Taarifa rasmi ya kusitisha mgomo kutoka chama cha madaktari 10/03/2012

Ndo maana nampenda Lowassa alipoona kelele alikaa pembeni, Mponda and Nkya should learn from the great Laigwanani!
 
Nafahamu msimamo wenu ulikua kwamba hamtaji mazungumzo hadi mponda na huyo mama watimuliwe...sasa iweje mmeruhusu iyo stej ya pili ya mazungumzo kabla hiyo ya kuwasimamisha kutekelezwa..unless j3 jk aseme amewasimamisha tofaut na apo hatutawaelewa...ikulu juice at work!!n
 
Baada ya Gahwa na Juisi za tende, hizo ni ngonjera. Ukweli unabaki kuwa ukweli, madai yenu mliahidiwa pia kushughulikiwa na Pinda na yanashughulikiwa, kwa hilo hamna jipya.

Nyinyi mlikazania Mponda na Nkya wafukuzwe kazi, sasa yamewashinda ngonjera imedilika na kuwa kama watoto wadogo mnakuja eti Nkya kafukuzwa uanachama wa MAD na Mponda na Nkya ni "maadui wa madaktari" "hatuwapi ushirikiano|, Huo ni utoto na ujinga.

Mkubali tu kuwa mliyoyakuta Ikulu hamkuyategemea na yamewanyamazisha na Mponda na Nkya wanadunda kama Waziri na Naibu Waziri. Huyo ndio Jakaya Mrisho Kikwete, kaweza kuwaunganisha Wapemba na Waunguja itakuwa nyinyi?

Umewashuka.

ni MAT kaka sio MAD.....usiharibu jina la Chama chetu
 
Hongera kwa Mhe. rais kujali maslahi ya wataalamu na pia nimeipenda hoja ya kwanza kuwa mtaalamu si mashine ya kufanyia kazi. Ni mategemeo yangu serikali itatekeleza ahadi zake mapema zaidi kwa afya bora ya wananchi
 
Baada ya Gahwa na Juisi za tende, hizo ni ngonjera. Ukweli unabaki kuwa ukweli, madai yenu mliahidiwa pia kushughulikiwa na Pinda na yanashughulikiwa, kwa hilo hamna jipya.

Nyinyi mlikazania Mponda na Nkya wafukuzwe kazi, sasa yamewashinda ngonjera imedilika na kuwa kama watoto wadogo mnakuja eti Nkya kafukuzwa uanachama wa MAD na Mponda na Nkya ni "maadui wa madaktari" "hatuwapi ushirikiano|, Huo ni utoto na ujinga.

Mkubali tu kuwa mliyoyakuta Ikulu hamkuyategemea na yamewanyamazisha na Mponda na Nkya wanadunda kama Waziri na Naibu Waziri. Huyo ndio Jakaya Mrisho Kikwete, kaweza kuwaunganisha Wapemba na Waunguja itakuwa nyinyi?

Umewashuka.


Jamani hapa hatutafuti mshindi..kama wanarudi kazini ni kheri. Cha msingi hapa serikali ni kujua kuwa kuna fani si za kuchezea...Wamesema vizuri kuwa Dr unaweza kutumia dola na nguvu kumrudisha kazini kakini nature ya kazi yake uwezi kumlazimisha kufanya kazi. Tusipoangalia na statement yao hii...Kupasua kichwa badala ya mguu sasa itaanza kuwa normal issue....

Na kama wametangaza kuwa hawatoa ushirikiano na hao wamaziri basi lazima watang'oka tu... Medicine si fani ya kuchezea....Kuna fani zingine unaweza kumlazimisha mtu aende kazini na akafanya kazi si Doctors (Life & Death).
 
Pia tunawashukuru madaktari wote kwa mshikamano wetu tulioonyesha na tunaomba mshikamano huu uendelee daima.

Madr sasa kazi kwa kwenda mbele mgomo umekwisha.
 
Hongereni madaktari kwa kuwa flexible na kushughulikia issues zaidi kuliko kutafuta ushindi usio na tija kwa gharama ya watu maskini wa Tanzania. JK,kama waziri mkuu, waziri wa afya na wasaidizi wake hawawezi kufanya kazi, kwanini unawapa madaraka mpaka leo?
 
Good.

Kipengele namba 1, 2 na 3 vinakinzana kabisa na kipengele na 4.

4. Jamii itambue kuwa madai na hoja kuu za madaktari ni kwa ajili ya faida ya madaktari na familia zao,yakiwemo mazingira bora ya kufanya kazi mjini na vijijini, na kuboresha afya za watanzania kwa ujumla. Pia vifaa na dawa ziwepo mahospitalini zinakohitajika.
 
RIPOTI KWA VYOMBO VYA HABARI.

UTANGULIZI
Baada ya kikao cha madaktari kilichofanyika leo tarehe 10/3/2012. Madaktari nchini kupitia chama cha madaktari Tanzania (MAT), tunapenda kutoa ufafanuzi ufuatao:

... 1. Jamii ielewe kuwa daktari kama binadamu mwingine anayefanya kazi Tanzania ana mahitaji muhimu (basic needs) na mahitaji ya kijamii (social responsibility) na hivyo si chombo cha kufanyia kazi (Machine).

2. Pia Daktari ana haki ya kupata ujira unaomfaa kutokana na kazi anayofanya na ana haki ya kuacha kazi muda wowote iwapo ataona kazi hiyo ya udaktari haimpi ujira wa kutosha na heshima ya kuendesha maisha yake.

