Taarifa ya ajali ya Treni katika eneo la Bahi jijini Dodoma

Mwaka jana nilisafiri kwa treni kwenda moshi, treni ilitarajiwa kufika saa 2 asubuhi lakini tulifika saa saba mchana. Sababu ya kuchelewa ilikuwa ni kusimama simama kwa treni kisa NYASI ZIMEFUNIKA RELI hasa baada ya stesheni ya Korogwe.
Maana yake hata kiberenge hakikupita kukagua hio reli kabla ye safari yenu sio mkuu?
 
Mwaka jana nilisafiri kwa treni kwenda moshi, treni ilitarajiwa kufika saa 2 asubuhi lakini tulifika saa saba mchana. Sababu ya kuchelewa ilikuwa ni kusimama simama kwa treni kisa NYASI ZIMEFUNIKA RELI hasa baada ya stesheni ya Korogwe. Niliona ni uzembe wa stesheni masters wa vituo vile na kutokujali maisha ya abiria. Kufyeka nyasi tu kunawashinda?
Kuna mengi yanasikitisha, huwa namshangaa Sana yule Mr. katika Reli TV anavyoupindisha uhalisia ila Time Will Tell.
 
Mwaka jana nilisafiri kwa treni kwenda moshi, treni ilitarajiwa kufika saa 2 asubuhi lakini tulifika saa saba mchana. Sababu ya kuchelewa ilikuwa ni kusimama simama kwa treni kisa NYASI ZIMEFUNIKA RELI hasa baada ya stesheni ya Korogwe. Niliona ni uzembe wa stesheni masters wa vituo vile na kutokujali maisha ya abiria. Kufyeka nyasi tu kunawashinda?
Siasa inatumika badala ya weledi
 
SGR inakuja, kwa style hii hakika tutayaona makubwa. Treni inaanza safari kumbe hawajafanya ukaguzi wa njia. Huo mmomonyoko hapo unauliza mara mbili kujua chanzo cha ajali? Pathetic!

Tunaweza kujenga/kutengeneza vitu vizuri, usimamizi zero kabisa, wait and see hiyo SGR inayojengwa kwa trillions of shillings, utashangaa huo usimamizi wake. Futseke!
 
Duuh, Mungu awaweke mahali pema peponi.

Poleni wote mliokutwa na Mkasa huu
 
SGR inakuja, kwa style hii hakika tutayaona makubwa. Treni inaanza safari kumbe hawajafanya ukaguzi wa njia. Huo mmomonyoko hapo unauliza mara mbili kujua chanzo cha ajali? Pathetic!

Tunaweza kujenga/kutengeneza vitu vizuri, usimamizi zero kabisa, wait and see hiyo SGR inayojengwa kwa trillions of shillings, utashangaa huo usimamizi wake. Futseke!
Kunjani!

Maintenance ni shida, nimeangalia vituo vipya vya mabasi ikifika miaka mi5, vingi vitakuwa na hali mbaya, cha Dodoma ukuta wa jengo tiyari unakuwa mchafu!

Everyday is Saturday :cool:
 
Nimepitia ule uzi wa ajali inasemekana vifo ni vinne na mmoja wapo ni mfanyakazi wa treni? Imekuaje hawa waripoti vifo 3
 
Tutamuachia Mungu na hili litapita badala ya uchunguzi kufanyika wenye makosa wakumbane na mkono wa sheria na watu kujifunza kutokana na makosa.
 
Mwaka jana nilisafiri kwa treni kwenda moshi, treni ilitarajiwa kufika saa 2 asubuhi lakini tulifika saa saba mchana. Sababu ya kuchelewa ilikuwa ni kusimama simama kwa treni kisa NYASI ZIMEFUNIKA RELI hasa baada ya stesheni ya Korogwe. Niliona ni uzembe wa stesheni masters wa vituo vile na kutokujali maisha ya abiria. Kufyeka nyasi tu kunawashinda?
Hii ndio bongo.
 
Kuna hiyo treni iliua watu 500+ hapo bahi kituo hicho hicho.
Siku moja treni hiyo hiyo nimepanda hapo manyoni. Jamaa wanaweka abiria ndani ya mabehewa mi nimekutana na dereva analewa tu safari na carwosh yake nikamwongeza .
Na kweli jamaa kazichapa honi imepigwa ndo huyoo ndani ya kichwa cha treni.mi nimezama ngoma inaondoka.
E bana tulipita tu hapo Saranda taratibu akapakia, toka hapo ile treni nafkiri jamaa alifumua kila kitu sababu pia toka hapo ni mteremko mkali na tambarare mpk dom.
Treni inaita tu na kufonya, spidi usifanye mchezo ,ile spidi kuna nini wala nini mbele ni kupita tu.
Hatukupata ajali ila humo njiani hamna abiria anajua kitu. Mi najua huyu jamaa kalewa
 
YAH: TAARIFA YA AJALI YA TRENI B17 NA KICHWA CHA TRENI CHENYE NAMBA 9004

Dar Es Salaam Tarehe 3 Januari 2021

Uongozi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Unasikitika Kutangaza tukio la Ajali lilitokea Maeneo ya Kigwe-Bahi umbali wa Kilomita 508 Kutokea Dar Es Alaam na Kilomita 58 Kutokea Dodoma, Treni hiyo ilikuwa inatokea jijini Dar Es Salaam ikielekea Mikoa ya Tabora, Katavi (Mpanda), Kigoma na Mwanza ikiwa na Abiria wapatao 720.

Treni hii iliwasili Dodoma majira ya saa 9:15 alasiri na Kuondoka Dodoma majira ya Saa 11:40 Jioni. Treni hii iliwasili katika kituo cha Kigwe majira ya saa 12:25 Jioni na Kuondoka saa 12:27 Jioni.

Treni hii ilikuwa na Behewa 12 na kati yake Behewa 6 ndizo zilipata ajali Usajili wake ni kama ifuatavyo:
 TCB 3603 ya kwanza kutoka kwenye kichwa cha Treni
 TCB 3612 ya Pili kutoka kwenye kichwa cha Treni
 TCB 3652 ya tatu kutoka kwenye kichwa cha Treni
 TCB 3650 ya Nne kutoka kwenye Kichwa cha Treni
 TCB 3619 ya Tano kutoka kwenye Kichwa cha Treni
 Na ya Mwisho ni yenye Usajili wa Na. RCB 4526.

Mpaka sasa Majeruhi ni 66 na waliopoteza maisha ni watatu (3), akiwemo mtoto mmoja (1) na watu wazima wawili (2).
Majeruhi wamekwisha chukuliwa eneo la Tukio na wanaendelea na matibabu katika
Hospitali za Bahi na hospitali ya Mkoa wa Dodoma.

Uchunguzi wa Chanzo cha ajali unaendelea kufanyika na Shirika litaendelea kutoa Taarifa.

Uongozi wa Shirika la Reli unatoa Pole kwa Abiria wote waliofikwa na ajali, Majeruhi na Ndugu na Jamaa waliopoteza Wapendwa wao.

View attachment 1666115
Poleni
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom