Taarifa: Usalama Wangu Hatarini

Hii thread ni muhimu sana, ila kama kawaida yetu kuna watu wameamua kuivuruga kwa sababu wanazojua wenyewe; huenda wanatumika, au wanajitumia vibaya

if it was my wish, ningesema ipelekwe kule jukwaa la great thinkers ili kupunguza impurities... this thread deserves great mind to discuss, maana mleta mada sio Timing wala wale vipandikizi, he is a real deal na has been mkweli since day one bila ushabiki wa kipuuzi-puuzi
 
Magamba hoja zao hazifichiki hivi huwa mnapambana ili mpate nn ma cowards?na kutwa mzima humu!HV humu si huwa tu mnaishia kupata stress?

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Hapo penye nyekundu,wanawaambia viongozi wetu ukweli unaouma.
Ukweli gani huo kwao unafikiri mpaka chama kiamue kuwapa vitisho.

Kama ameweza kuja JF na kusema yaliyo moyoni mwake, basi angemalizia na kuwataja hao anaodai ana uhakika nao ndio wanaotishia maisha yake. Nje ya hapo ni kama kupika majungu.
 

Mkuu watu walishakupa tahadhari siku nyingi, huko nyuma, kuwa CCM hakukufai na hata mimi binasfi nikisomaga mabandiko yako niliamini iko siku tuu watachoka kuchokonolewa. Japokuwa napenda kusoma mabandiko yako na ninafurahia kuona kuna vijana wenye uelewa wa hali ya juu kama wako katika mambo ya siasa na itifaki lakini hutakiwi kuomba simanzi hapa JF kwakuwa watu walishakuonya.

CCM siyo chama cha wafanyakazi na wakulima tena ni kundi la majangili ambalo linaweza fanya lolote kusafisha njia ili waendeleze uhalifu wao, watu walimuondo mwasisi itakuwa wewe? Nilishawahi sema huko nyuma kuwa nikigundua ndugu wa damu ni mkereketwa wa CCM katika zama hizi basi simuhesabu kama ni ndugu yangu na nitakuwa na muangalia kwa jicho la tatu. Hawa watu wanaopiga makelele hapa kuitetea CCM wengi wao ni wachumia tumbo wapo kimaslahi zaidi. Sijui unataka kuwa shujaa huko CCM au vipi, lakini hayo ni maji ya shingo, huwezi kumshida papa kuogelea.
 
Last edited by a moderator:
wananchi wapo na wewe mkuu, a general conclusion humu ni hama chama ASAP na ongeza tahadhari mkuu.we are praying for you.
 
Wewe siyo mnyakyusa!
tenende kama hii pia ni ID ya propaganda ya CDM basi chama kimekosa waongozaji, kitengo cha wapambanaji wa mtandaoni kilikuwa na afadhali alipokuwepo Ludo siku hizi vijana mnajiandikia tu ilimradi muoneshe idadi ya posts kwa mabwana zenu.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mchambuzi kuwa makini msitu wa pande unakulilia!
 
Last edited by a moderator:

Kweli mkuu! Watu wanaleta utani wa MMU hapa kwa mtu mwenye mchango uliotukuka hapa JF kama Mchambuzi!

Dawa si kuihamisha bali Mods kujitahidi kuondoa post za mizaha kwa heshima ya Mchambuzi!

Wengine amekuwa mwalimu wetu humu!
 
Alafu kuna wachangia wanajiita wanaCDM wanaandika utumbo hadi inakera yaani bora usome post ya Ritz kuliko hawa watoto wanaojiita makamanda na post zao zilizojaa comedy kwenye mambo serious!
 

Kumbe na wewe unaamini kuwa kitu wanachoamini wengi ndio kiko sahihi!!!

Dunia ya kisasa imeshaachana na imani ya namna hiyo miaka mingi iliyopita na kuiacha kuitumia kwenye chaguzi za kisiasa tu. Kama huu ni uchaguzi wa kisiasa basi wengi wako sahihi lakini kama ni hii ni forensic science basi wengi wameenda "kichwa kichwa"...
 
Mlimpitisha kwa mbwembwe, kura nyingi, na mkampa majina mazuri eti hendsam....atapendeza kwenye noti. Kumbe roho ni nyeusi kuliko giza!! Nyumba ya magogoni imekuwa jumba la wauwaji, wezi wa nyara za taifa, na mabaya mengine lukuki.
 
Acha kuwa na mashaka na usalama wako luka ukuta njoo kwa makamanda CDM upate salama yako huko kumeoza hakufai kukaa mtu mwenye pua zinazo nusa harufu mbaya.
 
Duh! Hivi nitakosea nikisema kwamba kwa maelezo yako unauthibitishia UMMA wa WATANZANIA kuwa sera ya kutesa, kuua na kung'oa kucha na meno imeanzia ndani ya hicho CHAMA ulichopo!
Kaa chonjo...........................
 
Mkuu pole sana na uwe makini na wana CCM wenzako,kwani huwa hawapendi kuambiwa ukweli,wanachokiamini wao ni zidumu fikra za mwenyekiti.
 

baba ubarikiwe pamoja na tumbo lililo kuzaa
 
Fuata taratibu za chama chenu za kukosoana kwa kutumia vikao halali.
 
Uliyoandka ni mazur ya kujifunza kwa vyama vyote. Hili la kutishiwa wahi polisi toa taarifa ili kujihami na wang'oa kucha.

duh polisi wapi sasa hatuna polisi Tanzania.. tuna policcm utashangaa badala ya kusaidiwa ndo wanambambika madawa ya kulevya... mie hamna mtu ninaemuogopa kama polisi siku hizi bora ni kutane na jambazi nipambane nae mwenyewe...khaaaaaaaaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…