3. Pia jamii itambue kuwa daktari anaweza kulazimishwa kurudi kazini lakini hawezi kulazimishwa kufanya kazi. Matokeo ya kulazimishwa yanaweza yasiwe mazuri kwa wale watakao hudumiwa.

4. Jamii itambue kuwa madai na hoja kuu za madaktari ni kwa ajili ya faida ya Watanzania wote,yakiwemo mazingira bora ya kufanya kazi mjini na vijijini, na kuboresha afya za watanzania kwa ujumla. Pia vifaa na dawa ziwepo mahospitalini zinakohitajika.

5. Pia tunawashukuru madaktari wote kwa mshikamano wetu tulioonyesha na tunaomba mshikamano huu uendelee daima.

TAMKO LETU:

JANA TAREHE 9/3/2012, TULIKUTANA NA MH. RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MH. DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE. TULIMWELEZA HOJA ZETU, AMBAZO ALIZIELEWA NA ALIAHIDI KUZISHUGHULIKIA KIKAMILIFU. TUNA IMANI SANA NA MH. RAIS KWAMBA HATATUANGUSHA.

KUTOKANA NA HILO, TUNAPENDA KUUTANGAZIA UMMA WA WATANZANIA KUWA TUNARUDI KAZINI RASMI KUANZIA LEO TAREHE 10/3/2012, WAKATI MHESHIMIWA RAIS AKISHUGHULIKIA MADAI YETU.

PIA WAKATI MADAI YETU YAKISHUGHUKLIKIWA TUNAPENDA KUSEMA KUWA HATUNA IMANI NA WAZIRI WA AFYA MH. DR. HAJI MPONDA NA MH. DR. LUCY NKYA, NA KUWA TUNAMSIMAMISHA RASMI UANACHAMA WA MAT MH. DR. LUCY NKYA.

MADAKTARI TUNATAMKA WAZI KUWA WAZIRI WA AFYA DR. HAJI MPONDA NA NAIBU WAKE DR. LUCY NKYA NI MAADUI WA MADAKTARI NA SEKTA YA AFYA KWA UJUMLA HAPA NCHINI NA TUNAAHIDI KUTOKUWAPA USHIRIKIANAO WA AINA YOYOTE WA KIBINAFSI AU WA KIUTENDAJI.

SOLIDARITY FOREVER.
RAIS(MAT)

Tangu mwanzo hata mimi nilitoa hii suggestion kwamba hiyo hapo kwenye red ni suluhisho mbadala la kuonyesha kuwa mnataka hao watu waachie ngazi badala ya hili mlilotaka kulifanya!!Thanks madaktari kwa kumaliza mgomo,mungu awape moyo wa ustahimilivu na uvumilivu katika kutusaidia walalahoi wa tz!!
 
MADAKTARI TUNATAMKA WAZI KUWA WAZIRI WA AFYA DR. HAJI MPONDA NA NAIBU WAKE DR. LUCY NKYA NI MAADUI WA MADAKTARI NA SEKTA YA AFYA KWA UJUMLA HAPA NCHINI NA TUNAAHIDI KUTOKUWAPA USHIRIKIANAO WA AINA YOYOTE WA KIBINAFSI AU WA KIUTENDAJI.
Hapa ndiyo wachezaji wa chess tunasema checkmate...! Yaani hata JK aki stall kuwafukuza hawa jamaa sasa ,mwisho wa siku ni lazima waondoke.
 

Uadui wenu na akina Nkya na Mponda unawahusu nini wagonjwa? Wap****vu kabisa nyie!
 
Mkuu amejitahidi kwa wakati huu maana mara nyingi heka heka zinapotokea huwa anaenda nje ya nchi kukimbia stress.
 
Hongereni madaktari kwa kuwa flexible na kushughulikia issues zaidi kuliko kutafuta ushindi usio na tija kwa gharama ya watu maskini wa Tanzania. JK,kama waziri mkuu, waziri wa afya na wasaidizi wake hawawezi kufanya kazi, kwanini unawapa madaraka mpaka leo?

Madaktari ndio walioshindwa na si hao Mawaziri, nna kuhakikishia hao Mawaziri wamefunga mianya ya ubadhirifu mingi kwa madaktari na ndio sababu za kuchukiwa, hakuna zaidi. Na Ikulu wakapewa taswira kwa mbali, wameelewa kuwa huwezi kuwa na dhambi halafu ukajifanya wewe ni msafi na fulani ndio mchafu wakati hujaonesha huo uchafu wake uko wapi.

Sijasikia hao MAT wakisema Mponda au Nkya kafanya hiki na hiki na hiki kibaya na ndio sababu hatuwataki. Hawana lolote zaidi ya walitaka kuficha maovu yao Na wameoneshwa, eeeeh nyie hiki nini na hiki nini na hiki nini, sasa amuweni wenyewe mnarudi kazini na kutangaza kusitisha mgomo au mnaendelea na madai yenu ya kijinga na kubakisha yale ya awali mliokubaliana na Pinda? wenyewe wakasema basi, yaishe Mzee, sisi tunabakisha yale yale, tunaomba uyashughulikie Mzee, haya mengine yote basi, tumetubu. Unacheza na Serikali?
 
Pamoja na obovu wote wa JK
Lakini JK anakitu kimoja very unique....... ushawishi mnapokutana naye uso kwa uso.
He never failed in this

Hongera JK hongera Drs
Paulss, hiyo ni moja ya sifa kuu za JK, inaitwa "good convincing power"!.
Jana nilisema mahali, leo mgomo utakwishwa "unconditional"
JK Kiboko!.
 
Back
Top Bottom