Mchambuzi,
kuna haja ya kupigana kwa nguvu zaidi na kujizatiti zaidi ili kujihakikishia usalama wako.
1. Wanaoweza kukuhakikishia usalama wako ni haohao wanaotaka kukuua/kukudhuru. Na wametengeneza mazingira ili uone kuwa bila wao huna pa kuegemea. Their first victory is to instll fear in you to the point that you will be running from your own shadow.
2. Kuingiliwa bila ridhaa yako - Hakuna mtu mwenye hati miliki ya Taifa la Tanzania. Kumbuka kwamba akili yako na mawazo yako ndicho kitu binafsi ulicho nacho (na cha kujivunia ) hivyo hakuna mwanadamu yeyote mwenye right of access kichwani mwako/ na usimpe yeyote makazi kichwani mwako - maana hakuna anaeweza kulipa kodi ya pango kichwani mwako (hahahahahah)
Hivyo baada ya kushindwa kuingilia akili yako, wanataka ubadili yale yanayotoka kichwani mwako (yaani wanakuamuru ubadilishe hasa wakikuambia kuwa hawayapendi unayosema/unayoandika/unayosimamia.
Ni vigumu kuamini kuwa utakua salama hata ukihamia chadema maana maadui wa mawazo/misimamo yako wako kila mahali. Naamini kuwa salama yako itatokana na ni kiasi gani utafanikiwa kujizungushia wigo wa wana mapinduzi wenye mawazo,misimamo,mioyo ya kupigania haki (people with convictions around you)kama wewe.
Maadui zako wakijua umezalisha maadui wao, watakutambua kuwa wewe ni sauti ambayo lazima waiheshimu.