Taarifa: Usalama Wangu Hatarini


Umenena vyema sana, ni bora pia akaweka bayana hao wanaomtishia ni akina nani ili jamii iwatambue kwani hata akitoa taarifa kwa vyombo vya usalama kama polisi hawatafanya lolote la kumsaidia zaidi ya kumbeza kama ambavyo wamewafanyia wengine.
 
Pole sana,
Chukua hatua za haraka za kujihakikishia usalama wako. Baada ya hapo wasiliana na wadau wengine wakusaidie kuwa salama na kuendeleza unayodhani ni azma yako kwa faida ya nchi yako. Karibu Tanzania: Mungu akulinde.

Naona wahanga mnafarijiana! Poleni sana kwa kuwindwa kama ndege.
 


Tatizo la ccm pana watawala hakuna viongozi,watawala lengo lao ni kuendelea kutawala bila kubugudhiwa.Unachokifanya wewe ni chema ktk uongozi lakini ni kibaya katika watawala wa ccm.Ushauri wa bure njoo huku Chadema kwenye viongozi.
 
du!pole mchambuzi....usitishike wala kusita kuusema na kuusimamia ukweli..kwani utakuweka huru...Ni vizuri unawambia hali halisi vijana wenzako ccm...maana wengi wanaishi gizani.. I wish ccm kungekuwa na vijana wenye msimamo kama wako....maana simwoni hata mmoja...wengi wanaishi kwa illusions..wakati wakubwa zao wanaitafuna nchi....
 
Mchambuzi said:
mbali ya kupokea vitisho,pia nimedokezwa na vyanzo vyangu vya kuaminika sana kuhusu mpango uliopo wa kunidhuru,hivyo niwe makini hasa in the public arena na nimetajiwa wahusika kwa "majina" na "kitaasisi"!
Mkuu muda si mrefu wanausalama watakutafuta,wamo humu huwa wanapita naskia.
 
Pole sana Mchambuzi. kwa kweli katika medani ya siasa hakuna mahali salama aslimia mia. Umonnyesha msimamo mzuri tofauti na wengine wanaoikejeli Chadea kwamba itakufa kabla ya 2015.Watanzania wanataka uongozi bora si majina. wanataka maendeleo si propaganda na ahadi hewa.wanataka amani si ugaidi na hujuma. wanataka kuishi si kuuwawa. ifikapo2015 wananchi watakuwa na maamuzi tayari. kila atakae uongzi aanze kujipnaga vema azichange kaata zake vizuri nafasi ipo kidogo...
 
fanya haraka kuwataja kabla CDM hawajakuteka
 
Mungu akupe Nguvu, na kukulinda na Wabaya wote, wapate kushindwa, upate kulitumikia Taifa letu kwa moyo na uzalendo wote, uushinde udhalimu, uoga na majaribu yote.
Kikubwa umweke Mungu Kwanza.



 
Mkuu umemsoma vyema lakini?
mbali ya kupokea vitisho,pia nimedokezwa na vyanzo vyangu vya kuaminika sana kuhusu mpango uliopo wa kunidhuru,hivyo niwe makini hasa in the public arena na nimetajiwa wahusika kwa "majina" na "kitaasisi"!
 
Pole kijana, sioni kama watu wanafanya siasa ndani ya ccm zaidi ya vitisho tu, haya ndo aliyochaguliwa nayo kinana?
 
Hapa li-KOVA na mimacho yake yote JF. Kesho utasikia anasema CHADEMA.
 
Hao wanaokutishia waweke hadharani ili kuwapunguza kasi ya utekelezaji na badala yake waanze kujipanga upya. Mchawi mpe mtoto alee, peleka taarifa polisi. Peleka maelezo yako pia kwa Hellen Kijo Bisimba na mwisho ujisaimishe kwa amiri jeshi. Yawezekana ukapata rehema yake akakulinda sambamba na vijana wake wa kazi. Unaweza ukaona ninakushauri mambo ya kuchosha lakini gharama zake ni ndogo kuliko maisha yako.
 
Jamii yetu inadanganyika kirähisi sana.
Critical thinking haipo kabisa!!!
Ndio maana misururu ya wagonjwa ilijaa Loliondo...

Chifu, misisuru hiyo ilifunguliwa na kaka mkuu, alijifanya yupo mapumzikoni, lakini akaamua kwenda 'kudanganyika' na kikombe cha jero.
Kaka mkuu mjanja sana, alitumia ukaribu wa Olduvai Gorge na Samunge kutokomea kwenye kikombe bila raia wengi kujua.

Baada yake, misusuru ya mawaziri (Lukuvi, Magufuli n.k.) vigogo wa polisi, wakuu wa mikoa na wilaya, wabunge n.k. ilionekana.

Katika hilo chifu ZeMarcopolo nakubaliana nawe. Ni hatari kwa taifa kuongozwa na viongozi wasio critical thinkers, wanaodanganyika kwa kikombe cha jero.
 
Last edited by a moderator:
Pole sana mkuu Mchambuzi kwa hivyo vitisho unavyopewa. Tunakuombea usalama. Wewe ni mmoja kati ya vijana wachache ambao ninawakubali kwa kusimamia ukweli na kuwa na mapenzi ya kweli kwa nchi yetu ya Tanzania.
 

Chief hii na usalama wa Mchambuzi unahusiana vipi?

Wengine maneno yenu yanauzito humu msihamanike kuandika bila kueleweka wengine tukajitafsiria tu!
 
Last edited by a moderator:
Pole sana Mkuu ujichunge sana na pia kuacha kabisa matembezi ya usiku ukiwa peke yako.
au ikibidi kutoka usiku awe anachukua kabisa dawa ya ganzi na wembe wa kukatia kucha!!natania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…