Taarifa: Usalama Wangu Hatarini

kwa jinsi mambo yanavyoenda nakushauri kama unaweza ondoka nchini kwa muda. Bado waweza endeleza harakati zako hata ukiwa nje; I feel for your life Mchambuzi
 
Last edited by a moderator:
Ukiingia kundi la wachawi utakula nyama ya watu tu!
 
Wauwaji utawajua tu. Kama wanatania vile ila wakikukuta kwenye kikona kibaya kwa usalama wako, utajua walivyo Madentist Wazuri na walivyo wazuri wa kufanya Nails Wax. Hii Tanzania, Tembo na Wapinzani wapo kwenye kapu moja, meno yenu ni haki yao.
Wewe taja majina bana acha kubeep watu.
 
Hatari kwa kweli,ila Mungu atakupigania mkuu
 
Kwa hali ilivyo ya CCM , kujaribu kuibadili ukiwa ndani ya chama ni kama unafanya suicide. Tafakari , chukua hatua!
 
Wauwaji utawajua tu. Kama wanatania vile ila wakikukuta kwenye kikona kibaya kwa usalama wako, utajua walivyo Madentist Wazuri na walivyo wazuri wa kufanya Nails Wax. Hii Tanzania, Tembo na Wapinzani wapo kwenye kapu moja, meno yenu ni haki yao.
Kuna mmoja humu ameingia na unga wake.
 
Am I dreaming or what? Its really you and not somebody stole your password?


Umeelewa sasa
 
wewe taja majina bana acha kubeep watu.

tulia kijana unahusika nini?? Maana kama mliweza kwa nyerere (r.i p) nyie ni watu hatari sana kwa nchi hii hamna huruma kabisa, ila mjue nanyi siku yatawakuta tu duniani sote tunapita, pesa za lumumba zisikutie upofu kijana ushindwe kuangalia maisha ya watz walalahoi wanaokufa mapokezi kwa kukosa dawa, wanaoshindwa hata kulipa 20,000 ya ada ya watoto waO, wasioijua kesho yao, wanaokufa kwa njaa, mmeharIbu elimu kwa kuwa wakina mwanaasha wenu hawasomi hizi st,kata.
 
Pole Mchambuzi ..........intimidations kama hizo hazikosekanagi. Kuwa makini ila baada ya kusema hivi watakupotezea. Badili ID ndelea na kazi
 
POle sana mkuu Mchambuzi. Tuweke dua zetu pamoja ili Mungu akusaide kuepukana na njama hizo za shetani na wajumbe wake. Naamini Mungu atakulinda kwa sababu unafanya kazi njema
 
Last edited by a moderator:
Mchambuzi tunakuombea sana kwa kweli mada zako unazozimwaga hapa JF siku zote zimekuwa na mafunzo mapana na yenye lengo la kuweka siasa za ushindani katika mizania zilizo sawa,
Mchambuzi tunajua wewe umetanguliza uzalendo ukijua kwamba vyama ni platform ya kufikia malengo ya siasa ya waumini wa sera fulani hapa nchini lakini kuna mambo ya msingi ya kujenga nchi na maendeleo yake ambayo huwa ni zaidi ya kuangalia vyama na sera zake hayo ndio ambayo wewe umesimamia

Ni kweli kabisa kwamba kwa sasa tulipofikia kwenye nchi hii kuna ambao wameharalisha kwamba kwenye nchi hii kuna kikundi cha watu wenye haki ya kuzungumza na wengine kusikiliza ,lakini pia pasiwepo na nafaasi ya kuwajibu au kutoa mawazo
Nchi yetu tunakokwenda lazima vijana wote tukubaliane kulinda nchi yetu kwa namna yeyote vile bila kujali itikadi zetu za vyama,juzi kwenye TV ya ITV kulikuwa na vijana wawili waliokemea uroho uliopitiliza wa wana CCM kutaka madaraka kwa namna na njia zozote zile waliasa kuwa wana CCM wengi sasa hivi wameacha kuhamasisha maswala ya maendeleo na kuboresha maisha ya wananchi na kukazania zaidi kujilimbikizia mali na kujiweka sawa kisiasa kwa sababu ya madaraka hii hali ni hatari sana
hasira za wananchi ni kubwa kupita kiasi sasa hivi angalia vipindi vyote kwenye TV awe Raisi,Abdala BUlembo, Chiligati, wanahubiria watu wawili watano kumi ,manake wananchi hawaridhiki nao
mungu akupe ulinzi kwani upo kutetea nafsi
 
Hahahaa, Majebere, ningelifurahi kama ungelikuwa Mgogo kweli ili Nikutukane Kinyamwezi.

Yaani kwa Sababu kaka Chenge alikuwa na Unga bungeni basi kila Mnyamwezi amekuwa mtu wa kuja na Unga?

Msaidie kijana bana na acha kufanya masihara kwenye maisha ya mtu, si jambo la kuchekesha hili ila la kutisha.

Omba Mungu kijana, USIKU NA MCHANA ili yasije yakakutokea kutishwa maisha. Mimi nilishawahi kutishwa ila baadaye jamaa wakasema walikuwa wanatutania. Nilikuwa darasa kama sikosei la tano miaka mingi sasa ila hadi leo nakumbuka kila kitu kama ni jana. Temea chini Majebere na wala siombei yaje yakukute.
Kuna mmoja humu ameingia na unga wake.
 
Hivi Tanzania ndo tumefikishwa hapa....??!! Kwamba mnataka wapinzani walioko nje ya CCM pekee? Hao wa ndani hamuoni kwamba watawasaidia kujirekebisha mnapokosea? AU NDO AFUATE VIKAO VYA CHAMA?
Mchambuzi pamoja na kwamba POLISI wanaweza wasisaidie, basi fanya kama Mwakyembe, peleka taarifa hiyo POLISI ili in case yametokea yasiyotarajiwa wewe unakuwa umeshafanya taratibu zote zinazohusika katika kutoa taarifa kama hii. Unaweza usiwe na imani na polisi lakini better do report it..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…