye tabia za nguruwe za kula watoto wake mwenyewe pindi apatapo njaa.

Chadema ni kama nguruwe ambaye huweza kuzaa watoto wake kisha akishikwa njaa huanza kuwala watoto wake mwenyewe. Mchakato wa katiba nchini ni matunda ya viongozi wa CCM akiwemo Rais Jakaya Kikwete, Mwenyekiti wa CCM Taifa, kutangaza kuanza kwa mchakato huu. Hatuwezi kuuzaa wenyewe mchakato halafu tukauhujumu wenyewe mchakato huo.

Itakumbukwa umezuka utamaduni mbaya kwa baadhi ya Wabunge wa CHADEMA kutumia Bunge kama jukwaa la kuwashambulia isivyo sawa watu ambao hawana fursa ya kuingia Bungeni kujibu mashambulizi hayo. Utamaduni huu ni wa hovyo unakiuka haki za msingi ambazo zinataka mtu anayetuhumiwa/kushutumiwa apewe fursa ya kusikilizwa. Watanzania lazima tuukatae utamaduni huu.

Hivi karibuni baadhi ya Wabunge wa CHADEMA wamefanya vitendo vya aibu vilivyowakera sana Watanzania. Hili bado limo kwenye akili na midomo ya watu na sasa Chadema wanatafuta namna ya kuficha aibu yao(nitoke vipi) kwa kurukia hoja ya Mabaraza, kuzusha na kushutumu watu kwa uongo uliokubuhu.

Vituko vyote hivi vya Chadema vimeongezeka baada ya katibu mkuu wa CCM hivi karibuni mjini Morogoro kutoa maelezo ya kina na hoja nzito dhidi ya ukibaraka wa Chadema kwenye suala zima la mchakato wa Katiba.

Nchi nyingi hasa za Afrika zilizokumbwa na machafuko moja ya ajenda kubwa ilikuwa ni swala la katiba mpya. Sasa hapa nchini Chadema wanaona watanzania wanaendelea na mchakato bila machafuko wanakosa majibu kwa mabeberu wanaowafadhili kuchafua nchi yetu, ndio maana kila kukicha wanakuja na visa na vituko kusumbua mchakato wa katiba.

Walianza kwa kukataa matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 ikiwemo kutomtambua rais. Wakatangaza hadharani nchi haitatawalika kisa wamenyimwa ridhaa na watanzania. Mchakato ulipoanza wa katiba mpya wabunge wao wakazira na kutoka nje ya bunge, baada ya muda wakarudi.

Juzi bungeni wametishia kujitoa kwenye mchakato wa katiba ifikapo tarehe 30/04/2013, leo ni tarehe 05/05/2013!! Wamezoea kutishia nyau, tumechoka na vitisho vya vibaraka hawa. Tunapongeza msimamo wa Tume ya mabadiliko ya Katiba kwa kupuuza hoja ya kufuta mabaraza ya katiba. Chadema wakisusa na wasuse tu.

Tunawasihi watanzania wote wapuuze utoto na ukibaraka huu wa Chadema kwani ugonjwa wao tumesha ufahamu WANAUMWA KIFAFA CHA SIASA. Kila ugonjwa huu ukipanda wanatupa mateke sana. Tuwaombee ipo siku huenda mwenyezi Mungu atawarehemu watapona.

Taarifa mbona haina menyewe? Nilitegemea kuona jina na saini ya mtoa tamko na si mawazo ya security guard!
 
Last edited by a moderator:
Kidumu chama cha mapinduzi. Kazi iendelee.
 
hii si taarifa ya yule mtoto anaepekuapekua ndani ya wazee wa ccm akijaribu kujua nani baba yake katika wazee waliolala singida usiku ya nkuzaliwa chama miaka hiyo?
 
Aliyeandika upuuzi huu siamini kama anaakili timamu.
 
Hivi ni kweli kwamba CCM imeshuka kiasi hiki ? Hii ni Taarifa ya CCM au inatoka T.O.T PLUS ?
 
Ama kweli ccm mmeishiwa taarifa imejaa matusi na mipasho tu! Jaribuni kutuliza akili na kujibu hoja , acheni jazba na matusi kama wabunge wenu.
 
hii si taarifa ya yule mtoto anaepekuapekua ndani ya wazee wa ccm akijaribu kujua nani baba yake katika wazee waliolala singida usiku ya nkuzaliwa chama miaka hiyo?

kuna mtu kaanzisha uzi ana muulizia, huyo hapo sasa.

