Kweli mtu aliyekuuzia kukufundisha na kwanini TRA wasifundishe walipa kodi ili aya malalamiko yasijirudie tena?
Hiyo nadhani itakua ngumu kidogo, ila wana idea nini cha ku expect kutoka kwako. Mashine zipo za aina nyingi na zinatofautiana kwenye jinsi ya kutumia, ila mwisho wa siku matokeo ni yale yale kwa maana report zinazohitajika.
Ni sawa na kuomba TIGO wakufundishe wateja kutumia simu zao,
Ni jukumu la supplier, aliyemuuzia mteja mashine kumfundisha kutumia mpaka aelewe kabisa, kwa maana mteja amelipia huduma hiyo. Hela aliyolipa kununulia mashine, ina jumuisha mafunzo na service kwa mwaka mzima.