Taarifa: TRA kugawa mashine za EFD jijini Dar

Taarifa: TRA kugawa mashine za EFD jijini Dar

Dai risiti toa risiti. Acheni mambo mengi. Wageni wamekimbia kwasababu nyingi. Huko nyuma nahisi walikua wanaingia bila passport ssahv ni muhimu wakaguliwe, walikua wanakwepa kodi sasa hv wametafta kwingine ambako hapajabana kama hapa. Af cha mwisho na cha msingi san sana, walikua wananunia sukari sahv haipatikani
 
Tatizo sio EFD machine tatizo watu wanachanganya bei na faida,umeambiwa weka gharama na faida halafu pngeza Vat juu ili upate bei ya kuuzia.mimi nimekuwa natumia EFD machine toka 2012 sijawahi kuona tatizo kwenye mfumo tatizo lipo kwa mimi kushindwa kufanya biashara na wenzangu ambao wamekataa kufuata mfumo huu.
Wafanyabiashara wengi wanaigiza mizigo bila kulipia kodi ndio maana hawataki machines.
 
Tatizo sio Mashine za EFD ,tatizo ni mfumo mzima wa uendeshaji wa hizi mashine .Hizi Mashine zinatambua mauzo tu na hazitambui gharama ,kwa maana ya kuwa utatozwa kodi ktk mauzo iwe umeuza kwa hasara au kwa faida kiduchu.

Sheria inakutaka mfanya biashara kutoa taarifa ndani ya SAA 24 kama hutofungua biashara,na faini ni mlioni 3 pamoja na kifungo juu au moja kati ya hizo.Sasa tujiulize unapopatwa na dharura zilizo nje ya ubinadamu kama ugonjwa kufiwa au vyovyote vile ni namna gani unaweza kukabiliana na hilo tatizo.

Sasa hivi Kariakoo hapafai ,T.R.A wanakamata wafanya biashara walioandika risiti za mkono(Za kitabu),wanamkamata mnunuzi na wanakamata mzigo...Wageni wamepungua kutokana na usumbufu huu ..

Zipo kero nyingi na Serikali imeziba masikio ,unaweza kuzuka mgogoro tena wa wafanya biashara kama Serikali hii itaendelea kutia pamba masikioni...

Mgogoro? Subutuu! Hakuna mgogoro
 
Ndo udhaifu wa kutumia efd mkuu. Sasa tutalalamika hadi lini? Waathirika wakuu ni super dealers na semi super dealers. Kwa nini kupitia jumuiya zao wasifungue kesi mahakamani kuomba ufafanuzi wa mahakama?
Nashangaa sana kwa nini mwanasheria wa jumuia yao halioni hili may matter of time au uelewa wa haya mambo.
Sio mbaya kama yupo humu na akipita hapa anaweza jua wapi pa kuanzia.
 
Tokea mwanzo mashine ni bure, tatizo elimu haikutolewa ya kutosha, na pia kutokua na tabia ya kuuliza wahusika sahihi, information nyingi tunapata mtaani ambazo zinakua si sahihi na siasa pia zikaingia tena juu yake.

Sheria ya EFD inavyosema, mfanyabiashara anaponunua mashine ya efd (moja au zaidi) kwa mara ya kwanza atarudishiwa pesa yake yote kwa njia ya kodi pindi atakapoanza kuitumia. Mfano alitakiwa alipe kodi milioni moja, na kanunua mashine laki nane basi atatakiwa kulipa kodi laki mbili tu. Kwa wale ambao huwa wanakwepa kodi, ndio watakua hawana namna ya kurejesha hela yao.
Nami nilikuwa najua hivyo lakini watu hawakuelimishwa ndio maana wakawa wanagoma.
 
Mkuu hizo hesabu za wapi?, TRA wanakata 18% ya mauzo yako na siyo 18% ya faida yako na ndiyo ugomvi na wafanyabiashara unapoaanzia
umesomea nini mkuu labda tuanzie hapo kukusaidia.
 
Nimesafiri nchi mbalimbali nimeona baadhi ya nchi za africa zinazosimamia ukusanyaji wa kwa mashine mpaka kwa mama lishe,machinga nk,na wananchi wamezoea na ni jambo la lazima Hivyo basi watanzania lazima tubadilike kila unaponunua bidhaa yoyote dai risiti na mfanyabiashara toa risiti kwani kuna ugumu gani?
Mashine za EFD kutolewa bure mimi binafsi ninamuunga Rais
Taja hizo nchi.
 
Back
Top Bottom