Inshort nilianza kuisoma nikitegemea itaendelea kutolea ufafanuzi hoja ya Lissu kwa maelezo yenye mashiko.

ilipoanza tu sehemu ya baregu kwa kumpongeza huku zikitolewa hoja nyepesi na mipasho nikaishia hapo hapo hata siisomi tena.
 
Camon Serukamba you...

Eti serikali ya CCM ya kizalendo.Mbona haina uzalendo kwa tembo wetu?,mbona haina uzalendo kwenye twiga wetu? mbona haina uzalendo kwenye madini yetu?

Eti Chadema ni vibaraka wa mabeberu. Mbona JK alihongwa suti na hao mabeberu? Mbona JK haishi safari za huko kwa mabeberu? Suti tu zimemfanya aingize nchi kwenye mikataba mibovu. Kama CCM ni chama cha kizalendo basi hata ibilisi ataingia peponi. Twiga na urefu wake kakunjwa mpaka akatosha kwenye ndege. Meli za Kinana zinamaliza tembo wetu. Kama mwenyekiti wa chama anahongwa suti na katibu wa chama atafanya biashara ya meno ya tembo, usitegemee kabisa chama kitatoa serikali ya kizalendo. Hapo zao lake ni ufisadi na ujangiri tu.
 
Chama cha wanafiki, hii nini sasa...hivi humu kuna watoto? ...nani atakubaliana na report ya kijinga namna hii
 
Chadema ni kama nguruwe ambaye huweza kuzaa watoto wake kisha akishikwa njaa huanza kuwala watoto wake mwenyewe. Mchakato wa katiba nchini ni matunda ya viongozi wa CCM akiwemo Rais Jakaya Kikwete, Mwenyekiti wa CCM Taifa, kutangaza kuanza kwa mchakato huu. Hatuwezi kuuzaa wenyewe mchakato halafu tukauhujumu wenyewe mchakato huo.

Hawa jamaa wanadhani sisi ni vishoka! leo wanasema mchakato wa katiba walianzisha wao, wakati wote tunajua ni kiasi gani waliupinga.
 
MLENGWA WA MLIPUKO ALIKUWA BALOZI WA VATICAN?

(Naona mods wana watu wao wenye haki ya kuanzisha threads, sisi wengine haturuhusiwi)

Ndugu WanaJamvi;

Kwa muda sasa kumekuwa na hoja mbali mbali juu ya uhalali wa uwepo wa Ubalozi wa Vatican hapa Tanzania. Katika hili kuna, kuna pande kuu mbili zinazokinzana - wanaopinga na wanaounga mkono kama ifuatavyo:-

(1) Wanaopinga: wanajenga hoja kwamba kwa kuwa Vatican ni nchi ya kidini (Kikatoliki) na kwa kuwa, kwa mujibu wa Katiba, Tanzania haina dini hivyo sio sahihi kwa "nchi" hiyo kuwa na ubalozi wake hapa nchini. Wengine wanaenda mbali zaidi kiasi kwamba hawataki kukubali Vatican ni nchi. Hata hivyo "wanalegeza" masharti kwamba kama Vatican ina ubalozi wake hapa basi ni halali kwa Tanzania kama nchi kuwa mwanachama wa taasisi za kidini kama OIC. La kushangaza hapa ni kwamba kwao uhalali wa Ubalozi wa Vatican utakuwepo endapo Tanzania itakuwa mwanachama wa hizo taasisi za kidini vinginevyo sio halali.

(2) Wanaounga mkono:hawa wanajenga hoja kwamba; kwanza Vatican ni nchi huru, yenye mamlaka kamili, na inayojitegemea kwa mujibu wa tafsiri sahihi ya neno "nchi" lilivyo na linavyotambulika kimataifa. Na wanaenda mbali zaidi kwamba sio tu kwamba Vatican ni nchi bali inatambulika hivyo rasmi na UN. Hivyo, kwa hoja hii, ni sahihi kabisa Vatican na Tanzania kuwa na mabalozi wanowakilisha nchi zao.

MLIPUKO WA LEO:

Kati ya viongozi wakuu wa Kanisa waliokuwepo kwenye shughuli ya leo kule Olasiti, Arusha, ni Balozi wa Vatican nchini Tanzania ambaye pia ana hadhi ya Askofu Mkuu. Hivyo zimeanza kuzagaa habari pengine kutokana na ukinzani wa baadhi ya makundi kutotaka Vatican kuwa na ubalozi wake hapa nchini, kuna uwezekano pia mlengwa mkuu alikuwa Balozi husika. Mimi sijui, ila kama GT tudadavue na hili.

LAWAMA:

Lawama pia zimeanza kuelekezwa kwa serikali kwa kutochukua hatua madhubuti na kwa wakati pindi zinapotokea chochoko kama hizi katika jamii. Kwa mfano, hili la upotoshoji wa uhalali wa Ubalozi wa Vatican hapa nchini propaganda zake zimeenezwa kwa muda mrefu sana kwa njia mbalimbali kama mihadhara, ibada, na hata kwenye media mbalimbali. Badala ya serikali kutolea ufafanuzi wa uhalali wa huo ubalozi, imekuwa kimya bila kujali athari za baadaye za propaganda hizi chafu pengine kwa falsafa ya "ni upepo tu utapita". Je, ni kweli serikali inastahili lawama katika hili?

HITIMISHO:

Je, kama serikali ikitekeleza madai YOTE ya haya makundi, kuna uwezekano wa chokochoko hizi kukoma na hivyo nchi yetu kuwa ya amani na utulivu kama ilivyoachwa na waasisi wetu? Lakini je, walengwa wa haya matukio ni wakatoliki peke yao? Au ni pamoja na makundi mengine? Haya matukio yana uhusiano wowote na siasa za nchi yetu? Mimi sijui, nalileta kwenu wakuu.
 
Mbona haionyeshi hata hoja moja kati ya zilizoibuliwa na Tundu Lissu?
 
Ijumaa iliyopita Mei 3, 2013 Msemaji wa kambi ya Upinzani Bungeni Masuala ya katiba na Sheria Ndg. Tundu Lissu katika hotuba yake pamoja na kuzishutumu taasisi zingine, lakini pia alitoa tuhuma kadhaa dhidi ya CCM.

Tuhuma hizo zilielekezwa kwenye maeneo kadhaa hasa yahusuyo suala la mchakato wa uundwaji wa katiba mpya unaoendelea nchini na ushiriki wa makundi tofauti katika mchakato huo.

Katika kuipa uzito hoja hiyo, Lissu alitoa malalamiko mengi dhidi ya CCM kwa madai kuwa tumeteka mchakato huo kwa kujaza Makada wa CCM katika Mabaraza ya Katiba yaliyoundwa kwenye ngazi ya kata hivi karibuni.

CCM Kama ilivyo taasisi yoyote makini na wenye uzalendo kwa nchi yao, katika mchakato wa uundwaji wa katiba mpya ina jukumu la kuwahamasisha wanachama na wasio wanachama wake kushiriki mchakato wa katiba nchini kutokana na kutambua umuhimu wake.

Tofauti ya CCM na Chadema katika hili ni, wakati CCM tunahamasisha watu washiriki kwenye mchakato wa katiba nchini, Chadema wao wanahamasisha watu wavuruge au wasishiriki kabisa mchakato huu.

Mfano mzuri ni jitihada zao za kuziria mchakato huu kwa visingizio vya kitoto kabisa. Juhudi zao za kumtaka Prof. Baregu, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, ambaye wao Chadema walimpendekeza kwenye tume, ajitoe kwenye tume zinafahamika na wala sio SIRI.

CCM inampongeza kwa dhati Prof. Baregu kwa uzalendo na ukomavu wa kisiasa aliouonyesha kwa kuwakatalia kujitoa kwenye tume na kuweka mbele masilahi ya taifa lake. Kukataa kwa Prof. Baregu kujitoa kwenye tume kwa hoja za kitoto kabisa za Chadema ilipaswa kuwa fundisho kwa vibaraka hawa.

Ilivyo fanya CCM, kuhamasisha wanachama na watanzania kwa ujumla kushiriki mchakato huo, ndivyo taasisi nyingine pia zilivyofanya. Zikiwemo taasisi za dini ambazo zimekuwa zikihamasisha zoezi hili kupitia mikusanyiko ya Ibada, Taasisi zisizo za Kiserikali yaani NGOs kwa kufanya makongamano na makundi mengine kwa kuendesha midahalo, dhambi kwa CCM inatoka wapi?.

Ifahamike kuwa mawasiliano na mjadala juu ya zoezi la mchakato wa uundwaji wa katiba mpya nchini hayakuanza jana ndani ya CCM, bali yalianza siku nyingi kwa Chama kuunda kamati iliyopitia na kuja na maoni ya CCM juu ya nini kiwemo kwenye katiba mpya.

Taarifa hiyo haikufanywa Siri. Iliwasilishwa mbele ya vikao kadhaa vya Chama na kisha kutangazwa kwa umma. Hivyo hoja kwamba mawasiliano ndani ya Chama juu ya mchakato huo wa Katiba nchini umelenga kuhujumu mchakato huo hayana maana yoyote, badala yake hoja hiyo imebeba mtazamo finyu wa wanasiasa wenye tabia za nguruwe za kula watoto wake mwenyewe pindi apatapo njaa.

Chadema ni kama nguruwe ambaye huweza kuzaa watoto wake kisha akishikwa njaa huanza kuwala watoto wake mwenyewe. Mchakato wa katiba nchini ni matunda ya viongozi wa CCM akiwemo Rais Jakaya Kikwete, Mwenyekiti wa CCM Taifa, kutangaza kuanza kwa mchakato huu. Hatuwezi kuuzaa wenyewe mchakato halafu tukauhujumu wenyewe mchakato huo.

Itakumbukwa umezuka utamaduni mbaya kwa baadhi ya Wabunge wa CHADEMA kutumia Bunge kama jukwaa la kuwashambulia isivyo sawa watu ambao hawana fursa ya kuingia Bungeni kujibu mashambulizi hayo. Utamaduni huu ni wa hovyo unakiuka haki za msingi ambazo zinataka mtu anayetuhumiwa/kushutumiwa apewe fursa ya kusikilizwa. Watanzania lazima tuukatae utamaduni huu.

Hivi karibuni baadhi ya Wabunge wa CHADEMA wamefanya vitendo vya aibu vilivyowakera sana Watanzania. Hili bado limo kwenye akili na midomo ya watu na sasa Chadema wanatafuta namna ya kuficha aibu yao(nitoke vipi) kwa kurukia hoja ya Mabaraza, kuzusha na kushutumu watu kwa uongo uliokubuhu.

Vituko vyote hivi vya Chadema vimeongezeka baada ya katibu mkuu wa CCM hivi karibuni mjini Morogoro kutoa maelezo ya kina na hoja nzito dhidi ya ukibaraka wa Chadema kwenye suala zima la mchakato wa Katiba.

Nchi nyingi hasa za Afrika zilizokumbwa na machafuko moja ya ajenda kubwa ilikuwa ni swala la katiba mpya. Sasa hapa nchini Chadema wanaona watanzania wanaendelea na mchakato bila machafuko wanakosa majibu kwa mabeberu wanaowafadhili kuchafua nchi yetu, ndio maana kila kukicha wanakuja na visa na vituko kusumbua mchakato wa katiba.

Walianza kwa kukataa matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 ikiwemo kutomtambua rais. Wakatangaza hadharani nchi haitatawalika kisa wamenyimwa ridhaa na watanzania. Mchakato ulipoanza wa katiba mpya wabunge wao wakazira na kutoka nje ya bunge, baada ya muda wakarudi.

Juzi bungeni wametishia kujitoa kwenye mchakato wa katiba ifikapo tarehe 30/04/2013, leo ni tarehe 05/05/2013!! Wamezoea kutishia nyau, tumechoka na vitisho vya vibaraka hawa. Tunapongeza msimamo wa Tume ya mabadiliko ya Katiba kwa kupuuza hoja ya kufuta mabaraza ya katiba. Chadema wakisusa na wasuse tu.

Tunawasihi watanzania wote wapuuze utoto na ukibaraka huu wa Chadema kwani ugonjwa wao tumesha ufahamu WANAUMWA KIFAFA CHA SIASA. Kila ugonjwa huu ukipanda wanatupa mateke sana. Tuwaombee ipo siku huenda mwenyezi Mungu atawarehemu watapona.

mkuu hii kazi ya nani?
 
Back
Top Bottom